Hayo Humwarifu Daima
Msomaji fulani katika Ohio, Marekani, aliandika hivi: “Nataka kuwajulisha tu jinsi nithaminivyo sana magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Kwa kweli hayo ni vito.” Mwanamke huyo alieleza jinsi kuyasoma humwarifu daima.
“Mimi niliacha shule ya sekondari miaka 13 iliyopita,” akaandika. “Majuzi, nilitakiwa na serikali nifanye mtihani ulinganao na wa shule ya sekondari, ambao wajulikana vizuri zaidi kuwa mtihani wa GED (Usitawi wa Elimu ya Jumla). Ili kujitayarisha kwa ajili ya mtihani huu, nililazimika kuhudhuria madarasa. Kwa kawaida, mtu akifanya vema katika madarasa haya, kwa muda mchache kama miezi sita, aweza kuufanya mtihani wa GED. Ingawa hivyo, nilikuwa tayari kuufanya mnamo majuma manne, na nilipokea alama ya juu sana.
“Sababu ni nini? Karibu kila jambo katika mtihani huo—sayansi, masomo ya kijamii, na kadhalika—lilikuwa limekwisha kushughulikiwa kwa njia moja au nyingine katika matoleo yaliyopita ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Kwa kusoma tu magazeti hayo, stadi zangu katika kusoma, kuendeleza maneno, na kuweka vituo vya sentensi zilidumishwa. Kwa kweli, mimi hata sikujifunza lolote la masomo haya. Madarasa niliyohudhuria yalinisaidia kuunoa uwezo wangu wa hesabu tu.”
Ikiwa wewe ungependa kupata nakala ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! au ungependa kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.