Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 10/22 uku. 32
  • Amkeni! Hutoa Masuluhisho Halisi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Amkeni! Hutoa Masuluhisho Halisi
  • Amkeni!—1994
Amkeni!—1994
g94 10/22 uku. 32

Amkeni! Hutoa Masuluhisho Halisi

Hilo ndilo jambo ambalo msomaji mmoja katika Vinton, Iowa, Marekani, apendalo juu ya Amkeni! Akifungua kwa salamu “Mhariri Mpenzi,” mwanamke huyo alisema:

“Ninaandika kuonyesha shukrani zangu kwa zile makala za wakati ufaao katika gazeti Amkeni! Mimi huvutiwa na kila toleo nipokealo nami hukumbushwa daima juu ya ubora wa hali ya juu zaidi wa makala zilizo katika gazeti hili.

“Magazeti mengi huvunja moyo sana yasomwapo au yapitiwapo, kwa sababu tu leo ulimwenguni habari mbaya ni nyingi sana. Kwa upande mwingine, ingawa sikuzote Amkeni! hushughulikia habari zilizo na hangaikio na umaana wa karibuni kwetu sote, mfikio utumiwao hauna kifani. Sikuzote wasomaji waweza kuwa na hakika ya kupata kwamba Amkeni! hutoa tumaini la suluhisho halisi na lenye kudumu kwa matatizo ya ulimwenguni pote kwa kutia moyo kuzitumaini ahadi za Biblia na kuelekeza uangalifu kwenye Biblia kuwa mamlaka, wala si katika maoni ya wanadamu yanayotofautiana au ya kibinafsi.

“Muda wa miaka mingi iliyopita nimefurahia kikweli kusoma Amkeni! Usomaji utufaao sana sisi sote ni ule utoao mfikio wa kufuata haki ili kuboresha maisha huku ukidumisha maoni chanya juu ya wakati ujao. Asanteni kwa kusaidia wasomaji wenu waone lililo la maana.”

Ikiwa ungependa upelekewe nakala ya Amkeni! nyumbani kwako, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki