Ukurasa wa Pili
Majiji Yetu Jitihada Yayo ya Kuendelea Kuwapo 3-12
Kujapokuwa uhalifu na msongamano wa watu, kwa nini mamilioni ya watu huchagua kuishi majijini? Ni baadhi ya matatizo gani yanayokabili wakazi wa majijini leo? Makala hizi zaanzisha mfululizo utakaotokea katika matoleo sita ya Amkeni!
Maisha Maradufu—Ni Nani Apaswa Kujua? 18
Huenda ikawa rahisi kwa vijana fulani kuwadanganya wazazi wao—lakini ni nini gharama ya kuwa na maisha maradufu?
Wanasayansi Wahadaa Umma 24
Katika kufasili vipande vya mifupa, nyakati nyingine tamaa ya jambo fulani ndiyo hutokeza wazo, kama vile wanasayansi katika Uhispania walivyogundua kuhusu yule “Mtu wa Orce.”