Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 5/8 uku. 32
  • Msamaria Mwema wa Ki-Siku-Hizi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msamaria Mwema wa Ki-Siku-Hizi
  • Amkeni!—1994
Amkeni!—1994
g94 5/8 uku. 32

Msamaria Mwema wa Ki-Siku-Hizi

MWANAMKE mmoja katika Kanada alipatwa na aksidenti ya gari. Msamaria Mwema wa ki-siku-hizi alikuja kumsaidia. (Luka 10:29-37) Kwa kuvutwa na fadhili ya mwanamume huyo, mwanamke huyo aliandikia The Georgetown Independent yafuatayo:

‘Kwa Mhariri:

‘Ninaandika kwa sababu mbili. Kwanza, nataka kumshukuru mkaaji mmoja wa Georgetown aliyenisaidia mwisho-juma huu uliopita baada ya mimi kushindwa kudhibiti gari langu na kutumbukia ndani ya shimo.

‘Bw. John Saunders alikuwa akiendesha gari kupitia hapo na alisimama. Alianza kunipa msaada wa kwanza na alinipa uhakikishio mwingi wa kunituliza. Alikaa pamoja nami mpaka madereva wa gari la wagonjwa na madaktari wakaja kusaidia. Jumuiya yenu imebarikiwa kuwa na Msamaria Mwema kama Bw. Saunders anayeishi katika jumuiya yenu.

‘Bw. Saunders alikuja kuzuru mume wangu na mimi hospitalini, kuhakikisha tu nilikuwa katika hali nzuri. Nilishangaa sana kujua kwamba Bw. Saunders hufanya kazi kwenye ofisi kuu ya Mashahidi wa Yehova katika Georgetown. Sikuzote nilifikiri kwamba watu hao hawapendi mambo ya matibabu, na kumbe mmoja wao alikuwa ametumia mazoezi ya tiba ya kutoa msaada wa kwanza kunisaidia. Hiyo yanileta kwenye sababu ya pili ya kuandika.

‘Ningependa kuwaomba radhi Mashahidi wa Yehova wote kwa ukosefu wa adabu ambao nimewaonyesha wakati wamenitembelea mlangoni pangu. Sikuzote nimeamini kwamba nyinyi ni washupavu wenye kushikilia maoni yenu tu. Bw. Saunders alithibitisha kwamba dhana hiyo ya kupita kiasi ni yenye makosa. Nyinyi nyote ni watu wa kawaida tu mnaojaribu kufanya lile mhisilo kuwa lafaa.

‘Asante tena, Bw. Saunders, na uendelee na imani. Mungu akubariki.

‘T. M., Toronto’

Mashahidi wa Yehova huamini kwamba ‘ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe.’ (Luka 10:27, ZSB) Ikiwa wewe watamani kujifunza mengi zaidi juu ya Mashahidi wa Yehova au ungetaka kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo iliyoorodheshwa katika ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki