Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 4/8 uku. 32
  • Ashangazwa na Uchapishaji wa Amkeni!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ashangazwa na Uchapishaji wa Amkeni!
  • Amkeni!—1994
Amkeni!—1994
g94 4/8 uku. 32

Ashangazwa na Uchapishaji wa Amkeni!

MSOMAJI MMOJA WA AMKENI! KATIKA MINNESOTA, U.S.A., anafanya kazi katika chuo kimoja ambako mwanabiolojia Sam LaBudde angetoa hotuba yenye kichwa “Dolfini Wameenda Wapi?” Msomaji huyu akikumbuka kwamba mhutubu huyo alipata kunukuliwa katika makala ya Amkeni! ya “Je! Uvuvi wa Neti Inayovutwa na Meli Unamalizwa?” (Mei 22, 1992, Kiingereza), alipeleka gazeti hilo kwenye mhadhara huo.

“Nilimwandikia Bw. LaBudde taarifa fupi kwenye gazeti hilo. Nilitaja kwamba angefurahi kusikia kwamba makala hiyo nzuri ingesomwa ulimwenguni pote katika lugha nyingi na kwamba gazeti hilo lilikuwa likichapishwa kwa nakala zaidi ya 13,000,000. Kisha nikaandika jina langu na kuliacha Amkeni! hilo kama limefunguliwa jukwaani nami nikarudi kwenye kiti changu.

“Muda mfupi baadaye niliona mtu akienda jukwaani, akachukua gazeti hilo, na kuanza kulisoma. Baada ya dakika chache, aliinua kichwa na kuuliza kwa sauti ikiwa mtu yule aliyeacha gazeti hilo alikuwapo. Nilipoinua mkono wangu na kusema, ‘Nipo,’ akaja kuketi karibu nami. Alinishukuru kwa ajili ya gazeti hilo naye akasema kwamba yeye huthamini sana mtu anapompa habari zinazokazia kazi wanazofanya na mambo wanayotimiza. Hata hivyo, alihisi kwamba huenda nilikosea kwa kusema kwamba uchapishaji wa gazeti hilo ni 13,000,000. Alifikiri kwamba ni lazima nilimaanisha 13,000. Nilifungua ukurasa wa kwanza wa gazeti hilo na kumwonyesha kwamba ulikuwa 13,000,000. Alishangaa sana. Alivutiwa pia na hesabu ya lugha ambazo magazeti hayo yalichapishwa [sasa lugha 74]. Yeye alifikiri kwamba gazeti hilo lilikuwa likigawanywa katika United States pekee, lakini nikaeleza kwamba linagawanywa ulimwenguni pote.”

Kama ungependa kupokea nakala ya Amkeni! nyumbani mwako, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki