Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 7/8 kur. 13-14
  • Kutafuta Hazina ya Aina Tofauti

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutafuta Hazina ya Aina Tofauti
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Vifaa na Mahali
  • Mawe ya Kukusanywa na Watu Wasio na Ustadi
  • Mawe ya Aina Nyingine
  • Mwamba Mkubwa Ajabu
    Amkeni!—2007
  • Mfanye Yehova Kuwa Mwamba Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2024
Amkeni!—1993
g93 7/8 kur. 13-14

Kutafuta Hazina ya Aina Tofauti

KUTOKEA siku za zamani sana, watu wamekuwa wakithamini umaridadi wa hazina zilizogunduliwa za uumbaji zilizokuwa zimejificha duniani. Kwa mfano, Havila, mahali panapohusianishwa na Arabia ya kale, palijulikana sana kwa mawe ya shoham yenye rangi-rangi. (Mwanzo 2:11, 12) Au wazia ukimwona kuhani mkuu wa Israeli ya kale akiwa na bamba la chuma la kifuani lenye vito vya shoham, akiki, emeraldi, yakuti ya rangi ya manjano, na vito vingine—vyote vikiwa 12—vikiwekwa kwa dhahabu. Ni lazima lilikuwa ono lenye kuvutia kama nini! (Kutoka 28:15-20) Pia, wazia wingi wa mawe yenye thamani yaliyotumiwa katika kujenga hekalu katika Yerusalemu, liliwekwa wakfu kwa ibada ya Yehova. (1 Mambo ya Nyakati 29:2) Huenda vingi vya vito hivyo viling’arishwa mpaka vikang’aa kwelikweli. Magunduzi ya hivi karibuni ya kiakiolojia yanaonyesha kwamba maelfu ya miaka iliyopita, watu walitumia mashine sahili ya shinikizo ili kuendesha jiwe la kusaga la kung’arisha miamba. Kwa hiyo kazi yetu ya leo ya kukusanya miamba si jambo jipya.

Vifaa na Mahali

‘Nitahitaji vifaa gani kwa kukusanya mawe?’ huenda ukauliza. Nyundo ya mawe, yenye mwisho wa mraba kwenye upande mmoja na kuwa na ncha kwenye upande mwingine, ni muhimu kabisa. Karatasi ya kufungia mawe tuliyokusanya na mfuko wa kuyabebea yanatosha. Waona? Si vifaa vya bei ghali.

‘Nitaanza kutafuta mawe wapi?’ kisha unajiuliza. Mabonde na sakafu za mito ni sehemu nzuri za kuanza utafutaji. Kwa nini katika sehemu hizo? Kwa sababu visehemu vya mawe visivyo vya kawaida, vilivyoanguka kutoka kwa miamba mikubwa kwenye miinuko ya juu, vinaweza kufingirika kutoka mlimani kuelekea chini au kwenye kijito, vikilainishwa na kung’arishwa vikija. Katika mahali ambapo mito huungana na bahari, unaweza kupata mawe yaliyobebwa kwenye mlango wa mto na mawe madogo-madogo yakiwa yameletwa ufukoni kutoka kwenye miamba ya chini ya bahari. Sehemu nyinginezo zinazotoa uwezekano kwa wakusanya-mawe ni mahali ambapo ardhi imekatwa kwa ajili ya barabara na mahali machimbo yalikuwa na yakaachwa. Lakini uwe mwangalifu katika sehemu hizo. Sikuzote kuna hatari ya jiwe lenye kulegea kuanguka. Katika sehemu nyinginezo, huenda ukahitaji ruhusa kabla ya kuanza utafutaji wako.

Ikiwa unaishi katika Afrika Kusini au Brazil, huenda unaweza kufaulu kupata visehemu vya almasi. Mawe ya akiki na safaya [yenye rangi ya samawati] yanaweza kupatikana katika sakafu ya mito katika India, Myanmar, na Thailand, na emeraldi katika Kolombia, India, Afrika Kusini, na Zimbabwe. Katika Uchina na Japani, jedi (jiwe la kijani-kibichi) na jedaiti zinapenda kutumiwa sana kwa vito, madoido, na vichoma uvumba. Jedi inapatikana katika Myanmar, New Zealand, na Alaska, na vilevile Japani.

Mojapo kito chenye umaridadi zaidi ni opali (chenye rangi ya maziwa), namna ya silika isiyopenyezwa na nuru. Zikiwa zinapatikana katika Australia na Meksiko, opali zina rangi mbalimbali zenye kuvutia—rangi kidogo ya nyekundu kama moto, manjano, kijani, na buluu. Opali si ngumu kwa kulinganishwa na mawe mengine na mara nyingi hupakwa kidogo kwa quartz (jiwe gumu jeupe) ili kuzuia isikwaruzwe.

Mawe ya Kukusanywa na Watu Wasio na Ustadi

Mawe kama hayo hupatikana na wastadi na si rahisi yapatikane na watu wasio stadi. Ingawa hivyo, quartz ni nyingi na ni rahisi kupata. Ni mojapo miamba yenye kupatikana kwa wingi zaidi kati ya miamba inayofanyiza madini, nayo hupatikana katika aina tatu ya miamba mikubwa. Unaweza kupata aina fulani ya mawe ya quartz kuwa yenye kupenyezwa na nuru, na nyinginezo kuwa zenye kupenyezwa na nuru kidogo au hata zisizopenyezwa na nuru. Baadhi yazo yana rangi nyekundu, manjano, zambarau, kijani, au hudhurungi. Bila shaka, kwa kuongezea kutafuta quartz, waweza kukusanya jiwe lolote dogo lenye rangi zenye kupendeza au lenye urembo fulani. Na jiwe linapong’arishwa, unaweza kushangaa kwa uzuri walo na unaweza kutamani kulitumia kuwa kito chenye kuvutia, kuwa kitu cha kuonyesha watu kikiwa juu ya kabati, au kama mfano wa sehemu ya mlima wenye mawe-mawe katika shamba lako.

Baada ya kukusanya vipande vya mawe vya kutosha, unapaswa kujua namna ya kuyang’arisha. Baadhi ya vilabu vingine vya wakusanya-mawe hupendekeza kwamba mawe yafingirishwe na changarawe yenye kukwaruza na maji katika pipa tupu linalozunguka na kuendeshwa na mtambo mdogo wa umeme. Hilo litahitaji saburi na wakati, labda majuma, kwanza kwa changarawe yenye kukwaruza, kisha kwa changarawe laini, na hatimaye kwa vumbi ya kung’arisha. Lakini matokeo yanastahili jitihada hiyo.

Mawe ya Aina Nyingine

Kukusanya mawe hakufanywi tu kwa vipande vidogo. Katika Japani mawe makubwa zaidi yanatumiwa sana katika kutengeneza mandhari ya bustani. Kwa kushangaza mawe hayo yanaweza kuwa yenye bei ghali sana. Kwa mfano, kipande kimoja cha jiwe lenye rangi nyekundu-nyekundu lenye uzito wa kilogramu 700 kilikuwa na bei ya zaidi dola 2,300. Kwa nini ni ghali hivyo? Thamani yayo imo katika uzuri wa asili wa umbo lake. Unaweza kupanga kuwe na kijito kinachotiririka kutoka kwa kitu kama kikombe karibu na sehemu ya juu ya jiwe hilo, kikiteremka chini katika maporomoko kadhaa ya maji.

Je! umechochewa sasa kuenda kukusanya mawe? Ikiwa ndivyo, tunatumaini kwamba utapata hazina ya aina tofauti.—Imechangwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki