“Maoni Yangu ya Wajibu wa Daktari Yamebadilika”
AKANE, msichana wa miaka minne katika Osaka, Japani, alikuwa na kasoro za moyo zilizotatanika—dosari ya veli ya vipinde vitatu vya moyo na ya kuta za vyumba vya damu moyoni—zilizomlazimisha kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo. Wazazi wake waliwasihi madaktari waufanye upasuaji huo bila damu.a
Upasuaji wa kufungua moyo wazi bila damu ni mgumu kufanyiwa watoto kwa sababu ya kiasi chao kidogo cha damu. Katika kisa cha Akane, madaktari walikubaliana kupasua bila damu. Ikionyesha stadi zao bora zaidi za kitiba, upasuaji wa Akane ulifaulu. Alipona upesi na sasa afurahia afya nyingi.
Mama ya Akane aliwaandikia madaktari walioshiriki katika upasuaji huo, akitia ndani picha ya Akane ya majuzi. Tabibu fulani wa nusu-kaputi alijibu kwa kuandikia mama ya Akane. Kwa sehemu, barua hiyo ilisomeka hivi:
“Pono la kustaajabisha la Akane latusisimua. Nilikuwa na wakati mgumu kuzuia machozi yasinitoke nilipoona ile picha ya kupendeza uliyotia ndani ya barua yako. Kilichonifadhaisha sana hakikuwa ugumu wa upasuaji huo bali ni tofauti iliyopo kati ya imani zenu na zangu. Sasa, kutokana na ono hili, maoni yangu ya wajibu wa daktari yamebadilika. Madaktari wapaswa kutumia uelewevu wao thabiti wa ujuzi wa kitiba kuokoa uhai, lakini yawapasa pia wastahi hali ya kujiheshimu na mapendezi ya mgonjwa.”
[Maelezo ya Chini]
a Kwa kupatana na Matendo 15:29, Mashahidi wa Yehova hujiepusha na damu, kutia na mitio-damu mishipani. Hata hivyo, wao hukubali utumizi wa tiba isiyo na damu.