Maisha Moja ya Pekee
“ALIZALIWA katika kijiji kisichojulikana sana, mtoto wa mwanamke wa maisha ya hali ya chini. Akalelewa katika kijiji kingine tena, ambapo alifanya kazi katika duka la seremala mpaka alipofikia miaka thelathini. Kisha kwa miaka mitatu alikuwa mhubiri wa kuzunguka-zunguka.
“Hakuandika kitabu chochote. Hakuwa na cheo chochote. Hakuwa na familia wala nyumba. Hakwenda chuo. Hakupata kutembelea jiji kubwa. Hakupata kusafiri [kilometa mia tatu na ishirini] kutoka alikozaliwa. Hakufanya yoyote ya yale mambo ambayo watu huhusianisha na ukuu. Hakuwa na barua za ustahili ila yeye mwenyewe.
“Alikuwa na miaka thelathini na tatu tu wakati umma ulimgeuka. Rafiki zake walimtoroka. Alikabidhiwa kwa maadui wake na akapitia hukumu ya dhihaka. Alitundikwa [mtini] katikati ya wezi wawili. Alipokuwa akifa, wauaji wake walipigia kura vazi lake, mali pekee aliyokuwa nayo duniani. Alipokuwa amekufa, alizikwa katika kaburi lililoazimwa kupitia huruma ya rafiki.
“Karne kumi na tisa zimekuja na kupita, na leo anaendelea kuwa mtu mkuu wa jamii ya ainabinadamu, na kiongozi wa maendeleo ya ainabinadamu. Majeshi yote yaliyopata kupiga miguu, na manowari zote zilizopata kuundwa, na mabunge yote yaliyopata kuwa na kikao, wafalme wote waliopata kutawala, wakijumlishwa pamoja hawakupata kuwa na uvutano juu ya maisha za wanadamu katika dunia hii kwa nguvu nyingi kama maisha hiyo moja ya pekee.a”—An anonymous commentary on the life of Jesus Christ.
[Maelezo ya Chini]
a Maelezo zaidi juu ya maisha hiyo ya pekee yanapatikana katika kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi, kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.