Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 12/22 uku. 32
  • ‘Kilichookoa Uhai wa Mwanangu’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Kilichookoa Uhai wa Mwanangu’
  • Amkeni!—1994
Amkeni!—1994
g94 12/22 uku. 32

‘Kilichookoa Uhai wa Mwanangu’

Mama mmoja katika California, Marekani, alieleza kwamba kilichofanya hivyo ni kile alichokuwa amesoma katika Mnara wa Mlinzi na gazeti jenzi lalo, Amkeni! Aliandika hivi:

“Mwanangu mchanga (wa miaka minne) na mimi tulitekwa kwa kushikiwa bunduki tukalazimishwa kuendesha gari hadi benki yangu. Mshambulizi alininyang’anya, lakini niliweza kumshika mwanangu kwa haraka na kutoroka. Kile nihisicho kwa kweli kuwa kiliokoa uhai wa mwanangu, na pia wangu mwenyewe, ni yale madokezo yenye kutumika ya Biblia yachapwayo katika magazeti haya yenye thamani kubwa.”

Mama huyo aliongezea elezo zaidi: “Mapema kidogo nilikuwa nimesoma katika mojapo magazeti ya Amkeni! jinsi ya kubaki mtulivu ukabiliwapo na hali ya hatari kama hii. Nilisali mara hiyo kwa Yehova Mungu ili anisaidie kutulia. Niliweza pia kutuliza mshambulizi huyo kwa kumnukulia maandiko ya Biblia.”

Kusudi la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! ni kuonyesha kwamba nyakati zetu zenye msukosuko zilitabiriwa katika Biblia. Pia magazeti hayo huandalia watu msaada ili wakabiliane na hali za leo zenye mikazo. Lakini magazeti hayo hufanya mengi zaidi. Hukazia suluhisho la pekee lililo la daima—serikali ya Ufalme wa Mungu ambayo Yesu Kristo alifundisha wafuasi wake kusali ije. (Mathayo 6:9, 10) Hakika wewe waweza kunufaika kutokana na kusoma Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwa ukawaida.

Ikiwa ungependa kupelekewa Mnara wa Mlinzi na Amkeni!, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki