Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • bq kur. 3-61
  • Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
  • Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ule Msingi wa Kidini
  • Vipi Wakristo?
  • Wakristo wa Mapema na Damu
  • Damu Ikiwa Dawa
  • Je! Kukataa Ni Namna ya Ujiuaji?
  • Jukumu la Daktari
  • Ushirikiano Kati ya Mgonjwa na Daktari
  • Kuondolea Madaktari Dhima
  • Kustahi Daraka la Kiuzazi
  • Kutibu Yule “Mwanadamu Mzima-mzima”
  • Je! Msimamo Wao Si wa Kiakili Kitiba?
  • Damu—kitu Tata Kisicho na Kifani
  • Kutia Damu Mishipani—hatari Halisi Ni ya Kadiri Gani?
  • Ni Nini Zile Hatari?
  • Namna za Miitikiano ya Kutiwa Damu Mishipani
  • Njia Nyinginezo za Kutibu
  • Upasuaji Mkubwa Bila Damu
  • Wewe Utafanya Nini?
  • MAREJEZO
  • Maswali ya Funzo la Kijitabu Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
    Huduma Yetu ya Ufalme—1988
  • Kuokoa Uhai kwa Damu—Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Damu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Azimio Letu Imara Juu ya Uhai na Damu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
bq kur. 3-61

Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu

1. Ni uhakika gani juu ya damu unaoendelea kueleweka vizuri zaidi?

1 DAMU ni muhimu kabisa kwa uhai. Ingawa jambo hili limetambuliwa kutoka nyakati za kale, utafiti wa ki-siku-hizi unaandaa uelewevu mkubwa zaidi juu ya kazi zayo za kuendeleza uhai.

2. Ni njia gani ya utibabu inayokubaliwa, lakini ni nani wasiokubali?

2 Zoea la kutia mishipani damu ya kibinadamu lina mahali pakuu katika matibabu ya ki-siku-hizi. Wale walio katika uwanja wa kitiba na wengine wengi wanaona uhamishaji wa damu kutoka kwa mwanadamu mmoja kuipeleka kwa mwingine kuwa njia ya matibabu inayokubaliwa.1a Lakini kuna watu wasiokubali kutiwa damu mishipani. Hao ni Mashahidi wa Yehova.

3, 4. Ni maoni gani ya Biblia ambayo Mashahidi wa Yehova hushikilia juu ya uhai, na ni maswali gani yanayozushwa na hili?

3 Mashahidi wa Yehova wanathamini sana uhai na kuustahi kwa kina kirefu. Hii ni moja ya sababu wao hawavuti tumbako, hawatumii dawa za kulevya wala hawatafuti kutoa mimba. Wao wamejifunza kutokana na Biblia kuona uhai kuwa mtakatifu, kitu cha kupewa himaya na kuhifadhiwa kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya watoto wao.

4 Kwa nini, basi, Mashahidi wa Yehova wanakataa kutiwa damu mishipani? Je! kuna msingi fulani wa kiakili wa kuwa na usadikisho huu ambao wao wanashikilia hata wanapokabili kifo? Na je! msimamo wao juu ya jambo hili ni usiopatana kabisa na maarifa na kanuni za tiba ya ki-siku-hizi?

5. Kusudi la kichapo hiki ni nini, na jambo hili litashughulikiwa jinsi gani?

5 Mada hii yapasa ipendeze kila mtu aliye katika kazi ya tiba, kwa maana huenda wakati wo wote daktari akakabiliwa na suala la damu. Hiyo inawezekana sana, kwa kuwa kuna zaidi ya milioni tatu za Mashahidi wa Yehova duniani pote. Labda baadhi yao wanaishi katika jumuiya yako. Yanayofuata yameandikwa ili yasaidie madaktari kuelewa Mashahidi wa Yehova wakiwa wagonjwa na kufikiria jinsi maoni yao yanaweza kukubaliwa kwa kadiri inayofaa. Kwanza sisi tutachunguza msingi wa kidini wa msimamo wao. Ndipo, kuanzia ukurasa wa 17, tutafikiria maadili yanayohusika, na mavumbuzi na maono fulani ya hivi majuzi ya madaktari wanaostahili ambayo huenda yakawa na mafaa katika kutatua matatizo yanayohusu utumizi wa damu.

6. Habari hii ni yenye kupendeza kwa nani?

6 Hata watu ambao hawamo katika uwanja wa kitiba wanaalikwa wachungulie ndani ya jambo hili la maana. Kwa kweli msimamo unaochukuliwa na Mashahidi wa Yehova unahusisha ndani haki na kanuni zinazoweza kuathiri kila mmoja wetu. Na maarifa ya kujua ni mambo gani ambayo wao wanaitikadi, na kwa nini wanayaitikadi, yatasaidia mtu aelewe vizuri zaidi suala hili ambalo limehangaisha madaktari, wastadi wa sheria, na wanafunzi wa Biblia. Basi, ni mambo gani makuu yaliyo katika suala hili?

Ule Msingi wa Kidini

7. Ni baadhi ya maoni gani mengine kuhusu damu, na ni juu ya msingi gani Mashahidi wa Yehova wanachukua msimamo kuhusu damu?

7 Madaktari walio wengi wanaona utumizi wa damu kuwa jambo la hukumu ya kitiba hasa, jambo la maamuzi yao ya kila siku juu ya kutumia dawa fulani au taratibu fulani za upasuaji. Huenda watu wengine wakaona msimamo wa Mashahidi wa Yehova kuwa suala la kiadili au kisheria hasa. Huenda wao wakafikiri kulingana na haki ya uhai, mamlaka ya kufanya maamuzi juu ya mwili wa mtu mwenyewe, au wajibu mwingi wa serikali kutoa himaya juu ya uhai wa raia zayo. Pande zote hizi zinahusiana na jambo lenyewe. Hata hivyo msimamo unaochukuliwa na Mashahidi wa Yehova ni wa kidini hasa; ni msimamo unaotegemea msingi wa mambo ambayo Biblia inasema.

8. Kwa sababu ya msimamo unaochukuliwa na Mashahidi wa Yehova, ni swali gani linalotokea kimantiki?

8 Huenda watu wengi wakautilia shaka uhalali wa taarifa hiyo juu. Wao wana habari kwamba makanisa mengi sana yanaunga mkono utumizi wa damu, yakiimarisha programu za benki ya damu na kutia watu moyo wachange damu. Kulingana na hilo, swali linatokea kimantiki:

Biblia inasema nini juu ya wanadamu kuingiza damu katika miili yao?

9, 10. Ni nini linaloonyesha kwamba Biblia ina mengi ya kusema juu ya damu, na Mungu alitoa amri gani kuhusu damu mapema mwa historia ya aina ya binadamu?

9 Hata watu mmoja mmoja ambao hawaioni Biblia kuwa neno la Mungu lililovuviwa lazima wakiri kwamba ina mengi ya kusema juu ya damu. Kutoka kitabu cha kwanza cha Biblia mpaka kile cha mwisho, “damu” inatajwa zaidi ya mara mia nne. Mistari fulani ya Biblia inahusiana kimahususi na lile suala la kuendeleza uhai kwa kutumia damu. Acheni tuichunguze kifupi:

10 Maandishi ya Biblia huonyesha kwamba, mapema katika historia ya aina ya binadamu Muumba na Mpaji-Uhai alijieleza mwenyewe juu ya suala la damu. Mara tu baada ya gharika ya tufe lote, Mungu alipowapa wanadamu kwa mara ya kwanza haki ya kula mnofu wa mnyama, yeye aliamuru Noa na jamaa yake hivi: “Kila mnyama anayejongea ambaye yu hai anaruhusiwa kutumika kuwa chakula kwa ajili ya ninyi. Kama vile katika kisa cha mboga-mboga za kijani, mimi nawapa ninyi zote. Ila tu mnofu pamoja na nafsi yao—damu yao—ni lazima ninyi msile.”—Mwanzo 9:3, 4, NW.

11. Ni nini linaloonyesha kwamba katika kuua wanyama mengi zaidi ya ulaji yanahusika?

11 Kwanza kabisa, Muumba alikuwa akiandaa kirekebi cha ulaji wakati ambapo aina ya binadamu ilikuwa ikifanya mwanzo mpya. (Linganisha Mwanzo 1:29.) Hata hivyo, Mungu alionyesha kwamba mengi zaidi ya ulaji yalihusika katika kuua wanyama kwa ajili ya chakula. Hiyo ilikuwa kwa sababu damu ya kiumbe iliwakilisha uhai wake au nafsi yake. Hivyo, tafsiri fulani za Biblia zinafasiri Mwanzo 9:4 hivi: “Ila tu ninyi hamtakula mnofu pamoja na uhai wao, yaani, damu yao.”—Revised Standard Version; Moffatt.

12, 13. Muumba aliambatanisha nini kwenye utumizi wa damu, na sisi tunajuaje kwamba si damu ya wanyama tu inayohusika?

12 Kwa hiyo kirekebi hiki cha kimungu hakikuwa kizuizi tu juu ya ulaji, kama vile daktari kushauri mgonjwa aepuke chumvi au shahamu (mafuta). Muumba aliambatanisha na damu kanuni ya kiadili iliyo ya maana sana. Katika kumimina nje damu yote ambayo kwa kiasi kinachofaa ingeweza kuminywa itoke, Noa na wazao wake wangedhihirisha staha yao kwa uhakika wa kwamba uhai ulitoka kwa na ulitegemea Muumba. Lakini acheni tuchunguze zaidi jambo hili.

13 Andiko lililonukuliwa juu linatumika kwa damu ya mnyama. Je! kanuni iyo hiyo ingetumika kwa damu ya kibinadamu? Ndiyo, tena kwa kani iliyo imara hata zaidi. Kwa maana Mungu aliendelea kusema kwa Noa hivi: “Mbali na hilo, damu yenu ya nafsi zenu mimi nitaomba kurudi. . . . Mtu ye yote anayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake mwenyewe itamwagwa na mwanadamu, kwa maana katika mfano wa Mungu yeye alifanya mwanadamu.” (Mwanzo 9:5, 6, NW) Sasa, ikiwa damu ya mnyama (inayowakilisha uhai wa mnyama) ilikuwa ya umaana mtakatifu kwa Mungu, kwa uwazi damu ya kibinadamu ilikuwa na umaana mtakatifu wa kima kikubwa hata zaidi. Watu wanaofuata maelekezo haya ya kimungu hawangekuwa wakimwaga damu ya wanadamu (kuwaua), wala hawangekuwa wakila ama damu ya mnyama ama ya kibinadamu.

Hata hivyo, je! amri hii kwa Noa ilikuwa kizuizi chenye hadi au cha muda tu? Je! inahusu vizazi vya baadaye, kutia na chetu?

14, 15. Ilikuwa aina gani ya amri aliyopewa Noa kuhusu damu, na ni maelezo gani ya rabi mmoja yanayohusu hapa?

14 Wanachuo wengi wa Biblia wanatambua kwamba hapa Mungu alionyesha wazi kirekebi kilichotumika, si kwa Noa na jamaa yake ya wakati huo tu, bali pia kwa aina ya binadamu wote kutoka wakati huo na kuendelea—kwa kweli wote walio hai tangu ile Gharika ni wa kutokana na jamaa ya Noa. (Mwanzo 10:32) Mathalani, Mwanatheolojia na Mwanamageuzo-ya-Kidini John Calvin alikiri juu ya lile katazo kuhusu damu kwamba “sheria hii ilikuwa imepewa kwa ulimwengu kwa ujumla mara tu baada ya gharika.”2 Na Gerhard von Rad, profesa kwenye Chuo Kikuu cha Heidelberg, anarejezea Mwanzo 9:3, 4, kuwa ni “amrisho kwa aina ya binadamu wote,” kwa sababu aina ya binadamu yote imetokana na Noa.3

15 Kwa kuwa sheria kuhusu damu iliunganishwa na tamko la Mungu lililokazia staha ya juu kwa ajili ya uhai wa kibinadamu, sisi tunaweza kuthamini maono ya Rabi Benno Jacob:

“Hivyo makatazo mawili yanaambatana pamoja. Hayo ndiyo madai yaliyo ya msingi zaidi kwa jamii ya kibinadamu katika maana halisi ya neno hilo. . . . Ile ruhusa ya kula nyama, lakini bila damu yayo, na lile katazo dhidi ya kumwaga damu ya kibinadamu ni mambo yanayoonyesha mahali pa mwanadamu ndani ya ulimwengu wa walio hai . . . Kwa muhtasari: sababu ya katazo la damu ni ya namna ya kiadili. . . . Dini ya Kiyahudi ya baadaye iliona kifungu hiki kuwa chenye kuimarisha maadili ya kimsingi kwa kila mwanadamu aliyeko.” (Italiki zimeongezwa.)4

Kwa uhakika, kutokana na ile sehemu ya mapema ya Mwanzo, Wayahudi wa baadaye walichota “sheria za msingi” saba kwa ajili ya aina ya binadamu, na amri hii iliyopewa kwa Noa na wana wake kuhusu damu ilikuwa moja yazo.5 Ndiyo, ujapokuwa uhakika wa kwamba mataifa mengi hayakuifuata, kwa kweli hii ilikuwa sheria kwa ajili ya aina ya binadamu wote.—Matendo 14:16; 17:30, 31.

16, 17. Ni sheria gani kwa Waisraeli iliyoonyesha kwamba marufuku ya Mungu juu ya damu yalikuwa yangali yakitumika, na ilikuwa njia gani pekee Waisraeli wangeweza kutumia damu?

16 Baadaye katika sheria yake iliyopewa kwa taifa la Israeli, Yehova Mungu alikataza uuaji, hiyo ikishuhudiza wazi kwamba agizo la kimamlaka alilokuwa amempa Noa lilikuwa bado likifanya kazi. (Kutoka 20:13) Kwa mujibu wa jambo hilo, Mungu aliharimisha pia kula damu, akisema:

“Kwa habari ya mtu ye yote wa nyumba ya Israeli au mkaaji fulani wa kigeni anayekaa akiwa mgeni katikati yao ambaye hula damu ya namna yo yote, mimi kwa uhakika nitaweka uso wangu dhidi ya nafsi ambayo inakula damu, na mimi kweli kweli nitamkatilia mbali kutoka miongoni mwa watu wake.”—Walawi 17:10, NW.

17 Waisraeli waliruhusiwa kutumia damu ya wanyama kwa njia moja tu. Hiyo ilikuwa katika kuitoa kama dhabihu kwa Mungu, wakimkiri kuwa ndiye Mpaji-Uhai ambaye walikuwa na deni kwake. Yeye aliwaambia hivi: “Nafsi ya mnofu imo katika damu, na mimi mwenyewe nimeiweka juu ya madhabahu ili ninyi mfanye upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu, kwa sababu ni damu ambayo hufanya upatanisho kwa njia ya nafsi [au uhai] iliyo ndani yayo.”—Walawi 17:11, NW.

18, 19. (a)Ni hadhari gani ambayo wawindaji Waisraeli walitakwa kuchukua walipoua wanyama kwa ajili ya chakula, na kwa nini? (b) Kwa kutii amri hii, walionyesha utambuzi wa uhakika gani?

18 Namna gani damu ya wanyama waliouawa kwa ajili ya chakula, si kwa ajili ya dhabihu? Mungu aliambia waabudu wake kwamba mwindaji aliyeshika hayawani-mwitu au nyuni “lazima katika kisa hicho amimine nje damu yake na kuifunika kwa mavumbi. Kwa maana nafsi ya kila namna ya mnofu imo katika damu yao kwa njia ya nafsi iliyo ndani yayo. Basi mimi nilisema kwa wana wa Israeli: ‘Ni lazima ninyi msile damu ya mnofu wa aina yo yote, kwa sababu nafsi ya kila namna ya mnofu ni damu yao. Mtu ye yote ambaye anaila atakatiliwa mbali.’”—Walawi 17:13, 14; Kumbukumbu 12:23-25, NW.

19 Huku kumimina damu nje hakukuwa desturi ya kidini tu; kwa kweli ulikuwa ni upanuzi wa sheria ya kimungu iliyopewa kwa Noa. Wakati wa kuua mnyama, mtu anapaswa kutambua kwamba uhai wake unatoka kwa na ni mali ya Mungu. Kwa kutokula damu, lakini ‘kuimimina nje’ juu ya madhabahu au juu ya nchi, kwa njia hiyo Mwisraeli alikuwa akirudisha uhai wa kiumbe kwa Mungu.

20. (a) Ni adhabu gani zilizoonyesha kwamba kuvunja sheria ya Mungu juu ya damu kulikuwa kosa zito? (b) Ni maandiko gani yanayoonyesha kwamba kula mnofu pamoja na damu ndani yao kulitokeza hatia?

20 Lilionwa kuwa kosa zito sana Mwisraeli kupuuza uhai kama ulivyowakilishwa na damu. Mtu mwenye kupuuza kwa makusudi sheria hii kuhusu damu alipaswa ‘kukatiliwa mbali,’ kuuawa. (Walawi 7:26, 27; Hesabu 15:30, 31, NW) Kipimo fulani cha hatia hata kilitokana na kula mnofu wenye damu wa mnyama aliyejifia mwenyewe au aliyeuawa na hayawani-mwitu.—Walawi 17:15, 16; linganisha Walawi 5:3; 11:39.

Je! sheria ya Mungu juu ya damu ingeweza kuwekwa kando katika nyakati za dharura?

21. Ni kielelezo kipi cha Kimaandiko kinachoonyesha kwamba sheria ya Mungu juu ya damu haingeweza kuwekwa kando wakati wa dharura?

21 Biblia inajibu, Hapana. Hakukuwa na mlegezo wa pekee wa sheria hiyo kwa ajili ya nyakati za mvutano. Tunaweza kuona jambo hili kutokana na lililotukia kwa askari fulani wa Israeli katika siku za Mfalme Sauli. Kwa sababu ya kuumwa na njaa baada ya pigano la muda mrefu, wao walichinja kondoo na ng’ombe na ‘wakaangukia kula pamoja na damu.’ Wao walikuwa na njaa na hawakuwa wakila damu kwa makusudi, lakini katika haraka-haraka yao ya kula nyama hawakuhakikisha kwamba wanyama hao walikuwa wameondolewa damu ifaavyo. Je! uhakika wa kwamba hii ilionekana kuwa “dharura” uliudhuru mwendo wao? Tofauti na hivyo, mfalme wao aliyewekwa rasmi na Mungu alitambua kitendo chao kuwa ni ‘kutenda dhambi dhidi ya Yehova kwa kula pamoja na damu.’—1 Samweli 14:31-35, NW.

Je! huku kutopenda damu vya kufaa kunatumika kwa damu ya kibinadamu pia?

22. Kwa nini ni jambo lenye akili kukata maneno kwamba sheria ya Mungu kuhusu damu ya mnyama inatumika pia kwa damu ya kibinadamu?

22 Ndiyo. Na hilo ni jambo linaloeleweka kabisa kwa sheria ya Mungu kukataza kula “namna yo yote ya damu,” “damu ya mnofu wa namna yo yote.” (Walawi 17:10, 14, NW) Tunaweza kuona jinsi taifa la Kiyahudi lilivyoona sheria hii kwa kufikiria kituko kimoja chenye kuhusisha ndani baadhi ya Wayahudi waliokuwa wamemfuata na kumsikiliza Yesu. Katika pindi moja yeye alinena kitamathali juu ya ‘kunywa damu yake,’ kwa maana yeye alijua kwamba baada ya muda fulani lazima damu yake imiminwe nje katika kifo cha kidhabihu na kwamba ingetokeza uhai kwa wale ambao, kwa njia ya imani, wangekubali dhabihu yake. (Yohana 6:53-58, NW) Kwa wazi bila kung’amua kwamba Yesu alikuwa akinena kwa ufananisho, baadhi ya wanafunzi wake Wayahudi walishtuka kuhusu maneno yake na wakaacha kabisa kumfuata. (Yohana 6:60-66) Ndiyo, ile fikira ya kutwaa damu ya kibinadamu ilikuwa ya kukirihisha kabisa Wayahudi hao waabudu Mungu.

Vipi Wakristo?

23. Ni matokeo gani ambayo kifo cha kidhabihi cha Mesiya kilikuwa nayo kwenye vizuizi vya ulaji vya ile sheria ya Musa?

23 Sheria ya Musa ilielekeza kwenye kuja kwa Mesiya na kifo chake cha kidhabihu. Kwa sababu hiyo, baada ya Yesu kufa, waabudu wa kweli hawakuwajibishwa tena kushika sheria ya Musa. (Warumi 10:4; 6:14; Wakolosai 2:13, 14) Vizuizi vya ulaji vya ile Sheria, kama vile vilivyokuwa dhidi ya kula shahamu au mnofu wa wanyama fulani, havikuwa vyenye kutumika tena.—Walawi 7:25; 11:2-8.

Basi, je! katazo la kimungu dhidi ya damu linatumika kwa Wakristo?

24. Wakati wa kushughulikia suala la tohara kwa ajili ya Wakristo wasio Wayahudi, ni nini lililoamuliwa kuhusu damu?

24 Jambo hili lilitokea kwa ajili ya mazungumzo katika 49 W.K., wakati wa kongamano moja la mitume na wanaume wazee wa Yerusalemu waliotumikia wakiwa baraza kuu la wazee kwa ajili ya Wakristo wote. Kongamano hilo lilifanywa kwa kujibu suala moja kuhusu tohara. Baraza hili la kimitume liliamua kwamba haikuwa lazima watahiriwe watu wasio Wayahudi waliokubali Ukristo. Wakati wa mazungumzo hayo Yakobo ndugu-nusu wa Yesu alileta kwenye uangalifu wa baraza hilo mambo fulani yenye kuhitajiwa sana aliyoona kuwa ya maana kutiwa ndani ya uamuzi wao, yaani, “washike mwiko wa vitu vinavyochafuliwa na sanamu na wa uasherati na wa vinavyonyongwa na wa damu.” (Matendo 15:19-21, NW) Yeye alirejeza nyuma kwenye maandishi ya Musa, ambayo yanafunua kwamba hata kabla ya Sheria kutolewa, Mungu alikuwa ameonyesha kutokubali mahusiano ya ngono zisizo za kiadili, ibada ya sanamu na kula damu, ambako kungetia ndani kula mnofu wa wanyama walionyongwa wakiwa na damu.—Mwanzo 9:3, 4; 19:1-25; 34:31; 35:2-4.

25. Uamuzi huu wa baraza la kimitume ulikuja kuwa sehemu ya nini?

25 Uamuzi wa baraza hilo ulipelekwa kwa njia ya barua kwenye makundi ya Kikristo. Sasa huo umetiwa ndani ya Biblia ukiwa sehemu ya Maandiko yaliyovuviwa ambayo yana manufaa “kwa kufundisha, . . . kwa kunyoosha mambo.” (2 Timotheo 3:16, 17, NW) Uamuzi huo ulikuwa:

26, 27. Uamuzi huo ulitaarifu nini waziwazi, na tunajuaje kwamba haukuwa kauli tu ya mitume?

26 “Roho takatifu na sisi wenyewe tumependelea kutoongeza mzigo zaidi kwenu ninyi, isipokuwa mambo haya ya lazima, kuendelea kushika mwiko wa vitu vinavyodhabihiwa kwa sanamu na wa damu na wa vitu vinavyonyongwa na wa uasherati. Ikiwa kwa uangalifu ninyi mnajiepusha wenyewe na vitu hivyo, ninyi mtafanikiwa.”—Matendo 15:28, 29, NW.

27 Ndiyo, hata ingawa Wakristo hawakuwa chini ya sheria ya Musa, ilikuwa “lazima” washike mwiko wa damu. Je! hiyo ilikuwa kauli tu ya kibinafsi ya mitume? Sivyo hata kidogo. Kama vile wao walivyotaarifu, uamuzi huo ulifanywa kulingana na roho takatifu ya Mungu.

28. Kulingana na Profesa Walther Zimmerli, amri hiyo ilifanyiza tofauti gani?

28 Kuhusu amri hiyo ya Kikristo, Profesa Walther Zimmerli, wa Chuo Kikuu cha Göttingen, Ujeremani, alieleza hivi:

Kundi la kwanza la Wakristo-Wayudea katika ule uamuzi ulioripotiwa katika Matendo 15 lilifanya tofauti kati ya Sheria iliyopewa kwa Israeli kupitia Musa na amri iliyopewa [kupitia] Noa kwa ulimwengu wote.”—Zürcher Bibelkommentare.6

29. Ni nini linaloonyesha kwamba amri ya kushika mwiko wa damu haikuwa kizuizi cha ulaji tu bali ilikuwa takwa la kimaadili?

29 Amri ya ‘kushika mwiko wa damu’ haikuwa kizuizi cha ulaji tu bali ilikuwa takwa zito la kiadili, kama inavyoonwa kwa uhakika wa kwamba ilikuwa jambo zito kwa Wakristo kama vile ‘kushika mwiko wa ibada ya sanamu au uasherati.’

Wakristo wa Mapema na Damu

30, 31. Ni nini linaloonyesha aina yenye kudumu ya katazo la damu na kwamba halikuwa takwa la muda tu?

30 Lile baraza la Yerusalemu lilipelekea makundi ya Kikristo uamuzi huu wenye kukata maneno wazi, na matokeo yakawa ya mwelekeo chanya. Tunasoma hivi katika Matendo sura 16 kwa habari ya Paulo na washirika wake: “Wao walipokuwa wakiendelea kusafiri kupitia majiji wangewasilisha kwa wale wa kule maamuzi rasmi yaliyokuwa yameamuliwa na mitume na wanaume wazee waliokuwa katika Yerusalemu kwa ajili ya kushikwa. Kwa hiyo, kweli kweli, makundi yaliendelea kufanywa thabiti katika imani na kuongezeka katika hesabu siku kwa siku.”—Matendo 16:4, 5, NW.

Je! ule uamuzi uliorekodiwa katika Matendo 15:28, 29 ulikuwa takwa la muda tu, si wajibu ulioendelea kukaa juu ya Wakristo?

31 Watu fulani wameshikilia kwamba uamuzi rasmi wa kimitume haukuwa wajibu wa kudumu kwa Wakristo. Lakini kwa uwazi kitabu cha Matendo kinaonyesha vingine. Kinaonyesha kwamba, yapata miaka kumi baada ya lile baraza la Yerusalemu kutokeza huo uamuzi rasmi, Wakristo waliendelea kutii “uamuzi wa kwamba wao wamepaswa kujiepusha wenyewe na kinachodhabihiwa kwa sanamu na pia na damu na kile kinachonyongwa na uasherati.” (Matendo 21:25, NW) Hii inaonyesha kwamba wao walikuwa na habari kwamba lile takwa la kushika mwiko wa damu halikuwa la waongofu tu wasio Wayahudi katika eneo moja wala halikutumika kwa kipindi kifupi tu.

32, 33 Eusebio anasema nini kuhusu kutambuliwa kwa katazo la damu katika siku yake?

32 Lakini hali ilikuwa nini katika karne za baadaye wakati Ukristo ulipoenea kuingia mahali pengi pa mbali? Acheni tuifikirie ithibati kutoka karne zilizofuata kutangazwa kwa ule uamuzi rasmi uliorekodiwa katika Matendo 15:28, 29, NW.

33 Eusebio, mwandikaji wa karne ya tatu anayefikiriwa kuwa ndiye “baba ya historia ya Kanisa,” anasimulia lililotukia katika Lyons (sasa katika Ufaransa) katika mwaka 177 W.K. Maadui wa kidini walishtaki Wakristo kwa ubandia juu ya kula vitoto vichanga. Wakati wa kuteswa-teswa na kuuawa kwa Wakristo fulani, msichana mmoja jina lake Biblias alijibu hilo shtaka bandia, akisema: “Ni jinsi gani sisi tunaweza kula vitoto vichanga—sisi, ambao kwetu si jambo la kisheria kula damu ya wanyama.”7

34-36. Ni nini walilosema Tertulliano na Minusio Feliki kwa habari ya Wakristo kutokula damu katika siku yao?

34 Mashtaka bandia yanayofanana na hilo yalisukuma Tertulliano mwanathelojia Mlatini wa mapema (yapata 160-230 W.K.) aonyeshe wazi kwamba ingawa kwa kawaida Waroma walikunywa damu, kwa uhakika Wakristo hawakufanya hivyo. Yeye anaandika hivi:

“Acheni njia zenu zisizo za asili ziaibishwe mbele ya Wakristo. Sisi hata hatuna damu ya wanyama kwenye milo yetu, kwa maana hii ina chakula cha kawaida. . . . Kwenye majaribu ya Wakristo ninyi mnawapa masoseji yaliyojazwa damu. Bila shaka, ninyi mnasadiki sana kwamba kitu chenyewe kile ambacho kwa hicho mnajaribu kuwafanya waache njia inayofaa si halali kwao. Inakuwaje kwamba, mkiwa na hakika ya kwamba watakirihi damu ya mnyama, mnaitikadi wataitamani sana damu ya kibinadamu?”8

35 Pia, akirejeza kwenye ule uamuzi rasmi wa Matendo 15:28, 29, yeye anasema: “Sisi tutalielewa lile katazo juu ya ‘damu’ kuwa ni [katazo] zaidi sana juu ya damu ya kibinadamu.”9

36 Minusio Feliki, mwanasheria Mroma aliyeishi mpaka yapata 250 W.K., anatokeza jambo ilo hilo, akiandika hivi: “Sisi tunaiepuka sana damu ya kibinadamu, hivi kwamba hatutumii damu hata ya wanyama wanaolika.”10b

37, 38. Ni taarifa gani alizotoa Askofu na mwanachuo wa Biblia Mkatoliki juu ya kisa cha damu?

37 Ithibati ya kihistoria ni nyingi na wazi sana hivi kwamba Askofu John Kaye (1783-1853) angeweza kutaarifu wazi kabisa hivi: “Wale Wakristo wa Kizamani walitii kwa uangalifu uamuzi rasmi uliotamkwa na Mitume katika Yerusalemu, katika kushika mwiko wa vitu vilivyonyongwa na wa damu.”11

Lakini je! hao ‘Wakristo wa kizamani’ na Mashahidi wa Yehova katika nyakati za ki-siku-hizi ndio watu pekee ambao wamekuwa na maoni kama hayo yanayotegemea msingi wa Biblia?

38 Sivyo hata kidogo. Akieleza juu ya Matendo 15:29, msomi wa Kibiblia Mkatoliki Giuseppe Ricciotti (1890-1964) anarejeza kwenye kile kituko cha kule Lyons (kilichotangulia kuelezewa) kuwa ni ithibati ya kwamba ‘Wakristo wa mapema hawangeweza kula damu.’ Ndipo yeye anaongezea hivi, “lakini hata katika karne zilizofuata mpaka kwenye Enzi za Katikati, sisi tunakabili miangwi isiyotarajiwa ya hii ‘karaha’ ya mapema [ya damu], ambayo bila shaka ni kwa sababu ya ule uamuzi rasmi.”12

39. Baraza la Kwiniseksiti lilitaarifu nini kuhusu damu, na Otto wa Bamberg alisema nini kwa waongofu wapya kuhusu damu?

39 Mathalani, Baraza la Kwiniseksiti lililofanywa katika 692 W.K. kule Konstantinopo lilitaarifu hivi: “Andiko la kimungu linatuamuru tushike mwiko wa damu, wa vitu vilivyonyongwa, na wa uasherati. . . . Ikiwa mtu ye yote kuanzia sasa na kuendelea anajasiria kula kwa njia yo yote damu ya mnyama, ikiwa yeye ni kiongozi wa kidini, acheni huyo ashushwe cheo; ikiwa ni mtu wa kawaida tu, acheni huyo akatiliwe mbali.”13 Vivyo hivyo, Otto wa Bamberg (yapata 1060-1139 W.K.), mwenye daraja kuu katika kanisa na mwevanjeli mashuhuri, alieleza waongofu katika Pomerania “kwamba haiwapasi kula kitu cho chote kisicho safi, au ambacho kilijifia chenyewe, au kilichonyongwa, au kilichodhabihiwa kwa sanamu, au damu ya wanyama.”14

40. Martin Lutheri aliandika nini kuhusu Matendo 15:28, 29

40 Tukisogea karibu na wakati wetu, Martin Lutheri pia alitambua ile midokezeo ya uamuzi rasmi wa 49 W.K. Katika kuteta juu ya mazoea na itikadi za Kikatoliki, yeye alikuwa na mbetuko wa kutia lile baraza la kimitume katika kikundi kimoja na mabaraza ya kanisa ya baadaye ambayo maamuzi yayo rasmi hayakuwa sehemu ya Biblia. Hata hivyo, Lutheri aliandika hivi kuhusu Matendo 15:28, 29:

“Sasa ikiwa sisi tunataka kuwa na kanisa linalotii baraza hili (kama ilivyo sawa, kwa kuwa ndilo baraza la kwanza na la mbele kabisa, na lilifanywa na mitume wenyewe), ni lazima tufundishe na kusisitiza kwamba kuanzia sasa na kuendelea mwana-mfalme, bwana, mwananchi wa tabaka la kati, au mkulima ye yote asile bata, paa jike, paa dume, au nyama-nguruwe iliyopikwa ndani ya damu . . . Na wananchi wa tabaka la kati na wakulima lazima washike mwiko hasa wa soseji nyekundu na soseji yenye damu.”15

41. Ni elezo gani alilofanya mwanatheolojia Mbaptisti juu ya Mwanzo 9:3, 4?

41 Katika karne ya kumi na tisa Andrew Fuller, ambaye alionwa kuwa “labda ndiye mwenye sifa na umashuhuri zaidi miongoni mwa wanatheolojia Wabaptisti,” aliandika hivi kwa habari ya katazo la Mwanzo 9:3, 4 juu ya damu:

“Kwa kuwa ilikatazwa kwa Noa, hii inaonekana ilikuwa imekuwa yenye kukatazwa kwa aina ya binadamu wote; wala katazo hili halipasi kutendewa kama la sherehe za kipindi cha Wayahudi tu. Haikuamriwa kabla ya kipindi hicho tu, bali pia ililazimishwa na yale maamuzi rasmi ya mitume ifuatwe na Wakristo wasio Wayahudi, Matendo XV. 20. . . . Damu ndio ule uhai, na Mungu anaonekana kuudai kuwa wenye utakato kwake mwenyewe.”16

42. Ni jibu gani ambalo William Jones kiongozi wa kidini aliwapa wale ambao wangepuuza katazo la Biblia juu ya damu?

42 Je! Mkristo angeweza kudai kwamba kujizoeza kile ambacho watu fulani wanakiita “uhuru wa Kikristo” kunapasa kumruhusu apuuze katazo hili juu ya damu? Katika kitabu chake The History of the Christian Church, kiongozi wa kidini William Jones (1762-1846) anajibu hivi:

“Hakuna kitu kinachoweza kuwa wazi sana kuliko lile katazo, Matendo XV. 28, 29. Je! wale wanaotetea ‘uhuru wao wa Kikristo’ kuhusiana na jambo hili wanaweza kuonyesha sehemu yo yote ya Neno la Mungu ambamo katazo hili linakuja kufutwa baadaye? Ikiwa sivyo, na turuhusiwe kuuliza, ‘Ni kwa mamlaka gani, isipokuwa yake mwenyewe, yo yote ya sheria za Mungu inaweza kubatilishwa?’”—Uku. 106.

43. Ni azimio gani la Mashahidi wa Yehova kuhusu damu, likitegemezwa juu ya mambo ya uhakika na maandiko gani?

43 Neno mkataa ni wazi: Chini ya mwongozo wa roho takatifu lile baraza la kimitume liliamua rasmi kwamba lazima Wakristo wanaotaka kibali cha Mungu ‘washike mwiko wa damu,’ kama vile Mungu alivyokuwa ametaka tangu siku za Noa. (Matendo 15:28, 29; Mwanzo 9:3, 4, NW) Maoni haya ya Kimaandiko yalikubaliwa na kufuatwa na Wakristo wa mapema, hata wakati kufanya hivyo kungegharimu uhai wao. Na tangu hapo katika muda wote wa karne zilizopita, takwa hili limetambuliwa kuwa la “lazima” kwa Wakristo. Hivyo azimio la Mashahidi wa Yehova kushika mwiko wa damu hutegemea msingi wa Neno la Mungu Biblia na hutegemezwa na visa vingi vya zamani vinavyotoa kielelezo katika historia ya Ukristo.

Damu Ikiwa Dawa

44. Ni mambo gani matatu ambayo yamethibitishwa, na ni upi ulio msingi wa Kimaandiko kwa kila moja?

44 Kufikia hapa tumethibitisha kwamba Biblia inataka yanayofuata: Mwanadamu hapaswi kuendeleza uhai wake kwa damu ya kiumbe mwingine. (Mwanzo 9:3, 4) Wakati uhai wa mnyama unapotolewa, ile damu inayowakilisha uhai huo inapasa ‘kumiminwa nje,’ itolewe kwa kumrudishia Mpaji-Uhai. (Walawi 17:13, 14, NW) Na kama ilivyoamuliwa rasmi na baraza la kimitume, Wakristo wanapaswa ‘kushika mwiko wa damu,’ ambao unatumika kwa damu ya kibinadamu na pia kwa damu ya wanyama.—Matendo 15:28, 29, NW.

Hata hivyo, je! taarifa hizi za Kibiblia zinatumika kwa ukubali wa damu yenye kutiwa mishipani ukiwa utaratibu wa kitiba wa kuokolea uhai?

45, 46. Ni swali gani linalojitokeza lenyewe sasa, na ni mbinu gani za kitiba za ki-siku-hizi ambazo huenda kanuni za Biblia zikasemwa kuwa zinatiwa ndani?

45 Watu fulani hubisha kwamba Biblia inakataza kula damu ikiwa chakula na kwamba kwa msingi hilo ni jambo tofauti na kukubali kutiwa damu mishipani, huo ukiwa ni utaratibu wa kitiba ambao haukujulikana katika nyakati za Biblia. Je! msimamo huo ni halali?

46 Hakuna kukana kwamba katika nyakati za Biblia sheria ya Mungu ilikuwa na utumiko mahususi juu ya kula damu ikiwa chakula. Uingizaji damu mishipani haukuzoewa wakati huo. Lakini, hata ingawa Biblia haikuzungumzia mbinu za ustadi wa tiba ya ki-siku-hizi zinazohusisha damu, kwa uhakika ilizitarajia na kuzitia ndani kwa njia ya kanuni.

47, 48. Ni tofauti gani isiyofanywa katika Matendo 15:29, na kwa sababu zipi?

47 Mathalani, angalia ile amri ya kwamba Wakristo ‘waendelee kushika mwiko wa damu.’ (Matendo 15:29, NW) Hakuna linalotaarifiwa hapo ambalo lingetetea haki ya kufanya tofauti kati ya kutwaa damu kwa kuiingiza katika kinywa na kuitwaa kwa kuiingiza katika mishipa ya damu. Na, kwa kweli, je! kwa njia ya kanuni kuna tofauti yo yote ya msingi kati ya mambo hayo?

48 Madaktari wanajua kwamba mtu anaweza kulishwa kupitia kinywani au mishipani. Hali kadhalika, dawa fulani zinaweza kuingizwa kupitia njia mbalimbali. Mathalani, dawa fulani ambazo ni viua-vijasumu zinaweza kutwaliwa mdomoni kwa namna ya vibonge au kuingizwa kwa kumdunga mtu sindano katika misuli yake au mfumo wa uenezaji damu (mishipani). Vipi ikiwa wewe ulikuwa umemeza kibonge fulani cha kiua-kijasumu na, kwa sababu ya mwili wako kupatwa na matokeo hatari kwa sababu ya dawa hiyo, ukaonywa ushike mwiko wa dawa hiyo wakati ujao? Je! lingekuwa jambo la kiakili kufikiria onyo hilo la kitiba kuwa linamaanisha hungeweza kumeza dawa ile kwa namna ya kibonge lakini ungeweza kwa usalama kuitia katika mkondo wa damu yako? Hasha! Jambo kubwa halingekuwa ile njia ya uingizaji, bali kwamba inakupasa wewe ushike mwiko kabisa wa kiua-vijasumu hicho. Vivyo hivyo, kwa uwazi ule uamuzi rasmi wa kwamba lazima Wakristo ‘washike mwiko wa damu’ unatia ndani utwaaji wa damu mwilini, iwe ni kupitia kinywani au moja kwa moja ndani ya mkondo wa damu.

Suala hili ni la maana jinsi gani kwa Mashahidi wa Yehova?

49. Ni msimamo gani thabiti ambao Mashahidi wa Yehova wanachukua, nao wanasadikishwa juu ya nini?

49 Watu wanaotambua tegemeo lao juu ya Muumba na Mpaji-Uhai wanapaswa waazimie kutii amri zake. Huu ndio msimamo thabiti ambao Mashahidi wa Yehova wanachukua. Wao wanasadikishwa kikamili kwamba ni sawa kutii sheria ya Mungu inayoamuru kushika mwiko wa damu. Katika jambo hili wao hawafuati kiwazo fulani cha kibinafsi au oni fulani la ushupavu lisilo na msingi. Ni kwa sababu ya utiifu kwa mamlaka iliyo juu zaidi katika ulimwengu wote mzima, yule Muumba wa uhai, kwamba wao wanakataa kutwaa damu ndani ya mifumo yao ama kwa kuila ama kwa kutiwa mishipani.

50, 51. Ni nini kilicho hatarini katika suala la damu, nasi tunakubali maneno gani ya mtunga zaburi kwa moyo wote mzima?

50 Kwa hiyo, suala la damu kwa Mashahidi wa Yehova linahusisha ndani kanuni zilizo za msingi zaidi ambazo wao wakiwa Wakristo wanategemeza uhai wao. Uhusiano wao na Muumba na Mungu wao umo hatarini. Zaidi ya hilo, wao wanaitikadi kwa moyo wote mzima maneno ya mtunga zaburi: “Maamuzi ya kihukumu ya Yehova ni ya kweli; hayo yamethibitika kuwa ya uadilifu kabisa kabisa. . . . Katika kuyashika mna thawabu kubwa.”—Zaburi 19:9, 11, NW.

51 Watu fulani wanaotazama ile athari ya muda mfupi tu ya maamuzi yanayofanywa huenda wakatia shaka kama kutii sheria ya Mungu kuhusu damu kunaweza kufikiriwa kuwa jambo la ‘kuthawabisha.’ Lakini Mashahidi wa Yehova wana uhakika kwamba kutii mielekezo kutoka kwa Muumba wao ni kwa wema wao wa kudumu.

52, 53. Ni msimamo gani waliochukua Wakristo wa kwanza na kwa gharama gani kwao wenyewe?

52 Wakristo wa mapema walihisi ivyo hivyo. Historia inaonyesha kwamba nyakati nyingine utiifu wao kwa Mungu ulitahiniwa mpaka upeo. Katika Milki ya Kiroma wao walitiwa chini ya mfinyo wa kufanya vitendo vya ibada ya sanamu au kujitia katika ukosefu wa adili. Kukataa kwao kukubali kungeweza kumaanisha kutupwa ndani ya uwanja wa Kiroma, wararuliwe na wanyama wabaya sana. Lakini Wakristo hao waligandamana na imani yao; wao walitii Mungu.

53 Fikiria jambo hilo lilihusisha nini ndani. Kwa Wakristo wa mapema waliokuwa wazazi, kukataa kuvunja sheria ya Mungu kungaliweza hata kuleta kifo juu ya watoto wao. Na bado sisi tunajua kutokana na historia kwamba Wakristo hao hawakugeuza kisogo kwa Mungu na kanuni walizoishi kwazo kwa kujawa na woga na kukosa imani. Wao waliitikadi maneno ya Yesu: “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Yeye ambaye huzoea imani katika mimi, hata ingawa yeye anakufa, atakuja kwenye uhai.” (Yohana 11:25, NW) Kwa sababu hiyo, ijapokuwa ile gharama ya papo hapo, Wakristo hao walitii uamuzi rasmi wa kimitume kushika mwiko wa vitu vilivyodhabihiwa kwa sanamu, wa uasherati na wa damu. Uaminifu kwa Mungu ulikuwa wa maana kwao kadiri hiyo.

54. Ni daraka gani ambalo Mashahidi wa Yehova wanabeba?

54 Huo ni wa maana kadiri hiyo leo kwa Mashahidi wa Yehova pia. Kwa kufaa wao wanahisi wana wajibu wa kiadili wa kujifanyia wenyewe na watoto wao maamuzi yanayohusu ibada. Kwa sababu hiyo, Mashahidi wa Yehova hawatafuti mtu mwingineye yote, awe ni daktari, msimamia mipango ya hospitali au hakimu fulani, awafanyie hayo maamuzi ya kiadili. Wao hawataki mtu mwingineye yote ajaribu kuwabebea daraka lao kwa Mungu, kwa maana kwa ukweli hakuna mtu mwingineye anayeweza kufanya hivyo. Hilo ni daraka la kibinafsi la Mkristo kuelekea Mungu wake na Mpaji-Uhai.

Je! Kukataa Ni Namna ya Ujiuaji?

55, 56. (a) Ni pingamizi gani linalozuka kwa kukataa kutiwa damu mishipani? (b) Kwa nini Mashahidi hawawezi kushtakiwa ujiuaji, kama inavyoonwa na ushuhuda wa wengine?

55 Usoni mwa upotevu mwingi sana wa damu kutokana na jeraha, ugonjwa au matatanisho ya upasuaji, mara nyingi damu imetumiwa kwa jaribio la kuhifadhi uhai. Kwa sababu hiyo, wakati watu wanaposikia kwamba mtu fulani anakataa kutiwa damu mishipani, huenda wao wakahisi kwamba hakika yeye anajiondolea uhai wake mwenyewe. Je! ndivyo?

Je! kukataa kutiwa damu mishipani ni “ujiuaji” au ni zoezi la “haki ya kufa” [ya mtu]?

56 Ujiuaji ni mtu kutafuta kujiondolea uhai wake mwenyewe. Ni jaribio la kujiangamiza. Lakini hata mtu ye yote anayejua itikadi na mazoea ya Mashahidi wa Yehova anaweza kuona kwamba wao hawafanyi jaribio la kujiangamiza. Ingawa wao wanakataa kutiwa damu mishipani, wao wanakubali usaidizi wa kitiba wa namna nyingine. Makala moja katika The American Surgeon ilieleza hivi kwa usahihi:

“Kwa ujumla, kukataa utunzaji wa kitiba si sawa na ‘kujiua.’ Mashahidi wa Yehova wanatafuta uangalizi wa kitiba lakini wanakataa uso mmoja tu wa utunzaji wa kitiba. Kukataa utunzaji wa kitiba au sehemu fulani za huo si ‘uhalifu’ wa mtu kujifanyia mwenyewe kwa kitendo cha waziwazi cha mmoja kutaka kuangamiza, kama ulivyo ujiuaji.” (Italiki zimeongezwa.)17

Profesa Robert M. Byrn alionyesha wazi katika Fordham Law Review kwamba ‘kukataa njia ya kutibu iliyo ya kuokoa uhai na jaribio la ujiuaji ni mambo tofauti katika sheria kama vile matofaa na machungwa yalivyo tofauti.’18 Na, akihutubia kongamano la kitiba, Dakt. David Pent wa Arizona alitoa maoni haya:

“Mashahidi wa Yehova wanahisi kwamba, ikiwa ni lazima wafe kwa sababu ya kukataa kwao kutiwa damu mishipani, wao wanakufa kwa ajili ya itikadi zao kwa njia inayofanana sana na vile wafia-dini wa mapema walivyofanya karne nyingi zilizopita. Ikiwa huu ni ujiuaji wa kitiba wa kutojifanyia, kuna matabibu kadhaa walio kati ya hadhira hii sasa hivi ambao wanavuta sigareti, na labda hiyo ni sawa kabisa na ujiuaji wa kutojifanyia.”19

57. Kwa nini kukataa kutiwa damu mishipani si zoezi la “haki ya kufa”?

57 Namna gani lile wazo la kwamba kwa kukataa kutiwa damu mishipani Mashahidi wa Yehova wanajizoeza “haki ya kufa”? Uhakika ni kwamba Mashahidi wa Yehova wanataka kukaa wakiwa hai. Hiyo ndiyo sababu wao wanatafuta msaada wa kitiba. Lakini wao hawawezi na hawatakiuka masadikisho yao ya kidini yenye msingi wa Biblia, yaliyo ndani yao kwa kina kirefu.

58. Ni haki zipi ambazo mahakama zimewapa watu mmoja mmoja, na kwa nini ndivyo ilivyo kimantiki?

58 Mara nyingi mahakama zimetegemeza ile kanuni ya kwamba kila mtu ana haki ya kushika ukamilifu wa kimwili, ikimaanisha kwamba katika uchanganuzi wa mwisho mtu mwenyewe ndiye mwenye daraka la kuamua litakalofanywa na mwili wake. Kwa kweli, je! hivyo sivyo wewe ungetaka iwe ikiwa ungekuwa mgonjwa au umelazwa hospitalini? Kwa kuwa ni uhai wako, afya yako na mwili wako, je! haikupasi wewe utoe uamuzi wa mwisho juu ya kama jambo fulani litafanywa kwako au la?

59, 60. (a) Mgonjwa ni mwamuzi wa mwisho juu ya nini? (b) Haki na wajibu wa tabibu unawekewa hadi na uhuru gani wa mwanadamu?

59 Kuna matokeo ya kimantiki ya oni hili la ueledi na la kiadili. Kijitabu kimoja kilichofanyizwa na American Medical Association kinaeleza hivi: “Lazima mgonjwa awe ndiye mwamuzi wa mwisho juu ya kama yeye atachukua nafasi za kukubali matibabu au upasuaji unaopendekezwa na daktari au atajasiria hatari ya kuishi bila. Hiyo ndiyo haki ya kiasili ya mtu mmoja mmoja yule, ambayo sheria inaitambua.” “Mgonjwa ana haki ya kukataa kutoa idhini yake ya kupata matibabu ya kuokoa uhai. Kulingana na hilo, yeye anaweza kuwekea idhini yake kanuni, masharti, na hadi hizo ambazo yamkini kutamani kuweka.”20

60 Hiyo ni kweli kwa habari ya kutiwa damu mishipani sawasawa na ilivyo kwa habari ya “matibabu ya kuokoa uhai” mengineyo yote. Dakt. jur. H. Narr wa Tübingen, Ujeremani, alitaarifu hivi: “Haki na wajibu wa tabibu kuponya unawekewa hadi na uhuru wa msingi ambao mwanadamu anao wa kujiamulia anayotaka kuhusu mwili wake mwenyewe. . . . Jambo hilo ni kweli pia kwa hatua nyingineyo ya kujiingiza kati kitiba, na hivyo pia kwa katao la kutiwa damu mishipani.”21

61. Watu fulani wana mwelekeo gani kuhusu kuhifadhi uhai, lakini jambo hili linatokeza swali gani?

61 Ni jambo la kueleweka kwamba watu fulani wanashtushwa na ile fikira ya mtu ye yote kukataa damu ikiwa kufanya hivyo kungeweza kuwa hatari sana hata kulete kifo. Wengi wanahisi kwamba uhai ndicho kitu cha kutanguliza mbele, kwamba uhai ni wa kuhifadhiwa vyo vyote vile. Ni kweli, hifadhi ya uhai wa kibinadamu ni moja la mapendezi yaliyo ya maana zaidi ya jamii ya watu. Lakini je! hii inapasa kumaanisha kwamba “kuhifadhi uhai” kunakuja mbele ya kanuni iwayo yote?

62. Kulingana na N. L. Cantor, ni nini linaloonyesha kwamba utakato wa uhai silo la maana kupita yote, na hili lingetolewaje kielezi?

62 Kwa kujibu, Norman L. Cantor, Profesa Mshirika kwenye Shule ya Sheria ya Rutgers, alionyesha wazi hivi:

“Fahari ya kibinadamu inaongezewa kwa kuruhusu mtu mmoja mmoja yule ajiamulie mwenyewe ni itikadi gani zinazostahili kufiwa. Katika muda wote wa enzi zilizopita, umati wa visa vyenye maana sana, vya kidini na vya kilimwengu, vimeonwa kuwa vinastahiki kujidhabihu. Kwa uhakika, serikali na jamii za watu zilizo nyingi, zetu wenyewe zikitiwa ndani, hazioni utakato wa uhai kuwa wenye kima kupita yote.”22

Bw. Cantor alitoa kielelezo cha uhakika wa kwamba nyakati za vita wanaume fulani walikuwa na nia ya kukabili majeraha na kifo kwa kupigania “uhuru” na “demokrasi.” Je! wananchi wa kwao waliziona dhabihu hizo zilizofanywa kwa ajili ya kanuni kuwa ni zenye makosa kiadili? Je! mataifa yao yalishutumu mwendo huu kuwa usio wa kisharifu, kwa kuwa baadhi ya wale waliokufa waliacha nyuma wajane au mayatima wenye kuhitaji utunzaji? Je! wewe unahisi kwamba wanasheria au madaktari wangalipaswa kuwa wametafuta maagizo ya mahakama kuzuia wanaume hawa wasifanye dhabihu kwa ajili ya shabaha zao? Kwa sababu hiyo, je! si wazi kwamba nia ya kuzikubali hatari kwa ajili ya kanuni si jambo la Mashahidi wa Yehova na wale Wakristo wa mapema peke yao? Uhakika ni kwamba ushikamanifu huo kwenye kanuni umejaliwa sana na watu wengi.

63. Ni msimamo gani wa Mashahidi unaozuia mtu mwingineye yote asijaribu kuwapa kinguvu utibabu fulani unaovunja kanuni zao?

63 Pia, inastahiki kukazia tena kwamba, ingawa Mashahidi wa Yehova hawakubali kutiwa damu mishipani, wao wanakaribisha njia nyingine za matibabu ambazo huenda zikasaidia waendelee kuwa hai. Kwa nini, basi, mtu mwingineye yote apaswe kusisitiza na hata kutumia kinguvu utibabu fulani unaovunja kabisa kanuni za mtu na itikadi za kidini anazofuata kwa kina kirefu sana?

64. Katika jarida moja la kitiba, ni taarifa gani iliyotolewa juu ya madaktari wanaojaribu kutumia kinguvu utibabu fulani unaoharibu dhamiri ya mgonjwa?

64 Hata hivyo jambo hilo limetukia. Madaktari fulani au wasimamia mipango ya hospitali hata wameenda mahakamani wakapewe mamlaka ya kisheria kumpa mtu damu kinguvu. Kuhusu wale ambao wamefuata mwendo huu, Dakt. D. N. Goldstein aliandika hivi katika The Wisconsin Medical Journal:

“Madaktari wenye kuchukua msimamo huu wamekana zile dhabihu za wafia-imani wote ambao wametukuza historia kwa bidii yao ya kujitoa kabisa kwenye kanuni hata kwa kupata hasara ya uhai wao wenyewe. Kwa maana wagonjwa wale wanaochagua kifo fulani badala ya kuvunja usitaji wa kidini ni wa namna moja na wale waliolipa uhai wao kwa ajili ya imani katika Mungu au walioenda kutundikwa mtini badala ya kukubali ubatizo [wa kinguvu]. . . . Wetu ni wajibu wa kuokoa uhai lakini ingefaa hata tutokeze swali juu ya kama sisi hatuna pia wajibu wa kulinda salama ukamilifu na kuhifadhi zile ishara chache za uhakika wa kibinafsi zinazoendelea kutukia katika jamii inayokandamizwa kwa jinsi inayoongezeka. . . . Hakuna daktari anayepaswa kutafuta usaidizi wa kisheria ili kuokoa mwili kwa kuangamiza nafsi. Uhai wa mgonjwa ni wake mwenyewe.”23

Jukumu la Daktari

65, 66. Kwa nini huenda daktari akaona inataabisha kushughulika na Shahidi anayekataa kutiwa damu mishipani?

65 Tumeona kwamba, kwa sababu ya itikadi zao imara za kidini, Mashahidi wa Yehova wanaepuka vyote viwili, chakula kilicho na damu na damu inayotumiwa kitiba. Lakini ni jinsi gani wengine wanavyoathiriwa na msimamo huu, kama vile madaktari wanaotibu wagonjwa Mashahidi?

66 Madaktari wamejitoa kwa ajili ya uokoaji au urefushaji wa uhai. Hiyo ndiyo kazi yao. Basi, daktari aliyesomea kuona utiaji damu mishipani kuwa zoea lililokubaliwa anapotibu mgonjwa mahututi au ambaye amepoteza damu nyingi, huenda akaona inataabisha kupata habari kwamba mgonjwa anakataa damu. Ijapokuwa huenda dhamiri ya mgonjwa iliyozoezwa na Biblia isiruhusu atiwe damu mishipani, tabibu yule, pia, ana dhamiri na anafuata maadili ambayo kwake ni ya maana sana sana.

Je! daktari afuate mazoezi na masadikisho yake mwenyewe ya kitiba ikiwa anahisi kwamba, ingawa mgonjwa anakataa, kutiwa damu mishipani kunahitajiwa ili kuokoa uhai wake?

67, 68. Ni kulingana na kanuni gani za kisheria na kitiba huenda daktari mpasuaji asifuate masadikisho yake mwenyewe ikiwa yanaharibu dhamiri ya mgonjwa?

67 Hakuna shaka kwamba katika visa kama hivyo hali ya kutatanisha inakuwako. Lakini kila mmoja wetu anaweza kuuliza: Kama mimi ningekuwa katika hali ambamo mna mhitilafiano kati ya dhamiri yangu mimi mgonjwa na usadikisho wa moyo mweupe wa tabibu mwenye kutumikia, ni mwendo gani ambao mimi ningefikiri unapasa kufuatwa? Fikiria maneno yaliyosemwa na Dakt. William P. Williamson kwenye Kongresi ya Kitaifa ya Kwanza Juu ya Maadili ya Kitiba na Uprofeshonali:

Kwa uhakika, fikira ya kwanza ya tabibu lazima iwe hali njema ya mgonjwa. Kwa kuwa uhai ni zawadi ya Muumba kwa mtu, kwa haki uamuzi wa msingi ni wa mgonjwa, kwa sababu mgonjwa ndiye mwenye kabidhi ya zawadi hiyo. . . . Tabibu anapaswa kutibu mgonjwa bila kuruka mipaka ya maagizo ya dini ya mgonjwa, wala asiweke kinguvu masadikisho yake mwenyewe ya kidini juu ya mgonjwa.” (Italiki zimeongezwa.)24

68 Kuna sababu nyingine, ya kisheria, inayofanya iwe lazima dhamiri ya mgonjwa isikandamizwe. Kama vile Profesa Byrn alivyoandika katika Fordham Law Review: “ . . . Mimi simaanishi kwamba daktari anafungwa na wajibu wa kufuata uchaguzi wa mgonjwa ili afanye jambo fulani lililo kinyume cha dhamiri ya daktari. . . . Mimi namaanisha kwamba mgonjwa hafungwi na wajibu wa kufuata dhamiri ya daktari ili afanye jambo fulani lililo kinyume cha uchaguzi wa mgonjwa, na basi huenda daktari akawa na haki na uchaguzi wa kufanya bure. Ile sheria ya idhini yenye kupashwa habari ingefanywa iwe bila maana ikiwa uchaguzi wa mgonjwa ungetiishwa chini ya uamuzi wa kitiba wenye kutegemea dhamiri.” (Italiki zimeongezwa.)25

69, 70. Badala ya kuachilia kisa fulani, daktari amepaswa afanye nini anapokabiliwa na katao la mgonjwa kutiwa damu mishipani?

69 Kuna uwezekano wa tabibu katika hali hii “kufanya bure,” yaani, kujiondoa kwenye kisa kile; lakini je! hiyo ndiyo njia nyingineyo pekee iliyopo? Katika makala yake “Taratibu za Upasuaji wa Dharura Katika Mashahidi wa Yehova Walio Watu Wazima,” Dakt. Robert D. O’Malley alieleza hivi: “Katao la mgonjwa kukubali kutiwa damu mishipani halipasi kutumiwa kuwa udhuru wa kuachiliwa na wanatiba.”26

70 Basi, daktari angeweza kufanya nini? Dakt. J. K. Holcomb alitaarifu hivi katika tahariri ya jarida moja la kitiba:

“Bila shaka, sisi, tulio matabibu, tunahisi tumevurugika akili, hata kukasirishwa, wakati mgonjwa fulani mwenye shingo ngumu anapokataa kukubali kile ambacho sisi tunaona kuwa ndicho kiwango kilichowekwa cha matibabu yanayopendelewa zaidi. Lakini, je! kwa haki sisi tunapaswa kuhisi hivyo wakati mgonjwa anapotaja itikadi fulani ya kidini kuwa ndiyo msingi wa kukataa kwake matibabu fulani? Ikiwa sisi wenyewe ni wenye haki, tutakiri kwamba katika zoea letu la siku kwa siku sisi huamua pamoja na wagonjwa wengi kwa ajili ya jambo fulani lililo punde kuliko utibabu bora wa kile kiwango cha kawaida. . . . Ikiwa sisi tunaweza kufanya hivyo kwa habari ya masadikisho yetu ya kitiba, je! haitupasi hali kadhalika kuwa na nia ya kufanya yote tuwezayo wakati masadikisho ya mgonjwa, hasa ya kidini, yanapotuzuia kumtolea kile ambacho sisi tungekiona kuwa ndiyo namna ya utibabu unaotamaniwa. Kwa kawaida, wagonjwa wenye sababu za kidini za kutokubali kutiwa damu, n.k. wana habari juu ya hatari za kitiba zinazohusika katika uamuzi wao, lakini wao wana nia ya kukubali hatari hizo, ila wanatuomba tufanye yale tuwezayo tu.”27

71. Ni nini linaloweza kusemwa juu ya wajibu mwingi wa kiadili wa wote wawili mgonjwa na daktari kuhusu utibabu ‘usio wa kikawaida’?

71 Kuna fikirio jingine juu ya ule upande wa kiadili wa jambo hili. John J. Paris, Profesa Msaidizi wa Maadili ya Kijamii, alionyesha wazi hivi: “Kuna ukubaliano mkubwa katika jumuiya za kitiba na za kiadili pia kwamba mtu ana wajibu wa kiadili kufanyiwa utibabu ‘usio wa kikawaida.’ Na ikiwa mgonjwa hana wajibu wa kiadili kufanyiwa utibabu ‘usio wa kikawaida’—hata kama huenda ukawa unafanywa na wote katika zoea la kikawaida—wala tabibu hana wajibu wo wote wa kiadili kuuandaa; wala hakimu kuuagiza.”28 Kwa ajili ya Mashahidi wa Yehova, wanaoelekeza maisha zao na Biblia, hakika kutiwa damu mishipani ni utibabu ‘usio wa kikawaida.’ Kwa uhakika, wamekatazwa kiadili.

Ushirikiano Kati ya Mgonjwa na Daktari

72. Ni msimamo gani wanaochukua Mashahidi kwa habari ya utibabu kwa ujumla, lakini isipokuwa nini?

72 Watu wote wanaohusika na jambo hili wanaweza kubaki wakiwa na uhakikishio wa kwamba Mashahidi wa Yehova si washupavu wanaopinga utunzaji wa kitiba. Kumbuka kwamba Luka, aliyeandika usimulizi wa Biblia juu ya ule uamuzi rasmi dhidi ya damu, yeye mwenyewe alikuwa tabibu. (Wakolosai 4:14) Hivyo, wakati Mashahidi wa Yehova ni wagonjwa au wana aksidenti fulani, wao hawatafuti ponyo fulani la kimuujiza la “kuponywa kwa imani.” Bali, wao wanatafuta msaada wa kitiba. Katika jambo hili wao hawajaribu kuwapa imla madaktari juu ya jinsi wanavyopaswa kujizoeza dawa au hata juu ya ushughulikiaji wa tatizo hususa ambalo wao wenyewe wanalo. Jambo lile moja wanaloomba kutoka madaktari bila kigeugeu ni kwamba damu isitumiwe.

73. Ni mambo gani ya uhakika ambayo Mashihidi wanathamini kuhusiana na msimamo wao wa damu?

73 Mashahidi wanajali sana mazoezi na uwezo wa watu walio katika uwanja wa tiba. Wao wanathamini kwa moyo mweupe madaktari wanaotumia ustadi wao kutibu mgonjwa, lakini wakifanya hivyo kupatana na itikadi za kidhamiri za mgonjwa. Mashahidi wanatambua kwamba inahitaji ushujaa kwa daktari kupasua mtu bila kuwa huru kutumia damu. Pia, inahitaji kipimo fulani cha ushujaa ili kutenda kinyume cha maoni ya wanatiba wenzake na kukubali kujizoeza dawa chini ya hali ambazo huenda zikaonwa kuwa hazifikii kile kiwango bora cha tiba.

74. Mashahidi wana habari juu ya uhakika gani, nao wana nia ya kukabili nini?

74 Kiasili, Mashahidi wa Yehova wana habari kwamba taratibu fulani za upasuaji huenda zikahusisha ndani upotevu mwingi sana wa damu hivi kwamba huenda daktari akaitikadi kwa haki kwamba taratibu hizo haziwezi kufuatwa kulingana na kanuni wanazotoa Mashahidi. Hata hivyo, upasuaji ulio mwingi unaweza kufanywa bila damu. Ni kweli kwamba huenda madaktari wakahisi kwamba kwa kutotumia damu upasuaji unafanywa uwe wa hatari zaidi. Lakini Mashahidi wana nia ya kukabili hatari hizo kwa msaada wa kishujaa wa madaktari.

75. Ni mkataa gani uliofikiwa katika kisa kimoja chenye kupita kiasi baada ya upasuaji wenye mafinikio bila damu?

75 Wakati wa mazungumzo ya kikoa kwenye Chuo Kikuu cha Pennsylvania, Dakt. William T. Fitz alisimulia kisa kimoja cha kupendeza. Kilihusisha ndani mgonjwa wa miaka 34 aliyekuwa ametokwa na damu nyingi sana kutokana na uvimbe wa utumbo mpana. Mwanamume huyo, mmoja wa Mashahidi wa Yehova, aliambia madaktari kwamba yeye ‘angefurahi kufanyiwa utaratibu wo wote wa upasuaji maadamu yeye hangepewa damu.’ Madaktari waliafikiana kupasua, wakiahidi kwamba damu haingetumiwa. Wakati wa upasuaji na baadaye, upotevu wa damu ulikuwa mkubwa sana hata hemoglobini ya mgonjwa yule, ambayo kwa kawaida huwa gramu 14 au 15, ikashuka kwenye gramu 2.4. Lakini yeye hakufa. Bali, hali yake ikawa thabiti halafu kihesabio cha damu yake kikapanda juu. Akieleza juu ya ahadi ya madaktari kutotumia damu, Dakt. Francis Wood, Mwenyekiti wa Idara ya Dawa, alisema: “Mimi nafikiri wewe ulikuwa na haki kamilifu ya kuahidi. Mwanamume huyo angekufa kama wewe hungepasua. Yeye alikuwa na fursa ya kupata nafuu likiwa ni tokeo la upasuaji huo wa bila damu; kwa hiyo, mimi nafikiri wewe ulikuwa na haki kamilifu ya kumpa fursa hiyo juu ya kanuni zake mwenyewe.”29

Kuondolea Madaktari Dhima

76. Kwa nini madaktari hawahitaji kuogopa kwamba Mashahidi watawashtaki kwa kutofanya kazi vizuri kwa sababu ya msimamo wao juu ya damu?

76 Madaktari wamo katika msimamo mgumu katika kutibu kisa cho chote kibaya sana, kwa maana kushindwa kutumia taratibu zote zinazopatikana huenda kukawahusisha ndani ya ushtakiwa wa kutofanya kazi vizuri. Hata hivyo, Mashahidi wa Yehova wana nia ya kuhimili daraka la kukataa kwao kutiwa damu mishipani. Wao watatia sahihi taarifa za kisheria zinazoondolea wafanya kazi wa kitiba na hospitali hangaiko lo lote juu ya mashtaka, itukiapo kwamba dhara litahesabiwa kuwa limesababishwa na kupasua kwao bila damu.

77. Ni sehemu gani muhimu ya fomu ambayo AMA hupendekeza itiwe sahihi na wagonjwa ambao wanakataa kutiwa damu mishipani?

77 American Medical Association limependekeza fomu moja yenye kichwa “Katao la Kutoa Ruhusa ya Kutiwa Damu Mishipani” kwa ajili ya wagonjwa ambao hawatakubali damu kwa sababu ya itikadi za kidini. Inasomwa hivi: “Mimi (Sisi) nina-(tuna-)omba kwamba damu yo yote au vitu vinavyotengenezwa kutokana na damu visitumiwe kwa ‐‐‐‐‐‐‐‐‐‐ wakati wa huku kulazwa hospitalini, hata ikiwa huenda kwa maoni ya tabibu anayemhudumia au wasaidizi wake utabibu huo ukafikiriwa ni wa lazima ili kuhifadhi uhai au kuendeleza hali ya kupona. Mimi (Sisi) nina-(tuna-)fungua tabibu mwenye kuhudumia, wasaidizi wake, hospitali na wafanya kazi wayo kutoka daraka lo lote lile la matokeo yo yote mabaya yanayoweza kutokana na katao langu (letu) la kutoa ruhusa ya utumizi wa damu au vitu vinavyotengenezwa kutokana na damu.”30 Hati hii inapasa kuandikwa tarehe na kutiwa sahihi na mgonjwa na mashahidi waliopo. Mtu wa ukoo wa karibu kama vile mwenzi wa ndoa au mzazi (ikiwa kisa ni cha mtoto) angeweza pia kutia sahihi fomu ile.

78. Mashahidi wanaonyeshaje kwamba wana nia ya kukubali daraka la kibinafsi kwa kukataa kutiwa damu mishipani?

78 Nia ya Mashahidi wa Yehova kukubali daraka la kibinafsi kuhusu msimamo wao juu ya damu inaonyeshwa zaidi na uhakika wa kwamba walio wengi kati yao wanatembea wakiwa na kadi iliyotiwa sahihi kuomba kwamba “Hakuna Kutiwa Damu Mishipani!” Hati hii inakiri kwamba mtia-sahihi anang’amua na kukubali yanayotiwa ndani ya kukataa damu. Hivyo, hata ikiwa yeye atapaswa kupoteza fahamu anapoletwa kwa daktari au kwenye hospitali, taarifa hii iliyotiwa sahihi inaonyesha wazi msimamo wake thabiti.

Je! daktari au hospitali ingeweza kuonwa ina dhima ikiwa damu haitolewi?

79. Ni nini ambalo limesemwa juu ya uwezekano wa daktari kushtakiwa kwa kutomtia kinguvu mgonjwa damu mishipani?

79 Makala moja katika University of San Francisco Law Review ilifikiria jambo hili. Ilieleza kwamba Hakimu Warren Burger, ambaye akawa Hakimu Mkuu wa Mahakama Kubwa Zaidi ya United States, alisema kwamba kesi inayohusu kazi iliyofanywa vibaya ‘ingeonekana kuwa isiyoungwa mkono’ katika kisa ambamo taarifa ya kisheria ilikuwa imetiwa sahihi. Makala hiyo iliendelea kusema:

“Uwezekano wa kushtakiwa kosa la jinai unakuwa mbali hata zaidi. Mwelezaji mmoja aliyeichunguza fasihi aliripoti kwamba, ‘Mimi nimekuwa siwezi kupata mamlaka yo yote ya taarifa ya kwamba tabibu angepatwa na . . . dhima [ya kosa la jinai] kwa kukosa kwake kumtia kinguvu damu mishipani mgonjwa asiyetaka.’ Hatari hiyo inaonekana zaidi kuwa zao tu la akili ya kisheria kuliko kuwa uwezekano wa kihalisi.”31

80. Ni msimamo gani ulio katika Uingereza mgonjwa anapokufa kwa sababu ya kuwa amekataa kutiwa damu mishipani?

80 Kwa mintarafu ya hiyo hali katika Uingereza, Emergencies in Medical Practice lilisema: “Ikiwa hali ya mambo imeonyeshwa wazi kwa mgonjwa naye anakufa bila kutiwa damu mishipani, hakuna hatua inayoweza kuchukuliwa dhidi ya daktari kwa maana hakuna mgonjwa anayewajibishwa kuhifadhi uhai wake kwa utumizi wa vipimo vya pekee au visivyo vya kikawaida.”32

81, 82. Daktari ana wajibu gani wa kiadili, lakini ni wajibu gani wa kiadili ambao hana?

81 Daktari anayefikiria kupasua mgonjwa atataka kiasili kueleza waziwazi ni nini zilizo hatari zinazowezekana kutokea kwa kukataa damu. Lakini mara akiisha kufanya hivyo, daktari hahitaji kuhisi wajibu wa kiadili kusonga jambo hilo zaidi. Kwa uhakika ingekuwa kinyume cha maadili kujaribu kumkazakaza mno au kumwogopesha mgonjwa ambaye ameamua kwa dhati kutokubali damu mpaka akubali.

82 Kwa kuwa Mashahidi wa Yehova wanakubali kwa nia daraka la uamuzi wao, kisheria na kwa hakika kiadili madaktari wanaondolewa wajibu wo wote wa kusisitizia damu. Na hivyo ndivyo matabibu wengi wenye kufuata maadili na wenye moyo mweupe wanavyopendelea iwe. “Mmoja hawezi kuonya haraka mno dhidi ya kudhoofishwa kwa haki ya kibinadamu ya kujiamulia mwenyewe, kutia na ile ya mgonjwa,” akaandika mpasuaji G. Haenisch wa Hamburg, Ujeremani. “Kupewa kwa tabibu haki ya kufanya utabibu ambao yeye anafikiria unafaa ingawa u kinyume cha kutaka kwa mgonjwa kwapasa kukataliwe katakata.”—Deutsche Medizinische Wochenschrift.33

83. Ni shtaka gani ambalo daktari angestahili ikiwa angemtia kinguvu damu mishipani mgonjwa aliye Shahidi?

83 Kwa sababu ya haki hii ya kibinadamu, vichapo vya kisheria na vya kitiba katika mabara fulani-fulani vimeonya-onya kwamba kutia damu mishipani dhidi ya matakwa ya mgonjwa kungeweza kufanya daktari (au wafanya kazi wa hospitali) wastahili mashtaka ya kushambulia na ya kuumiza mtu, au shtaka lenye sababu nzuri la kutofanya kazi vizuri.

Vipi kutumia damu mwilini bila kuambia mgonjwa, labda wakati yeye amepoteza fahamu?

84, 85. Ni mwendo gani wa daktari ambao ungekuwa “jambo la kuchukiza sana kimaadili” kwa daktari, na kwa nini hivyo?

84 Matabibu wengi wenye moyo mweupe wanahisi kwamba katika hali fulani-fulani, kama ile inayohusiana na kansa yenye kufisha, ni jambo la fadhili kutompa mgonjwa habari kamili juu ya hali yake. Ingawa huenda kukawa na kauli zenye kutofautiana juu ya kufaa kunyima mgonjwa habari juu ya hali yake, hiyo ni tofauti sana na daktari kufanya kimakusudi utibabu ambao anajua mgonjwa amekataza. Akiandika katika New York State Journal of Medicine, Dakt. Bernard Garner na washirika wake walikazia jambo hili. Wao walikiri kwamba nyakati fulani daktari ameacha mgonjwa Shahidi apoteze fahamu halafu akampa damu, labda akifikiri kwamba ‘Jambo asilojua halitamuumiza.’ Lakini wao walikata shauri hivi kwa mkazo: “Ingawa huenda matilaba yakawa ya kujali hali ya mwingine, hili lingekuwa jambo la kuchukiza sana kimaadili.”34

85 Sababu ya hilo kuwa hivyo ilionyeshwa wazi na Marcus L. Plante, Profesa wa Sheria, Chuo Kikuu cha Shule ya Sheria Michigan. Yeye aliandika kwamba “tabibu ana uhusiano wa kiamana [wenye kuasisiwa juu ya itibari] na mgonjwa wake na ana deni la wajibu kamili kabisa wa kutomwongoza vibaya kamwe mgonjwa kwa maneno au kimya kwa habari ya aina na tabia ya utaratibu wa kitiba anaopendekeza kufuata.”35

86, 87. (a) Medical Tribune ya Ujeremani Magharibi lililazimika kusema nini juu ya kumtia mgonjwa damu mishipani akiwa hana fahamu? (b) Ni amri gani iliyotolewa na mahakama iliyotilia nguvu msimamo huu, ikiongoza kwenye mkataa gani?

86 Waaidha, katika kata fulani, ni kosa kisheria daktari kuahidi kutompa mtu damu halafu kufanya hivyo kichinichini. Mathalani, katika Medical Tribune ya Ujeremani Magharibi ilionyeshwa wazi kwamba “hakuna jambo linalobadilishwa wakati mgonjwa hana fahamu.” Iko hivyo kwa sababu ‘katao la kukubali kutiwa damu mishipani, mara likiisha kutaarifiwa na mgonjwa mwenye uwezo, linakuwa ni halali pia ikija kutukia kwamba yeye anapoteza fahamu.’36 Ikitilia nguvu jambo hilo kwa mkazo mwingi zaidi, Mahakama Kubwa Zaidi ya Kansas ilitangaza rasmi hivi:

“ . . . Kila binadamu anaonwa kuwa bwana-mkubwa wa mwili wake mwenyewe, na yeye anaweza, ikiwa ana akili timamu, kukataza moja kwa moja tendo la upasuaji wa kuokoa uhai, au utibabu mwinginewo. Huenda daktari hata akaitikadi kwamba upasuaji au namna fulani ya utibabu inatamanika au inahitajiwa kabisa lakini sheria haimruhusu aweke uamuzi wake mwenyewe mahali pa ule wa mgonjwa kwa ufundi au udanganyifu wa namna yo yote.” (Italiki zimeongezwa.)37

87 Basi, kutia damu katika mishipa ya mmoja wa Mashahidi wa Yehova ni kinyume cha maadili ya kazi taalamu ya matabibu wa kiadili. Hiyo ingeweza kufanya daktari astahili hatua ya kisheria.

Kustahi Daraka la Kiuzazi

88, 89. (a) Ni upande gani wa habari hii ambao ni wenye kuwashwa sana hisia za moyoni? (b) Mashahidi wanahisije juu ya jambo hilo, na kwa nini?

88 Inaelekea kuwa upande wa jambo hili ambao ndio wenye kuwasha sana hisia za moyoni unahusisha ndani kutibu mtoto. Sisi sote tunang’amua kwamba watoto wanahitaji utunzaji na himaya. Hasa wazazi wanaoogopa Mungu wanathamini jambo hili. Wao wanapenda watoto wao kwa kina kirefu na wanahisi sana daraka walilopewa na Mungu kuwatunza na kufanya maamuzi kwa ajili ya hali njema yao ya kudumu.—Waefeso 6:1-4.

89 Jamii ya watu, pia, inatambua daraka la kiuzazi, ikikiri kwamba kwa msingi wazazi ndio wamepewa mamlaka ya kuandalia na kuamua kwa ajili ya watoto wao. Kimantiki, itikadi za kidini katika jamaa zinahusu jambo hili. Kwa uhakika watoto wananufaika ikiwa dini ya wazazi wao inakazia uhitaji wa kuwatunza. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mashahidi wa Yehova, ambao kwa njia yo yote hawataki kuzembea watoto wao. Wao wanautambua kuwa wajibu wao waliopewa na Mungu kuwaandalia chakula, mavazi, himaya na utunzaji wa kiafya. Waaidha, uthamini halisi juu ya uhitaji wa kuandalia watoto wa mtu unataka pia kukaza kikiki ndani yao ufuataji wa maadili na staha ya mema. Kama vile imetajwa, Wakristo wa mapema walikuwa kielelezo chema katika hili; wazazi walifundisha watoto wao na hata wao binafsi wakaishi kulingana na mafundisho ya kiadili waliyoyatamka. Historia inasimulia kwamba nyakati fulani jamaa nzima-nzima ziliachwa zife katika arena za Kiroma kwa sababu wazazi hawakutaka kuvunja itikadi zao za kidhamiri.

90. (a) Jambo gani limetokea kwa sababu ya ukosefu wa fundisho la wazazi? (b) Tofauti na hilo, wazazi Mashahidi wanafanya nini?

90 Sisi sote tuna habari kwamba ukosefu wa fundisho la kiuzazi na kielelezo cha kiadili umechangia uhakika wa kwamba vijana wengi leo hawana ubora wa kimsingi; katika utafutaji usiozuiwa na misisimuko, wao hawafikiri wanaweza kuhatarisha afya na uhai wao, na pia uhai wa wengine. Je! si bora sana vijana wawe na wazazi wanaoendeleza ufuataji wa maadili na staha ya kanuni bora? Wazazi ambao ni Mashahidi wa Yehova wanaonyesha upendo mkubwa kwa watoto wao na pia kwa Mungu wao kwa kutumia Biblia kusaidia watoto wao wawe watu wa kiadili. Hivyo, wakati watoto hawa wanapokuwa na umri wa kutosha kujua yale ambayo Biblia inasema kuhusu damu, wao wenyewe wanaunga mkono uamuzi wa wazazi wao ‘kushika mwiko wa damu.’—Matendo 15:29, NW.

Je! daktari anahitaji kuhisi kwamba inampasa kumpa mtoto damu bila kujali matakwa thabiti ya wazazi, na labda hata ya mtoto mwenyewe?

91, 92. Kwa nini daktari hapaswi kuhisi kwamba ni lazima amtie mtoto damu mishipani bila kujali matakwa thabiti ya wazazi kupinga hilo?

91 Kwa kusema wazi, kwa sababu ya ile haki inayotambuliwa sana ya daraka la kiuzazi, msimamo ulio wa kiadili, wa kanuni na wenye kupatana ni daktari kutambua lile daraka la wazazi wenye upendo na hangaikio la kuamua kwa ajili ya watoto wao wadogo.

92 Katika habari hii, Dakt. A. D. Kelly, Katibu wa Shirika la Tiba Kanada, aliandika kwamba “wazazi wa watoto wadogo na wale ambao ni wa ujamaa wa karibu na wagonjwa wasio na fahamu wana haki ya kufasiri mapenzi ya mgonjwa yule na kwamba sisi tunapaswa kukubali na kustahi matakwa yao. . . . Mimi sivutiwi na zile hatua za mahakama ya ujadili iliyokusanyika saa 8 za usiku ili kuondoa mtoto katika utunzi wa mzazi wake.”38

93. Kwa nini haipatani kimsingi kumtia kinguvu damu mishipani mtoto wa wazazi Mashahidi?

93 Watu fulani katika kazi za kitiba na za kisheria wametambua kwamba mtu mzima mwenye uwezo ana haki ya kukataa kutiwa damu mishipani. Lakini wao wameshikilia kwamba ikiwa wazazi wanakataa kutoa ruhusa kwa ajili ya mtoto wao, kutiwa damu mishipani kunapasa kutolewe kinguvu kwa agizo la mahakama. Hata hivyo, msimamo huu unakosa upatani na umoja wa kimsingi, kama ilivyoonyeshwa wazi katika jarida Forensic Science:

“Basi je! tudhani kwamba mahakama zina nia ya kugawia watoto dini iliyo tofauti na ile ya wazazi wao, hali takwimu zinaonyesha kwamba watoto walio wengi sana wanalelewa na kwa kweli wanafuata dhehebu lile lile la kidini kama la wazazi wao? Je! kwa kufanya hivyo mahakama hazingekuwa zikikiuka haki za kidini za watoto zilizo sawa na haki zile ambazo mahakama inajaribu kuzihami kwa ajili ya watu wazima chini ya lile Sahihisho la Kwanza [la Katiba] kwa kukataa utiwaji mishipani na kupendelea makatao ya mtu mzima? Je! mahakama haziwi ni kama zinawagawia watoto dini ikiwa zinakataa utiwaji mishipani kwa ajili ya watu wazima kwa misingi ya kidini na kuuruhusu kwa ajili ya watoto wa watu wazima hao hao?”39

94. Taja kutopatana kukubwa kunakopatikana katika hospitali fulani fulani.

94 Mara nyingi kuna kutopatana kukubwa kwa kiadili katika kutia kinguvu damu katika mishipa ya mtoto ambaye wazazi wake wameomba utibabu mwingine utumiwe. Kwenye hospitali fulani-fulani, huenda madaktari katika chumba kimoja wakawa wanatia kinguvu damu katika mishipa ya kitoto kichanga. Hata hivyo katika chumba kilicho karibu madaktari wengine huenda wakawa wanatoa mimba kisheria, wakikomesha uhai wenye miezi michache tu ukiwa mchanga kuliko mtoto yule anayetiwa damu kwa nguvu ‘ili kuokoa uhai’ eti. Hili limeongoza watu wenye kufikiri watake kujua kama sikuzote ‘kuhifadhi uhai’ ndilo suala halisi linalosababisha kutia kinguvu damu mishipani.

95. Mhadhiri Msikochi wa koleji alilazimika kusema nini juu ya kuwatia kinguvu damu mishipani watu wazima na watoto?

95 Fikiria vidokezi vya utibabu wenye mamlaka ya serikali, unaoondoa kinguvu haki ya daraka la mzazi. Katika Scotland, A. D. Farr, mhadhiri wa koleji moja kuhusiana na njia stadi za kutia damu mishipani, aliandika hivi kwa habari ya kutia damu kinguvu katika mishipa ya watu wazima na watoto:

96, 97. Ile kanuni ya kuchagua analotaka mtu katika utibabu inakanushaje kutia kinguvu damu mishipani?

96 Kule kutangua amri kwa mintarafu ya wachache wenye itikadi fulani ya kidini kunaendelezwa mpaka kunakuwa ni kutangua ile kanuni nzima ya mtu mzima kuruhusiwa kukubali au kukataa namna fulani ya utibabu. . . . Serikali inajitwalia pole kwa pole ile kazi ya kumfanyia mtu maamuzi. Ni kwa njia hii kwamba nchi zilizo huru zinaaacha kuwa huru na kuwa za utawala wa kutumia mabavu. Kwa kweli ilikuwa ni kwa kuwatwaa watoto Wajeremani na kuwaingiza katika harakati ya Vijana wa Hitler kwamba uhuru na ufaragha ulikuja kukandamizwa hatimaye katika Ujeremani ya Nazi. Hili si kisio la kuwaziwa tu. Uhuru ni mali ya thamani kubwa na iliyo adimu sana kulinganishwa, unaopasa kulindwa kwa wivu katika nchi zile ambamo umo. Mwingilio wo wote mmoja wa uhuru wa watu mmoja mmoja unasababisha mwingilio wa kupita kiasi.”40

97 Kuongezea, hata ikiwa kwa moyo mweupe daktari anaitikadi kwamba mtoto anahitaji kutiwa damu mishipani, je! hiyo inamaanisha kwamba utibabu mwingine hautafaa? Au inamaanisha kwamba yeye anafikiri kwamba kutia mishipani kunatoa uelekeo zaidi wa kufanikiwa kuliko utibabu mwingine? Kuhusiana na hili, baraza moja la mahakimu katika United States ya Amerika liliandika hivi katika “Miongozo kwa Hakimu Katika Maagizo ya Kitiba Yanayoathiri Watoto”:

“Ikiwa kuna uchaguzi wa taratibu za kufuatwa—ikiwa, mathalani, daktari anapendekeza utaratibu fulani ulio na uelekeo wa asilimia 80 ya mafanikio lakini ambao wazazi wanakataa kukubalia, na wazazi hao hawakatai utaratibu fulani ulio na uelekeo wa asilimia 40 tu ya mafanikio—ni lazima daktari afuate mwendo ulio hatari zaidi kitiba lakini usiokatalika kwa wazazi.”41

98. Ni jambo gani la uhakika juu ya aina ya maarifa ya kitiba hukanusha zaidi kutia kinguvu damu mishipani?

98 Pia mahakimu hawa walisema kwamba “maarifa ya kitiba hayajasonga mbele vya kutosha kuwezesha tabibu kutabiri kwa uhakika wa kiasi kwamba mgonjwa wake ataishi au atakufa au atapatwa na dhara au umbuko la daima mwilini.” Je! hamna ukweli mwingi katika hilo? Je! wenye mamlaka ya kitiba hawakazii kwamba jambo tu wanaloweza ni kusema lile linaloonekana kuwa laelekea kutukia? Kulingana na hilo, matabibu na wapasuaji wengi wastahiwa wameshirikiana na Mashahidi wa Yehova, wakiandalia vijana kwa wazee utibabu mzuri, huku wakistahi masadikisho yao yanayotegemea msingi wa Biblia kuhusu damu.

Kutibu Yule “Mwanadamu Mzima-mzima”

99. Ile kanuni ya kutibu mtu mzima ina uhusiano gani na utiwaji kinguvu wa damu mishipani?

99 Watu walio katika uwanja wa kitiba wanathamini zaidi na zaidi kwamba ni jambo la maana kushughulika na mgonjwa akiwa “mwanadamu mzima-mzima.” Kinachohitaji utibabu si kikoromeo tu wala ini, bali ni mtu mzima-mzima, binadamu mwenye hisia na itikadi ambazo kwa kweli huenda zikavuta namna ya kuitikia kwake utibabu. Katika tahariri moja ya Texas Medicine, Dakt. Grant F. Begley aliandika kwamba “mimi ninapotibu ugonjwa fulani unaoathiri mwili, akili, na roho ya mtu aliye katika utunzaji wangu, ni kile anachoitikadi yeye ndicho cha maana. Itikadi zake, si zangu, ndizo zinazosababisha yeye ahisi woga, shaka, na hatia. Ikiwa mgonjwa wangu haitikadi kutiwa damu mishipani, jambo lililo la maana si vile mimi ninavyokufikiria.”42

100, 101. Ni nini linaloweza kusemwa juu ya kuponya mwili huku roho ya mtu ikivunjwa?

100 Kutibu yule “mwanadamu mzima-mzima” ni jambo la kujali ubinadamu na ni lenye mafaa pia kwa sababu ya matokeo yenye msiba yanayotokana na kufanya vinginevyo. “Tabibu mwenye ufahamu,” akachagiza Dakt. Melvin A. Casberg katika The Journal of the American Medical Association, “lazima awe na habari juu ya nyuso hizi zilizotengana, lakini zinazohusiana, za mwili, akili, na roho, na athamini kwamba kuponya mwili usoni mwa akili au roho iliyovunjika ni ushindi wa upande, au hata ni ushinde kamili.”43

101 Kwa njia hiyo daktari anafuata mwendo wa hekima na anatibu yule “mwanadamu mzima-mzima” anapoonyesha staha kwa ajili ya masadikisho ya kidini ya mgonjwa kwa habari ya tumizi la damu.

Je! Msimamo Wao Si wa Kiakili Kitiba?

102-104. Ni mambo gani ya hakika yanayokanusha kwamba msimamo wa Mashahidi kuhusu kutiwa damu mishipani si jambo lisilo la kiakili?

102 Hata ingawa katao la msingi la Mashahidi wa Yehova kuhusu kutiwa damu mishipani lina sababu za kidini, watu wengi wanaona msimamo huu kuwa usio wa kiakili kitiba. Lakini je! ndivyo? Kwa kuwa msimamo wa Mashahidi juu ya damu unahusiana na suala la kitiba, kuna manufaa katika kuchunguza kifupi vidokezi vya kitiba juu ya kukataa damu.

103 Katika United States, Japani na Ufaransa pekee, yuniti (vipimo) zipatazo milioni 15 za damu (cc. 500 kila moja) zinatiwa katika mishipa ya watu kila mwaka. Inafaa kuuliza hivi: Je! damu yote hii inapewa kwa watu kwa sababu inahitajiwa ili kuokoa uhai?

104 Mkataa uliofikiriwa kukatwa na madaktari 800 wa Ulaya waliokutana katika Paris ni kwamba “mara nyingi mno damu inaonwa kuwa ‘dawa muujiza’ anayopewa mgonjwa, kwamba anaihitaji au la.” Madaktari hawa walikataa kukubalia hasa utiwaji wa yuniti moja-moja, ambao walisema “haufai kitu katika visa 99 kati ya 100.”44 Uchunguzi mmoja katika United States ulidokeza kwamba asilimia 72 ya visa vya damu iliyotiwa mishipani mahali fulani-fulani ‘haihitajiwi kabisa au ni ya kutilika mashaka.’45

105, 106. Kwa nini madaktari fulani wanashindwa kuona utiwaji damu mishipani kwa njia ya kupinga, na kwa sababu gani mahakimu fulani wamependekeza utibabu tofauti?

105 Dakt. Rune Eliasson wa Stockholm, Sweden, alithubutu kutoa maoni ya “kwamba matabibu wengi, labda kwa kuongozwa vibaya na hilo neno kwenye akili, wamejiruhusu wapofushwe kwa urahisi na utukufu mwingi ambao wao wenyewe wamezungushia utiaji damu mishipani, hivi kwamba faida na hasara za utibabu wa namna hii haziwezi kuonwa kulingana na zinavyofaa kuonwa.”46

106 Kwamba wewe unaafiki au huafiki sababu za kidini zinazofanya Mashahidi wa Yehova wasikubali kutiwa damu, “faida na hasara za utibabu wa namna hii” zinastahili kufikiriwa. Ndivyo ilivyo hasa kwa kuwa mahakimu fulani wanaozungumzia utiaji wa damu mishipani wamependekeza kwamba matakwa ya mgonjwa kuhusu utibabu wa namna nyingine yanapasa kufuatwa ikiwa kuna hatari fulani ya wazi kabisa kuhusiana na ule utibabu uliokubaliwa na wote.

Damu—kitu Tata Kisicho na Kifani

107, 108. Ni jambo gani la uhakika juu ya damu linaloathiri sana ubora wa thamani ya kutia damu mishipani?

107 Ijapokuwa huenda watu fulani wakafanya haraka kuita katao la damu kuwa ni “la ujiuaji,” mfikio wa kiasi kwenye jambo hili wataka kukiri uhakika kwamba kuna mambo fulani yasiyojulikana kwa uhakika, na hata hatari zinazohusiana na kutiwa damu mishipani.

108 Madaktari wanajua kwamba damu ni kitu tata sana sana. Hiyo inadhihirishwa hata katika lile jambo linalohusu aina za damu. Vitabu vya marejezo vinataarifu kwamba mifumo ya vikundi vya damu vinavyojulikana ni kama kumi na mitano mpaka kumi na tisa hivi. Kwa habari ya kimoja cha hivi, ule mfumo wa kikundi cha damu ya Rh, kitabu kimoja cha hivi majuzi juu ya damu kilisema kwamba “kwa wakati uliopo namna tofauti karibu mia tatu za Rh huenda zikatambuliwa kinadharia.”47

109-111. Ni tabia gani za damu zilizo na uhusiano na kihatarishi katika kutia damu mishipani?

109 Uso mwingine wa utata na kutokuwa na kifani kwa damu ya kila mtu ni ule unamna-namna wa viua-bakteria ndani yayo. Kwenye mkutano mmoja wa wanasayansi katika Zurich, Switzerland, kikundi cha wataalamu Waingereza wa kuchunguza vitendo vya uhalifu kilionyesha wazi kwamba viua-bakteria katika damu ni vya namna nyingi sana mbalimbali hivi kwamba huenda damu ya kila mtu ikasemwa kuwa ya namna mahususi na isiyo na kifani. Wanasayansi wanatumainia kuweza “kujenga upya kutokana na doa la damu mfano wa utu wa kila mtu anayeacha nyuma alama ya damu.”48

110 Uhakika wa kwamba damu ni tishu tata sana sana inayotofautiana kutoka mtu na mtu una athari ya maana sana juu ya kutia damu mishipani. Hili ni jambo alilosema hivi majuzi Dakt. Herbert Silver, kutoka Benki ya Damu na Sehemu ya Imyunohematolojia ya Hospitali ya Hartford (Konektikati). Yeye aliandika kwamba, kwa kufikiria vile visababisho-damu vinavyoweza kufanyiwa michunguzo, “uelekeo uliopo wa kumpa mtu damu inayolingana kabisa na yake mwenyewe ni chini ya 1 katika visa 100,000.”49

111 Basi, kwamba wana makatao ya kidini kuhusu kutiwa damu mishipani, huenda watu wengi wasitake damu kwa dhati kwa sababu tu ni kiungo-kipandikizwa ambacho, sana sana chafaana kidogo tu na damu yake mwenyewe.

Kutia Damu Mishipani—hatari Halisi Ni ya Kadiri Gani?

112-114. Kuna ushuhuda gani wa kuonyesha kwamba kutia damu mishipani kunazo hatari ndani?

112 Madaktari wanajua kwamba kuhusiana na kitayarishwa cho chote cha kitiba kuna hatari ya kipimo fulani, hata kuhusiana na dawa za kawaida sana kama aspirini na penisilini. Kulingana na hilo, huenda hata ikatazamiwa kwamba utibabu wa kutumia kitu tata kama damu ya kibinadamu kunahusisha ndani hatari fulani. Lakini ni hatari ya kadiri gani? Na hili laelekea kuleta athari gani juu ya maoni ya tabibu kuhusu msimamo unaochukuliwa na Mashahidi wa Yehova?

113 Mkadirio wa kikweli wa mambo ya uhakika unathibitisha kwamba ni lazima kutia damu mishipani kuonwe kwa haki kuwa utaratibu unaohusisha ndani hatari kubwa na hata unaweza kuleta kifo.50

114 Dakt. C. Ropartz, Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Kutia Damu Mishipani Katika Rouen, Ufaransa, alieleza kwamba “chupa moja ya damu ni kombora.” Kwa kuwa huenda yale matokeo hatari yasionekane mpaka wakati fulani unapokuwa umepita, yeye aliongezea, “zaidi ya hilo, huenda hilo likawa pia ni kombora-wakati kwa mgonjwa.”51 Kichapo kimoja cha Serikali ya United States kilikuwa na makala moja juu ya hatari za damu na kikasema kwamba

“ . . . kuchanga damu kunaweza kulinganishwa na kumpelekea mtu asiyeshuku neno, au asiye tayari, bunduki iliyojazwa risasi. . . . Kama vile bunduki iliyojazwa risasi kuna wenzo au kibonyezo salama kinachodhibiti utiwaji damu mishipani. Lakini, ni watu wangapi wamekufa kutokana na majeraha ya risasi za bunduki likiwa ni tokeo la kuitikadi huo wenzo ulikuwa umekaa ‘salama’?”52

Je! madaktari wenye maarifa wanaweza kupuuza hatari zilizotaarifiwa kwa kusema zimetiwa chumvi?

115-117. Kwa nini madaktari wenye maarifa hawawezi kupuuza hatari za kutiwa damu mishipani kwa kusema zimetiwa chumvi?

115 Hasha, kwa maana mara nyingi matabibu huonyeshwa waziwazi uhalisi wa hatari zenyewe. “Hakuna zao la kibayolojia,” akaandika Winfield S. Miller katika Medical Economics, “lililo na uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na makosa yenye kufisha katika zoezi la tiba kuliko damu. Zaidi ya daktari mmoja amejifunza kwa huzuni yake kwamba kila chupa ya damu katika benki za damu inaweza kuwa ni chupa ya naitrogliserini.”53

116 Huenda mgonjwa au jamaa yake wasing’amue hatari zile mpaka inapokuwa kuchelewa mno. Dakt. J. Garrott Allen wa Chuo Kikuu cha Stanford, aliye stadi mashuhuri kuhusiana na tatizo la damu, alikadiria kwamba kutia damu mishipani kunaua angalau Waamerika 3,500 kila mwaka, na kuumiza wengine 50,000.54 Lakini kuna sababu imara kuitikadi kwamba kwa kweli huo ni mkadirio uliopunguzwa. Mathalani, hivi majuzi Southern Medical Journal lilidokeza kwamba labda ule mkadirio wa kwamba “kati ya vifo 3,000 na 30,000 vinavyohusiana na kutiwa damu mishipani” ni mkadirio wa kiasi.55 Tena zingatia akilini kwamba hizi ni tarakimu za nchi moja tu, bila kusema zile za sehemu nyinginezo za ulimwengu.

117 Kwenye mkutano mmoja wa Koleji ya Kiamerika ya Wapasuaji, Dakt. Robert J. Baker aliripoti kwamba ‘hatari ya matokeo mabaya ya damu ni kubwa kuliko ilivyotangulia kuitikadiwa kukiwa na mgonjwa mmoja kati ya wagonjwa 20 wanaositawisha mwitikiano.’ Ni watu wangapi wanaong’amua jambo hili? Akionyesha ni kwa nini ripoti hiyo inapasa kutuhangaisha sisi sote, Dakt. Charles E. Huggins, mkurugenzi mshirika wa benki moja kubwa ya damu, aliongezea hivi: “Ripoti hiyo ni ya kuogopesha lakini iliyo halisi kwa sababu matatizo hayo hayo yanakabili kila shirika [katika sehemu zote za] ulimwengu.”56

118. Je! kuna uwezekano wa ondoleo la matatizo ya kutiwa damu mishipani? Ikiwa hakuna, kwa nini?

118 Je! kuna tumaini la ondoleo? Watu wengi, labda hata baadhi ya walio katika kazi ya kitiba, huenda wakahisi kwamba sayansi imekuwa ikifanya maendeleo halisi ya kushinda hatari za kutia damu mishipani. Lakini, kama ilivyotaarifiwa katika toleo moja la majuzi la jarida Surgery, “matatizo makubwa mapya yanayohusiana na kutia damu mishipani kwa wingi yamedokezwa, matatizo ambayo hivi majuzi tu miaka mitano iliyopita hayakufikiriwa sana au hayakufikiriwa hata kidogo, hata hivyo yanaweza kuwa ni makubwa zaidi ya takribani matatizo yote yaliyosumbua-sumbua ufahamu wa wanabenki wa damu, wanakliniki, na wachunguzi kwa muda wa ile miaka 40 ya kwanza ya kuhifadhi damu katika benki ya kikliniki.”57

Ni Nini Zile Hatari?

119, 120. Ni aina gani mbalimbali za hatari zinazoshirikishwa na kutiwa damu mishipani?

119 Bila kukazia mno uhakika wa kwamba hatari zipo, tunaweza kuchunguza kifupi tuone ni zipi zilizo baadhi yazo. Ingawa madaktari wengi wanajua habari zinazofuata, huenda ikasaidia watu wengine kuthamini kwamba, ingawa msimamo unaochukuliwa na Mashahidi wa Yehova ni kwa ajili ya sababu za kidini, huo una ustahili wa kitiba.

120 Kitabu cha mafundisho Hematology kina jedwali hii:58

Namna za Miitikiano ya Kutiwa Damu Mishipani

Febrile

Leukocyte antibodies

Platelet antibodies

Pyrogens

Allergic

Hemolytic

(incompatible transfusion)

Transmission of disease

Serum hepatitis

Malaria

Syphilis

Cytomegalovirus infection

Gross bacterial contamination

Cardiac overload

Citrate intoxication

Potassium intoxication

Abnormal bleeding

Incompatible transfusion

Massive transfusion

Isosensitization

Transfusion hemosiderosis

Miscellaneous

Thrombophlebitis

Air embolism

Injection of foreign material

121, 122. Ni baadhi gani za miitikiano yenye kudhuru ya mara hiyo ya kutiwa damu mishipani?

121 Namna hizi nyingi za miitikiano ya kutiwa damu mishipani ni zenye hatari kweli kweli, kwa maana zinaweza kusababisha kifo. Acheni tufikirie baadhi yazo.

122 Jedwali hiyo inaonyesha kwanza baadhi ya miitikiano ya “mara hiyo hiyo.” Mwitikiano febrile au kufanyiza homa aghalabu unaweza kutibiwa kwa mafanikio. Hata hivyo, kama anavyoripoti Profesa wa Dawa, James W. Linman, “miitikiano mikali yenye kufanyizwa na homa hutukia na huenda ikawa na mkazo vya kutosha hata kuwa yenye kutisha uhai katika wagonjwa fulani walio mahututi sana.”58 Damu isiyolandana na ile nyingine inaleta mwitikiano hemolytic, ukihusisha ndani kuharibiwa haraka sana kwa chembe nyekundu za damu, kunakoweza kutokeza ushinde wa figo, mshtuko na kifo. Miitikiano hemolytic ni yenye hatari hususa kwa wagonjwa waliopewa nusukaputi, kwa maana huenda dalili zisionekane mpaka inapokuwa ni kuchelewa mno.59

123-125. Ni kwa kadiri gani hatari ya kupitisha ugonjwa inashirikishwa na kutiwa damu mishipani?

123 “Transmission of disease” (Mpisho wa ugonjwa) umeorodheshwa pia miongoni mwa miitikiano inayoweza kutokea. Je! kuna hatari yo yote kubwa kutoka upande huu?

124 Hepataitisi B (seramu hepataitisi—mchochota wa ini kutokana na damu iliyoambukizwa) ni mtatanisho hatari hasa wa kutiwa damu mishipani. Damu ya mchangaji, bila ya kutuhumiwa, huenda ikawa na ile virasi ya hepataitisi inayoweza kudhuru afya ya mtu mwenye kupokea damu, au hata kumuua. Kadiri mtu anavyozidi kutiwa damu mishipani, ndivyo uelekeo wake wa kupata seramu hepataitisi unavyozidi kuwa mkubwa. Hata hivyo si damu nyingi sana inayohitajiwa. Punde kuliko tone moja inatosha; wewe unaweza kupata ugonjwa huo kutokana na asilimilioni moja ndogo ya mililita ya damu iliyoambukizwa.60

125 Ni kwa kadiri gani inaelekea kwamba huenda wewe ukapata hepataitisi kutokana na kutiwa damu mishipani? Kwa kadiri fulani hiyo inategemea unakoishi, kwa maana hepataitisi inayotokea baada ya kutiwa damu mishipani inatukia kwa ukawaida zaidi katika bara ambazo baadhi ya damu inatokana na “wachangaji” wanaolipwa, watu wanaouza damu yao.

126, 127. Ni jambo gani linaloweza kusemwa juu ya ugonjwa wa seramu hepataitisi?

126 Kadirio linaloonekana mara nyingi katika majarida ya kitiba ni kwamba asilimia moja, au mtu mmoja kati ya watu mia moja, hupata hepataitisi baada ya kutiwa damu mishipani.61 Hata hivyo, ithibati inaonyesha kwamba mtukio ulio wa kweli huenda ukawa wa juu zaidi sana. Ndivyo ilivyo kwa sababu hepataitisi B ina kipindi cha kutamia cha hadi miezi sita, hivi kwamba ugonjwa huo huenda usionekane mpaka upite muda baada ya kutiwa damu mishipani. Madakt. John B. Alsever na Peter Van Schoonhoven waliandika hivi katika Arizona Medicine:

“Kwa muda wa miaka kumi mpaka kumi na mitano iliyopita, mtukio wao katika vituo vya damu katika jumuiya umekuwa kama asilimia 1 katika uchunguzi wa kutazama nyuma ulioripotiwa wa ugonjwa wenye kuthibitiwa kikliniki. Hata hivyo, mtu anapowachunguza katika maabara kwa matazamio mema wagonjwa waliotiwa damu mishipani kwa vipindi vya majuma 2 mpaka 4, anakuta kufikia mara kumi za mtukio mkubwa zaidi wa ambukizo.”62

127 Tazama jambo hili kutokea upande mwingine. Imesemwa mara nyingi kwamba katika United States kuna visa 30,000 kila mwaka vya hepataitisi inayotokea baada ya kutiwa damu mishipani, kukiwa na vifo 1,500 hadi 3,000.63 Ikiwa ndivyo hali ingekuwa, ingekuwa nzito vya kutosha. Hata hivyo, habari zilizoandaliwa na Kitovu cha Kudhibiti Magonjwa cha serikali zinaonyesha tarakimu ya kiasi ya hepataitisi B kuwa ni 200,000 au zaidi kila mwaka.64 Na ni nani anayeweza hata kukadiria hesabu yenye jumla ya visa vya hepataitisi inayohusiana na kutiwa damu mishipani kwa nchi zote za Amerika ya Kaskazini na Kusini, Ulaya, Afrika na Esia?

128. Kwa nini uwezekano wa Shahidi kupata seramu hepataitisi ni zaidi ya hatari inayoweza kutetewa?

128 Bila shaka, watu fulani wanauona uwezekano wa kupata hepataitisi kutokana na kutiwa damu mishipani kuwa hatari inayoweza kutetewa. Huenda daktari akasababu kwamba, “Afadhali mgonjwa wangu awe hai akiwa na hepataitisi, ambayo mimi naweza kutibu, kuliko yeye kuwa mfu kwa sababu ya kutotiwa damu mishipani.” Lakini kusababu hivyo si msingi halali wa kuyaona makatao kidhamiri ya mgonjwa juu ya kutiwa damu mishipani kuwa ni ‘ya ujiuaji’ na yasiyostahiki kufikiriwa.

Je! mgonjwa anaweza kuhakikishiwa vya kufaa kwamba yeye ataendelea kuwa hai akipatwa na hepataitisi inayotokea baada ya kutiwa damu mishipani?

129, 130. Ni mambo gani ya uhakika yanayokanusha mgonjwa kuhakikishiwa vya kufaa kwamba ataokoka shambulio la seramu hepataitisi?

129 Uhakika wenye kutia makini ni kwamba wenye mamlaka wanakiri kwamba yapata asilimia 10 hadi 12 ya wale wanaopata seramu hepataitisi kutokana na kutiwa damu mishipani hufa likiwa tokeo.65 Kwa watu wenye umri wa miaka zaidi ya 40, wastani wa kifo ni asilimia 20—mmoja kati ya watano.66 Katika wagonjwa wenye umri wa zaidi ya miaka 60, wapatao nusu hufa kwa sababu ya hepataitisi.67

130 Zaidi ya hilo, hakuna njia hakika ya kukomesha ile hatari kubwa ya kuweza kupata hepataitisi kutokana na kutiwa damu mishipani. The Journal of Legal Medicine lilikiri kwamba “hakuna zo zote za njia zinazojulikana sasa za kuhifadhia damu zilizo na vitu vyo vyote vya kukinza virasi zilizomo damuni. Dawa yo yote yenye nguvu za kuharibu au hata kupunguza virasi ya hepataitisi itaharibu pia damu yenyewe au sehemu fulani ya damu hiyo.”68

131, 132. Ni kwa kadiri gani mbinu za ki-siku-hizi zimeondolea mbali hatari za kupata seramu hepataitisi kutokana na kutiwa damu mishipani?

131 Namna gani juu ya maendeleo katika mbinu za kuchunguza ili kutambua na hivyo kuondolea mbali damu chafu? Dakt. M. Shapiro, wa Utumishi wa Kutia Damu Mishipani Afrika Kusini, alionyesha wazi hivi majuzi kwamba “hata pamoja na michunguzo yenye unyeti zaidi sana, labda ni kisa 1 tu kati ya 8 au vichache zaidi vya hepataitisi inayotokea baada ya kutiwa damu mishipani kinachoweza kuepukwa kwa kupimwa pekee kwa damu za wachangaji katika maabara.”69

132 Basi, hata ikiwa seramu hepataitisi ingekuwa ndiyo hatari pekee ya ugonjwa unaotokea baada ya kutiwa damu mishipani, kungekuwa na sababu ya kitiba inayotosha kumfanya mtu awe na mashaka juu ya kukubali damu. Ingawa hivyo, uhakika ni kwamba hepataitisi ni mojapo tu ya hizo hatari. Angalia hizi nyingine:

133. Ni tatizo gani la pande mbili linalotokezwa na damu iliyoambukizwa kaswende?

133 “Damu inapasa kuonwa kuwa dawa hatari, na inapasa kutumiwa kwa hadhari ile ile kama inayotumiwa, mathalani, kuhusiana na mofini.”70 Hivyo, Profesa H. Busch, mkurugenzi wa dawa ya kutiwa mishipani, alimalizia ripoti moja aliyopelekea mkusanyiko wa wapasuaji wa Ujeremani ya Kaskazini. Alitaja ndani yayo tatizo la pande mbili linalohusu kutiwa damu mishipani. Yeye alisema kwamba ili damu iliyochangwa ibaki ikiwa na ubora wa kiuhai ulio wa juu zaidi, inapasa kutiwa mishipani katika muda wa saa 24; baada ya hapo hatari zinazohusu utaratibu wa kugeuza chakula mwilini zinaongezeka kwa sababu ya mabadiliko katika damu iliyowekwa akibani. Kwa upande ule mwingine, lazima damu iwekwe akibani kwa angalau saa 72 au sivyo huenda ikapisha kaswende. Na hata michunguzo ya kutambua damu yenye kaswende si kinga salama, kwa maana haigundui kaswende katika hatua zao za mapema-mapema. Hakuna uhitaji wa kueleza hapa madhara yanayoweza kupata mtu mwenye kupokea damu iliyoambukizwa kaswende, na pia umizo kwa jamaa yake.

134, 135. Ni maambukizo gani mengine ambayo yamkini kupitishwa kwa kutiwa damu mishipani?

134 Ripoti hiyo ya Kijeremani ilikazia pia hatari ya visa vya kutia damu mishipani vinavyoeneza maambukizo ya saitomegalovirasi (virasi zinazosababisha mkuzo au ongezeko la damu) na maleria. Saitomegalovirasi hujulikana kuwa hatari hasa kwa watoto. Basi, kukiwa na sababu nzuri, madaktari Wajeremani walionywa juu ya “matokeo mazito sana, hata yenye kufisha” yanayoweza kutokana na kutiwa damu mishipani. Na Shirika la Tiba Amerika lilishauri kwamba “kwa sababu ya ongezeko la usafiri katika tufe lote na kurudi kwa wanajeshi kutoka maeneo yaliyo na magonjwa ya huko huko tu, kumekuwa na ongezeko la mtukio wa maleria kwa wanaotiwa damu mishipani.”71

135 Katika maeneo ya kitropiki kuna magonjwa kadhaa yanayoweza kupishwa kwa kutiwa damu mishipani, kama vile ugonjwa wa Chagas (ulio na wastani wa kuua mtu mmoja kati ya kila watu kumi), ugonjwa malale wa Kiafrika, buba na ugonjwa unaotokana na vifyonza-damu mwilini.72

136. Ni hatari gani nyingine inayoshirikishwa na kutiwa damu mishipani, na ni kubwa jinsi gani?

136 Hatari nyingine isiyoweza kupitiwa mbali ni mchafuo mkubwa wa damu unaofanywa na bakteria. Namna fulani za bakteria zinaweza kuzidishwa hata katika damu iliyobaridishwa, hiyo ikitokeza tisho hata kwa mtu ye yote mwenye kupokea damu hiyo baadaye. Ingawa ni wagonjwa wachache zaidi wanaopatwa na utatanishi huu kuliko wale wanaopatwa na seramu hepataitisi, matokeo ni yenye msiba kwa wale wanaopatwa nao. Wastani wa kifo ni kati ya asilimia 50 na 75.73

137. Kwa sababu ya hatari zinazoshirikishwa na kutiwa damu mishipani, hospitali fulani zinawataka wagonjwa wafanye nini?

137 Wakati ujao una nini kwa habari ya hatari zinazoshirikishwa na kutiwa damu mishipani? “Orodha ya magonjwa ya kupishwa,” aripoti Dakt. John A. Collins wa Shule ya Dawa Katika Chuo Kikuu cha Washington, “itatofautiana na kwa uhakika itaongezeka, na huenda wasiwasi mwingi ukawako wakati virasi nyingi zaidi zinazohusiana na uvimbe hatari mwilini zinapotambuliwa katika damu ya kibinadamu.”74 Kulingana na hilo, sasa hospitali nyingi zinataka mgonjwa atie sahihi katika taarifa rasmi au mwafaka wa kwamba yeye hataweka daktari au hospitali chini ya dhima ya jeraha linalotokana na kutiwa damu mishipani.75

138. Ni sababu gani ya msingi inayofanya Mashahidi wasikubali kutiwa damu mishipani?

138 Je! mfikirio huu mfupi wa baadhi ya hatari za tiba ya kutumia damu unamaanisha kwamba Mashahidi wa Yehova wanakataa kutiwa damu mishipani kwa sababu za kitiba hasa? La, hivyo sivyo ilivyo. Sababu ya msingi inayofanya wao wasikubali kutiwa damu mishipani ni mambo ambayo Biblia inasema. Kimsingi katao lao ni la kidini, si la kitiba. Hata hivyo, uhakika wa kwamba kuna hatari nzito-nzito za kutwaa damu unakazia tu kufaa kwa msimamo ambao Mashahidi wa Yehova wanachukua, hata inapotazamwa kutokea upande wa kitiba.

Njia Nyinginezo za Kutibu

139-141. Katika upasuaji wa hiari, kuna njia gani nyinginezo zinazoweza kutumiwa badala ya damu?

139 Ikiwa mwendo unaofuatwa na Mashahidi wa Yehova ungekuwa wa ushupavu na wenye kuleta madhara kwao wenyewe na labda kwa wengine, kungekuwa na sababu ya kuhangaikia. Kuhusiana na hili labda yafaa kuulizwa hivi:

Je! maoni haya ya kidini yanayofuatwa na Mashahidi wa Yehova ni yasiyofaana sana na viwango vya jamii ya kibinadamu na maarifa ya kitiba hivi kwamba hayawezi kukubaliwa kwa kadiri inayofaa?

140 Jibu hakika ni kwamba katao lao la damu lenye msingi wa Biblia linaweza kukubaliwa katika visa vilivyo vingi kwa kutumia njia nyinginezo za kutibu.

141 Kama inavyojulikana vizuri, katika visa vya upasuaji wa hiari, huenda madaktari ‘wakaongeza damu ya mgonjwa’ kabla na baadaye, kama vile kwa kutumia asidi amino na michanganyiko ya chuma76c ya mdomoni au ya kuminywa mwilini; hiyo inaweza kupunguza uhitaji wo wote wa kutiwa damu mishipani. Kupunguza sana joto la mwili wa mgonjwa kumethibitika kuwa jambo la faida katika kupunguza upotevu wa damu wakati wa upasuaji, hata kwa vitoto vichanga.78 Vivyo hivyo, kupunguza mvutano wa damu kunaweza kuzuia damu isitoke kwa wingi sana katika mishipa midogo wakati wa upasuaji. Na labda jambo ambalo limethibitika kuwa la mafanikio makubwa zaidi ni kuziba kwa uangalifu sana hata mishipa midogo sana sana inayokatwa. Katika American Journal of Obstetrics and Gynecology, daktari mmoja ambaye amepasua wengi wa Mashahidi wa Yehova alisema:

“Hakuna shaka kwamba hali ambapo wewe unafanya upasuaji bila uwezekano wa kutia damu mishipani inaelekea kuleta maendeleo katika upasuaji wako. Wewe unakazana zaidi kidogo ili kubana kila mshipa wenye kutoka damu.”79

Ikiwa mgonjwa amepoteza damu nyingi sana wakati wa upasuaji au kupitia aksidenti, je! maoni ya kwamba hakuna njia nyingine isipokuwa kutumia damu ni ya kiakili?

142, 143. Ni upi ulio uhitaji mkubwa hasa wakati damu nyingi sana imepotezwa?

142 Mambo fulani ya uhakika yaliyotokezwa na Profesa James W. Linman katika Hematology yanatumikia kuwa msingi mzuri wa kukadiria ubora wa jibu:

“Damu si dawa ya kuongeza nguvu mwilini wala si kichocheo; haitasaidia jeraha lipone wala haitakandamiza ambukizo; na ni mara chache, iwavyo, ambapo uwezo wayo wa kupeleka oksijeni unapokuwa sababu yenye kuweka hadi katika upasuaji. Kutia damu mishipani kunatumikia tu kuongezea jumla ya kiasi cha damu, kuinua juu uwezo wa damu wenye kupeleka oksijeni, na kuwa chanzo cha vile visehemu vya kawaida vinavyofanyiza umajimaji wa damu.” (Italiki zimeongezwa.)80

143 Fikiria kwanza lile jambo la ‘kuongezea jumla ya kiasi cha damu.’ Mara nyingi sana mtu anapopoteza damu nyingi sana, kinachohitajiwa kwa msingi ili kuzuia mshtuko na kifo ni kuweka kiasi kingine cha umajimaji mahali pa kile kilichopotea. Kwenye kongresi moja ya Shirika la Kitiba la Afrika Kusini, mtaalamu wa kutia damu mishipani alieleza kwamba huenda mtu akapoteza kufikia lita 1.5 za damu na bado awe ana zaidi ya asilimia 60 ya chembe nyekundu zake,81 kiasi ambacho kinatosha ili kulisha tishu. Lakini mtu anahitaji umajimaji mwingi zaidi katika mishipa yake ili kusaidia chembe nyekundu za damu ziendelee kuzunguka.

144. Ni upi ulio umajimaji wa kuchagua wakati damu nyingi sana imepotezwa?

144 Jarida Anaesthesia la Uingereza liliripoti kwamba viyeyuko visivyo na damu vinafanya hivyo kwa matokeo mazuri kuliko damu inayotiwa mishipani, kwa maana havipunguzi utendaji wa moyo, jambo ambalo ni kitatanishi kinachotokea kwa ukawaida baada ya kutiwa damu mishipani. Makala hiyo ilisema kwamba katika pindi fulani fulani ambapo kwa wazi kiasi cha kutosha cha damu halisi kilishindwa kuzaa tokeo lililotamaniwa kuhusiana na jeraha, mara nyingi kutumia miyeyusho isiyo na damu kulizaa maendeleo ya kutazamisha. Kwa sababu hiyo, makala hiyo ilitoa maoni haya:

Hata ikiwa kuna kiasi cha kutosha cha damu halisi, hata hivyo ni jambo lenye mashaka kama huo ndio umajimaji unaofaa sana utibabu wa mwanzo kwa ajili ya utiwaji mishipani wa haraka sana wa wagonjwa ambao wamepoteza damu nyingi.”82

145, 146. Ni kwa kadiri gani mmoja anaweza kuongeza upotevu wa damu, na kwa nini viyeyuko vinavyotumiwa kuwa njia nyingine si vibadala vya damu?

145 Je! si jambo la kimantiki kwamba mtu wa kikawaida angeweza kupoteza kiasi kinacholingana na yuniti (cc. 500) au zaidi ya damu bila matokeo ya kifo? Watu wengi wamechanga yuniti moja ya damu halafu wakatoka hapo na kuendelea moja kwa moja na utendaji wao wa siku hiyo. Uchunguzi wa kikliniki wenye kudhibitiwa umeonyesha kwamba mtu mwenye ‘kiasi kikubwa cha damu huenda akavumilia upotevu wa kufikia lita mbili [cc. 2,000] za damu halisi’ bila uhitaji wa kitu cho chote, isipokuwa kutia miyeyusho isiyo damu mahali pa umajimaji uliopotea.83

146 Ingawa hivyo, namna gani juu ya ‘kuinua juu uwezo wa damu wenye kupeleka oksijeni’? Madaktari wanajua kwamba kwa kweli miyeyusho mingine si “vibadala vya damu.” Kwa nini sivyo? Kwa sababu ile hemoglobini ya chembe nyekundu hupeleka oksijeni katika sehemu zote za mwili. Miyeyusho isiyo na damu haina kitu hicho.

Kwa habari ya mgonjwa ambaye amepoteza damu nyingi sana, je! ni lazima damu halisi, au chembe nyekundu zilizotiwa katika pakiti, zitumiwe ili kueneza oksijeni kwenye mwili wake wote?

147, 148. Mambo ya hakika yameonyesha nini kuhusu kipimo kilicho salama cha damu au hemoglobini iliyomo kwa ajili ya upasuaji?

147 Hili ni oni linaloendelezwa mara nyingi, lakini je! linapatana na mambo ya uhakika?

148 Kwa kawaida mtu ana gramu zipatazo 14 au 15 za hemoglobini (rangi-protini yenye chuma iliyo ndani ya chembe nyekundu za damu) katika kila cc. 100 za damu. Kwa ujumla madaktari huchukua msimamo wa kwamba ‘chini ya hali ngumu-ngumu hemoglobini ya gramu 10.3 hadi 10.5 inahesabiwa kuwa thamani ya chini zaidi iliyo salama kwa upasuaji wa kawaida.’84 Lakini, kwa kweli, sehemu kubwa ya hemoglobini ya mtu huwa akibani ili itumiwe wakati wa mkakamuo mwingi; kwa sababu hiyo, mgonjwa asiyetoka kitandani anakuwa amestareheka vizuri akiwa na gramu chache kama 5 au 6.85 M. Keith Sykes, Profesa wa Dawa za Kupoteza Fahamu za Kliniki kwenye Chuo Kikuu cha London, alieleza hivi majuzi: “Ingawa vituo vingi vinachagua kiwango cha asilimia ya gramu 9 au 10 kuwa mstari wa kugawanya kati ya ukubali na katao la upasuaji wa hiari, ni lazima ikaziwe kwamba hakuna ithibati kamili kwamba viwango vya ubora vilivyo juu ya kitembo hicho ni ‘salama’ au kwamba viwango vya ubora vilivyo chini ya kitembo hicho vinaupa upasuaji hatari ya ziada. Kwa hiyo linaonekana kuwa si jambo la akili kuchagua tarakimu fulani isiyo na msingi kuwa kitembo kinachokubalika cha hemoglobini.”86 Hali kadhalika, Dakt. Jeffrey K. Raines, wa Hospitali Kuu ya Massachusetts, alitaarifu kwamba “sisi tunaweza kuacha kipimo cha damu kishuke chini ya vile tulivyokuwa tumefikiri. Tulikuwa tukifikiri ilikuwa lazima mgonjwa awe na hemoglobini ya 10, lakini sasa tunajua kwamba sivyo ilivyo hasa.”87 Dakt. Ricardo Vela wa idara ya dawa za kupoteza ufahamu katika Madrid, Hispania, alijionea hili kuhusiana na wagonjwa walio Mashahidi wa Yehova. Yeye aliandika kwamba vitembo vya chini sana vya hemoglobini ambavyo hapo kwanza vingalifikiriwa kuwa vyenye kukatazwa “vilivumiliwa ajabu na wagonjwa.”88

149, 150. Ni jambo gani ambalo limepata kujulikana kwa kujifunza habari ya kutia damu mishipani kuongezea mara hiyo uwezo wa damu kubeba oksijeni?

149 Kuna upande mwingine wa jambo hili ambao umekuwa haukuthaminiwa mahali pengi, hata katika uwanja wa kitiba.

Je! kutiwa damu mishipani kutaongezea mara hiyo ule uwezo wa damu wa kupeleka oksijeni?

150 Watu wengi wanaitikadi kwamba kutafanya hivyo, lakini tahariri moja ya hivi majuzi katika Anaesthesia ilisema jambo hili la maana: “Inastahiki kukumbukwa pia kwamba, hemoglobini ya chembe nyekundu zenye asidi zilizowekwa akibani haipatikani kikamili ili iweze kupeleka oksijeni kwenye tishu kwa muda wa saa 24 baada ya kutiwa damu mishipani . . . ; kwa hiyo utiaji damu mishipani haraka sasa lazima uonwe hasa kuwa kiongeza-kiasi tu cha umajimaji-damu katika zile hatua za kwanza.”89 Watafiti kwenye State University ya Ohio walipata kuona kwamba sababu ya jambo hili ni kwamba mabadiliko ya kikemikali hutukia katika damu iliyowekwa akibani. Uchunguzi wao ulionyesha kwamba damu iliyowekwa akibani kwa zaidi ya siku kumi “haileti maendeleo au huenda hata ikafanya upelekaji wa oksijeni uwe mbaya zaidi mara tu baada ya kutiwa mishipani.” Nao walipata kuona kwamba bado upelekaji wa oksijeni ulikuwa chini ya kadiri ile ya kawaida saa 24 baadaye.90

Ni nini baadhi ya umajimaji usio na damu unaotumiwa kuwa njia nyinginezo zinazotumiwa badala ya kutia damu mishipani? Je! zinatumiwa kwa matokeo mazuri? Faida za njia hizo ni nini?

151. Ni baadhi ya umajimaji gani ambao umetumiwa badala ya kutiwa damu mishipani?

151 Labda kitu kinachopatikana na kutumiwa kwa wingi zaidi katika ujazio wa dharura wa umajimaji-damu ni ile selaini solushoni (myeyusho-chumvi, wa asilimia 0.9). Ni rahisi kuutayarisha, si ghali, ni thabiti na unafaana kikemikali na damu ya kibinadamu.91 Lakteti ya Ringer (ya Hartmann) ni myeyusho zaidi unaotia mkondo wa umeme au wa kifuwele, ambao umetumiwa kwa mafanikio katika visa vya watu walioungua sana, na katika upasuaji ambapo wagonjwa wamepoteza kufikia asilimia 66 kiasi cha umajimaji wa damu yao.92

152. Ni vipi vingine viongeza-kiasi-cha umajimaji-damu ambavyo vimetumiwa kwa matokeo mazuri?

152 Njia nyingine ni kuweka mahali pa damu iliyopotea kwa kutumia koloidi dektirani. Huo ni myeyusho-sukari wa kliniki ambao umethibitika kuwa bora katika upasuaji na katika kutibu visa vya kuungua-moto na kushtuka pia.93 Nyakati nyingine umeunganishwa na myeyusho-chumvi wenye asidi ya kusawazisha nguvu, ili kupata kutokana na kila kimoja mafaa yaliyo bora zaidi. Myeyusho wa Hemaselu haidroksethili starchi umetumiwa pia kwa matokeo mazuri katika hali mbalimbali za upasuaji ukiwa viongeza-kiasi cha umajimaji-damu.94d

153. Ni jambo gani linaloweza kusemwa juu ya matumizi ya viongeza-umajimaji-damu mbalimbali katika hatua hatari ya upungufu wa damu?

153 Kila mmoja wa umajimaji huu una mafaa na ustahili wao pekee. Lakini kwa habari ya hali za msiba, Anaesthesia ilieleza hivi:

“Kwanza katika hatua hatari umajimaji hasa unaochaguliwa si wa maana sana, maadamu si wenye kudhuru. Baadaye, kiasi cha mzunguko kikiisha kutanuka, ni lazima matakwa mahususi yafikiriwe kwa habari ya kisa fulani hususa.”95

154, 155. Ni uthibati gani inaoyonyesha kwamba damu si njia pekee yenye matokeo badala ya damu iliyopotea?

154 Je! hii inamaanisha kwamba umajimaji huu ni wa dharura tu? Sivyo kabisa. Kwa habari ya “namna zote kubwa-kubwa za upasuaji,” wapasuaji kwenye Koleji ya Dawa ya Chuo Kikuu cha Kentucky waliandika hivi:

“Wagonjwa mia moja walipoteza kila mmoja zaidi ya mililita 1,000 za damu walipokuwa wakipasuliwa, na walipokea mara mbili hadi mara tatu kiasi hicho cha myeyusho wa Hartmann. Wastani wa vifo na magonjwa ya baada ya upasuaji haukuathiriwa na ukosefu wa damu katika utaratibu-badala wa ulishaji. . . . Ijapokuwa lile pokeo linalozidi kwamba damu ndiyo kitu pekee chenye matokeo badala ya damu inayopotea, zoea la kutumia miyeyusho-chumvi kuwa badala ya sehemu au yote ya damu limeimarika katika vituo vingi.”96

155 Ingawa kwa sababu za kidini Mashahidi wa Yehova hawatakubali damu, wao hawana makatao yo yote juu ya kutumia viongeza-kiasi cha umajimaji-damu visivyo na damu. Basi, kwa upande wa daktari, mazao haya yana faida ya kuwa yenye kutumika kuhusiana na wagonjwa Mashahidi. Lakini kuna faida nyingine nyingi sana.

156, 157. Taja baadhi ya faida viongeza-kiasi-cha umajimaji-damu kuliko damu yenyewe.

156 “Vibadala vya damu visivyo na chembe za uhai,” akaandika Profesa E. A. Moffitt wa Kanada, “vinaweza kutengenezwa kwa wingi na kuwekwa akibani kwa vipindi virefu vya wakati. . . . Hasara za kutiwa damu mishipani ni faida za vibadala vya umajimaji-damu: mwepuko wa ambukizo la bakteria au virasi, miitikiano ya kutiwa damu mishipani na mnyetesho wa Rh.”97

157 Kuna manufaa nyingine inayostahiki kuangaliwa kutokana na utumizi wa viongeza-kiasi cha umajimaji-damu. Wakati damu ya kibinadamu inapowekwa akibani, lazima kemikali ziongezwe kuzuia mgandamano. Baadaye wakati damu hii inapopewa kwa mgonjwa, viongezo hivyo vinaweza kuingiliana na uwezo-asilia wa kugandamana; tokeo linaweza kuwa upotevu wa damu wenye kuendelea. Dakt. Melvin Platt mpasuaji wa moyo amevuta fikira kwenye uhakika wa kwamba tatizo hili linaepukwa wakati “dutu batili” kama vile myeyusho-chumvi wa Ringer unapotumiwa badala ya damu iliyowekwa akibani.98

Upasuaji Mkubwa Bila Damu

158. Ni mambo gani ya hakika yenye kupendeza ambayo ujuzi wa Dakt. Denton Cooley umefunua

158 Madaktari mashujaa ambao wameafiki kupasua Mashahidi wa Yehova bila kutumia damu mara nyingi wameliona tukio hilo likiwafunulia mambo mengi. Kielezi cha jambo hilo ni matukio ya juzijuzi katika upasuaji wa moyo. Wakati uliopita, aghalabu damu nyingi sana ilitumiwa. Lakini timu ya upasuaji ikiongozwa na Dakt. Denton Cooley kwenye Taasisi ya Moyo Katika Texas iliamua kujaribu kupasua Mashahidi wa Yehova. Kwa sababu madaktari hawangeweza kutayarisha pampu ya baina ya moyo na mapafu yenye kuhitajiwa ikiwa na damu au kutumia damu wakati wa upasuaji au baadaye, walitumia viongeza-kiasi cha umajimaji-damu visivyo na damu. Dakt. Cooley anaripoti: “Sisi tulivutiwa sana na matokeo juu ya Mashahidi wa Yehova hata tukaanza kutumia utaratibu huo juu ya wagonjwa wetu wote wa moyo. Tumepata mafanikio mazuri ajabu na tuliutumia katika mipandikizo yetu [ya moyo] pia.” Yeye aliongezea hivi: “Sisi tuna mkataba na Mashahidi wa Yehova wa kutotia mishipani chini ya hali zo zote. Wakati huo wangonjwa wanabeba jukumu la hatari, kwa sababu sisi hata hatuweki karibu damu kwa ajili yao.”99

159. Yamekuwa matokeo gani ya muda mrefu ya upasuaji wa moyo bila kutumia damu kwa watu wazima na watoto Mashahidi?

159 Yamekuwa matokeo gani ya ‘upasuaji wa kutotumia damu’ juu ya watu wazima na watoto? Dakt. Jerome H. Kay wa Kalifornia aliandika hivi: “Sasa sisi tumefanya mipasuo ya moyo takriban 6,000 kwenye Hospitali ya Mtakatifu Vincent katika Los Angeles. Kwa kuwa sisi tumekuwa hatutumii damu kwa ajili ya wagonjwa walio wengi, chapa-akili yetu ni kwamba wagonjwa wanafanya vizuri zaidi.”100 Uchunguzi wa Kikanada uliandaa habari muhtasi, ukifunua kwamba wakati umajimaji usio na damu, kama vile dektirani na myeyusho wa Ringer ulipotumiwa badala ya damu “hesabu ya vifo ilishuka kutoka asilimia 11 ikawa 3.8”101 Namna hii ya upasuaji imefanywa kwa mafanikio pia juu ya Mashahidi wa Yehova na watoto katika Norowei, Australia, Afrika Kusini, Ufaransa, Uingereza na Japani.

160, 161. Yamekuwa matokeo gani mahali ambako Mashahidi wamelazimika kuhitaji upasuaji bila kutumia damu na ambako kwa kawaida damu ni muhimu sana?

160 Hata hivyo, wapasuaji wenye ujuzi wana habari kwamba wagonjwa wa upasuaji wa ujumla husababisha kiasi kikubwa zaidi cha damu inayotumiwa kuliko wale wanaofanyiwa mipasuo mikubwa zaidi kama ule wa moyo. Ni nini limetukia kwa Mashahidi wa Yehova wenye kuhitaji mipasuo ya kikawaida zaidi ambako aghalabu kiasi kingi sana cha damu hutumiwa?

161 Chini ya kichwa “Upasuaji Mkubwa Katika Mashahidi wa Yehova,” kikundi cha madaktari wa New York kilisimulia visa kadhaa vinavyohusisha ndani upasuaji mkubwa sana, kama vile kuondoa kabisa viungo vyenye kansa, na wakaeleza kwamba kwa kutumia mbinu stadi halisi za upasuaji taratibu hizo zinaweza kufanywa bila damu.102 Taratibu nyingine zilizofanywa kwa mafanikio bila kutumia damu zinatia ndani mipasuo ya kuondoa kabisa mizizi ya ugonjwa katika kichwa na shingo, upasuaji mkubwa sana wa tumbo na ule wa hemipelviktomi (kukatwa mguu na kiuno).103 Baada ya kuondoa katika Shahidi mtanuko ateri wa ubongo, Dakt. J. Posnikoff hakukubaliana na “kauli ya sasa ya wapasuaji neva walio wengi kwamba kutia damu mishipani ni kwa muhimu kabisa” kwa ajili ya upasuaji huo wa ubongo. Yeye alichagiza wapasuaji wengine “wasifanye kawaida ya kuwanyima upasuaji mkubwa wale ambao huenda wakawa katika uhitaji mkubwa sana lakini wasioweza kiadili kukubali kutiwa damu mishipani.”104

162. Ni mambo gani Dakt. Philip Roen ambayo ameona?

162 Mkataa uliofikiwa kukatwa na Dakt. Philip R. Roen katika “Upasuaji Mkubwa wa Kifereji cha Mkojo Bila Kutia Damu Mishipani” ulikuwa:

“Mambo ambayo sisi tumejionea kuhusiana na Mashahidi wa Yehova wenye kuhitaji taratibu za upasuaji yametuonyesha kwamba kutiwa damu mishipani si kwa muhimu kabisa hata wakati vitembo vya hemoglobini vinapokuwa chini—chini hata kufikia Gramu 5 kwa kila mililita 100. . . . Msimamo wa Mashahidi wa Yehova katika kukataa kutiwa damu mishipani wakati wa upasuaji mkubwa na wa uangalifu sana unaohitajiwa kabisa, unaandaa tatizo kubwa na jaribu la ustadi wa mpasuaji kifereji cha mkojo. Wagonjwa hao hawawezi na ni lazima wasiachwe kwa sababu ya itikadi zao za kidini. Sisi hatukusita-sita kufanya taratibu zo zote na hata zote za upasuaji usoni mwa kibadala cha damu kilichokatazwa.”105

Wewe Utafanya Nini?

163, 164. Ni mambo gani ya hakika yanayoonyesha kwamba msimamo wa Mashahidi kuhusu kutiwa damu mishipani unaweza kukubaliwa kitiba?

163 Katika kufikiria msimamo ambao Mashahidi wa Yehova wanachukua kuhusiana na damu, sisi tumeweka fikira kwenye pande fulani za maana. Tumechunguza msingi unaowafanya wakatae damu na tumeona kwamba wao wanafanya hivyo kwa sababu za kidini zenye msingi wa Biblia. Pia tumeyapitia maadili yanayohusishwa ndani, tukionyesha kwamba ni haki ya kila mtu kuamua ni jambo gani litakalofanywa kwa mwili wake na kuamua kwa ajili yake mwenyewe na watoto wake utibabu anaotaka. Katika kuchanganua jukumu la daktari, tumeona kwamba kutibu mtu kulingana na itikadi za mgonjwa huyo kunapatana na zile kanuni za msingi za kazi ya wanatiba. Na, katika kuzungumzia zile pande za kitiba zinazohusiana na kutia damu mishipani, sisi tumeonyesha kwamba msimamo ambao Mashahidi wa Yehova wanachukua unaweza kukubaliwa kitiba. Historia za visa vilivyotukia huthibitisha kwamba katika visa vilivyo vingi, madaktari wenye ustadi na ushujaa wanaweza kufanikiwa kutibu wagonjwa Mashahidi bila kutumia damu.

164 Ingawa huenda yote yakawa hivyo, haitupasi kulitazama jambo hili kuwa zungumzo la kuwaziwa tu la suala lenye kupendeza. Kila mmoja wetu huenda akahitajiwa kutumia habari hii katika kuamua atafanya nini yeye binafsi.

Namna gani daktari?

165, 166. (a) Kwa sababu ya mambo yote ya hakika yaliyotangulia, daktari amepaswa kuthamini nini juu ya Mashahidi wa Yehova? (b) Hii inamaanisha nini katika kutenda kwake hasa?

165 Kwa msaada wa yote ambayo tumefikiria, daktari anapaswa athamini kwamba Mashahidi wa Yehova si washupavu wa kidini ‘wenye kujiua’ wanaopinga utunzaji wote wa kitiba. Bali, ni wenye kiasi, watu wa kiadili walio na hamu nyingi ya kubaki wakiwa hai; wao wanapenda uhai na afya njema, na ndiyo sababu wanatafuta utunzaji wa kitiba unaostahili. Lakini inapasa daktari afahamu pia kwamba Mashahidi wa Yehova wamefikiria itikadi zao za kidini kwa uzito, na wanasadikishwa kabisa kabisa kwamba ni lazima wao na jamaa zao wasikubali damu. Kwa hiyo, wakati wafanya kazi wa tiba wanapokabiliwa na katao hili la damu, haiwapasi kuliona kuwa kisisimuko tu cha hisia-moyo kinachoweza kupuuzwa. Ni usadikisho wa kidini ulio wa maana, unaopasa kustahiwa, kuheshimiwa.

Hili lamaanisha nini kimatendo?

166 Lamaanisha kwamba, ili kustahi kanuni ambazo ushuhuda wa wakati uliopita umeonyesha zinastahili kuheshimiwa, ni lazima damu isitumiwe kinguvu juu ya mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Ni kweli kwamba ili daktari akubalie usadikisho wao wa kidini, huenda akahitajiwa kurekebisha njia yake ya kawaida ya kutibu. Lakini, kwa kutazama mambo juu ya msingi wa mfiko-mrefu, je! si afadhali masadikisho ya kidini ndiyo yawekee utibabu vizuizi fulani, badala ya itikadi msingi za kidini zitolewe imla au kuvunjwa na zoea la kitiba la sasa? Mfikirio uliosawazika unathibitisha jambo hilo kuwa kweli. Kwa kushirikiana na mmoja wa Mashahidi wa Yehova, daktari anaweza kuonyesha kujitoa kwake kikweli kutetea haki za kibinadamu na staha yake kwa ajili ya tumizi huria la dhamiri ya kidini. Wakati ule ule yeye atakuwa akitibu “mwanadamu mzima-mzima,” akitumia utibabu ule unaotumika ili kuponya mgonjwa kimwili bila kumdhuru ki-hisia-moyo au kiroho. Hiyo itakuwa kwa masilahi ya kudumu ya mgonjwa, na itafaharisha yale maadili ya msingi ambayo daktari amejitoa kutetea.

Namna gani Mashahidi wa Yehova au wengine wanaohangaikia kutumia Neno la Mungu katika maisha zao?

167, 168. Ni shauri gani wanalopewa Mashahidi wanapokabiliwa na suala la kutiwa damu mishipani?

167 Pitio letu juu ya swali la damu linapasa kuongezea zaidi staha ya mtu kwa maagizo ya Biblia dhidi ya kuendeleza uhai wa mtu kwa kutumia damu.

168 Kwa kufaa kila Mkristo anaazimu aendelee kuwa mthibitifu katika imani yake. Katika kushughulika na wafanya kazi wa tiba, inampasa Mkristo aonyeshe kiasi na roho ya ushirikiano, wakati ule ule akionyesha wazi kwamba ni lazima utibabu wo wote unaotolewa upatane na itikadi zake za kidini, kama vile kukataa kwake kutiwa damu mishipani. Ikiwa upasuaji unahitajiwa, litakuwa jambo la maana kuzungumza na madaktari kabla ya wakati juu ya msimamo wa Kikristo kuhusiana na damu, ili kupata uhakikishio wao kwamba chini ya hali zo zote damu haitatumiwa kabla, wakati au baada ya upasuaji. Na ikiwa daktari fulani hahisi kwamba anaweza kupasua bila kutumia damu, Mkristo akijua hivyo mapema anaweza kutafuta utumishi wa tabibu mwingine.

169. Kwa msimamo wao juu ya damu, Mashahidi wanadhihirisha nini, kupatana na kielelezo gani cha Wakristo wa mapema?

169 Katika kujitahidi kutetea sheria ya Mungu kuhusiana na damu, Mashahidi wa Yehova wanadhihirisha uthamini wao wa uhakika wa kwamba uhai wao umetoka kwa Muumba na Mpaji-Uhai, na unamtegemea Yeye. Yeye amesema katika Biblia kwamba furaha ya Mkristo na uhai wake utakaoendelea wakati ujao vinategemea imani na utii. (1 Yohana 2:3-6) Kwa sababu hiyo Wakristo wa mapema walikuwa na nia ya kuhatarisha uhai wao wa sasa badala ya kwenda kinyume cha itikadi zao za kidini. Mashahidi wa Yehova leo wameazimu jinsi hiyo hiyo kudumisha uhusiano wao mwema pamoja na Mungu. Hivyo wataendelea kutii amri ya Biblia ‘kushika mwiko wa damu.’—Matendo 15:29, NW.

MAREJEZO

1. The Gift Relationship (1971), by Professor Richard M. Titmuss, p. 27.

2. Calvin’s New Testament Commentaries; The Acts of the Apostles, Vol. II, p. 50.

3. Genesis—A Commentary (1961), by Gerhard von Rad, p. 128.

4. Genesis (1974), by B. Jacob, edited by E. I. and W. Jacob, p. 64.

5. The Torah: A Modern Commentary, Genesis (1974), by W. Gunther Plaut, p. 86.

6. Zürcher Bibelkommentare 1. Mose 1-11 (1967), p. 330.

7. The History of the Christian Church (1837), by William Jones, p. 106.

8. Tertullian, Apologetical Works, and Minucius Felix, Octavius, translated by Rudolph Arbesmann (1950), p. 33.

9. The Ante-Nicene Fathers, Vol. IV, kur. 85, 86.

10. The Ante-Nicene Fathers, Vol. IV, p. 192.

11. The Ecclesiastical History of the Second and Third Centuries (1845), by John Kaye, Bishop of Lincoln, p. 146.

12. The Acts of the Apostles (1958), by Guiseppe Ricciotti, p. 243.

13. Nicene and Post-Nicene Fathers of the Christian Church, by Philip Schaff and Henry Wace, Vol. XIV, p. 395.

14. Tertullian, Vol. I, translated by C. Dodgson (1842), p. 109.

15. Luther’s Works, Vol. 41 (Church and Ministry III), edited by Eric W. Gritsch, p. 28.

16. The Complete Works of the Rev. Andrew Fuller (1836), p. 751.

17. The American Surgeon, July 1968, p. 542.

18. Fordham Law Review, Vol. 44, 1975, pp. 23, 24.

19. American Journal of Obstetrics and Gynecology, June 1, 1968, p. 395.

20. Medicolegal Forms with Legal Analysis (1976), pp. 24, 38.

21. Medical Tribune (in German), March 19, 1976, p. 30.

22. Rutgers Law Review, Vol. XXVI, 1973, p. 244.

23. The Wisconsin Medical Journal, August 1967, p. 375.

24. The Journal of the American Medical Association, September 5, 1966, pp. 794, 795.

25. Fordham Law Review, Vol. 44, 1975, p. 29.

26. The Journal of Abdominal Surgery, June 1967, p. 160.

27. The Cape County Journal, June 1967, p. 5.

28. University of San Francisco Law Review, Summer 1975, p. 28.

29. Surgery, Gynecology & Obstetrics, April 1959, pp. 503, 504.

30. Medicolegal Forms with Legal Analysis (1976), p. 85.

31. University of San Francisco Law Review, Summer 1975, pp. 27, 28.

32. Emergencies in Medical Practice (1971), edited by C. Allan Birch, p. 564.

33. Deutsche Medizinische Wochenschrift, December 19, 1975, p. 2622.

34. New York State Journal of Medicine, May 1976, p. 766.

35. Fordham Law Review, Vol. 36, 1968, p. 651.

36. Medical Tribune (in German), March 19, 1976, p. 30.

37. Natanson v. Kline et al., 186 Kan. 393, 350 P.2d 1093, 1104.

38. Canadian Medical Association Journal, February 18, 1967, p. 432.

39. Forensic Science, July 1972, p. 135.

40. God, Blood and Society (1972), by A. D. Farr, p. 115.

41. Crime and Delinquency, April 1968, p. 116.

42. Texas Medicine, December 1970, p. 25.

43. The Journal of the American Medical Association, July 3, 1967, p. 150.

44. Ouest-France, March 10, 1975.

45. Drugs (1973), Vol. 6, p. 130.

46. Obstetrik och gynekologi (1962), edited by Carl Gemzell, p. 206.

47. God, Blood and Society (1972), by A. D. Farr, p. 32.

48. Die Welt, October 14, 1975.

49. The Journal of the American Medical Association, April 12, 1976, p. 1611.

50. Clinical Hematology (1974), by Professor Maxwell M. Wintrobe, p. 474.

51. Le Concours Médical, April 1, 1972, p. 2598.

52. Oasis, February 1976, pp. 23, 24.

53. Medical Economics, December 11, 1967, p. 96.

54. The National Observer, January 29, 1972, p. 1.

55. Southern Medical Journal, April 1976, p. 476.

56. Chicago Tribune, October 10, 1969, p. 2.

57. Surgery, February 1974, pp. 274, 275.

58. Hematology (1975), by Professor James W. Linman, p. 991.

59. Journal of Forensic Sciences, January 1969, p. 87.

60. The Gift Relationship (1971), by Professor Richard M. Titmuss, p. 142.

61. Journal of Hygiene, October 1974, p. 173; Southern Medical Journal, April 1976, p. 477.

62. Arizona Medicine, April 1974, p. 263.

63. Annals of the New York Academy of Sciences, January 20, 1975, p. 191.

64. The American Journal of the Medical Sciences, September-October 1975, pp. 276, 281; Morbidity and Mortality Weekly Report, May 7, 1976, p. 3; Inspection News, November-December 1972, p. 18.

65. Scandinavian Journal of Infectious Diseases, Vol. 6, 1974, p. 286.

66. Hematology (1975), by Professor James W. Linman, p. 994.

67. The Gift Relationship (1971), by Professor Richard M. Titmuss, p. 147.

68. The Journal of Legal Medicine, June 1976, p. 19.

69. South African Medical Journal, January 24, 1976, p. 107.

70. Die Welt, December 9, 1974.

71. General Principles of Blood Transfusion (1973), p. 15.

72. Tropical Diseases Bulletin, September 1972, pp. 828, 848.

73. Hematology (1975), by Professor James W. Linman, p. 995.

74. Surgery, February 1974, p. 275.

75. Medicolegal Forms with Legal Analysis (1976), p. 83.

76. The Journal of Thoracic and Cardiovascular Surgery, July 1974, p. 3.

77. Mayo Clinic Proceedings, November 1976, p. 725.

78. Medical World News, December 4, 1970, p. 7.

79. American Journal of Obstetrics and Gynecology, June 1, 1968, p. 395.

80. Hematology (1975), by Professor James W. Linman, p. 985.

81. South African Medical Journal, January 24, 1976, p. 107.

82. Anaesthesia, July 1968, pp. 395, 396.

83. Archives of Surgery, January 1969, p. 52.

84. Anaesthesia, July 1968, p. 413; Mayo Clinic Proceedings, November 1976, p. 726.

85. Postgraduate Medicine, November 1959, p. A44.

86. Canadian Anaesthetists’ Society Journal, January 1975, p. 8.

87. RN Magazine, May 1975, p. 38.

88. Bibliotheca Haematologica, “Intentional Hemodilution,” No. 41, 1975, p. 270.

89. Anaesthesia, March 1975, p. 150.

90. Columbus, Ohio, The Dispatch, August 31, 1972, p. 1B.

91. Anaesthesia, July 1968, pp. 418, 419.

92. Annals of the New York Academy of Sciences, August 14, 1968, p. 905; The Journal of the American Medical Association, March 29, 1971, p. 2077.

93. Blood Transfusion in Clinical Medicine (1972), by Professor P. L. Mollison, pp. 150, 153.

94. Surgical Clinics of North America, June 1975, p. 671.

95. Anaesthesia, July 1968, p. 416.

96. The Journal of the American Medical Association, February 5, 1968, pp. 399, 401.

97. Canadian Anaesthetists’ Society Journal, January 1975, p. 12.

98. The Elks Magazine, August 1976, p. 14.

99. The San Diego Union, Sunday, December 27, 1970, p. A-10.

100. The Journal of the American Medical Association, December 3, 1973, p. 1231.

101. The Toronto Star, November 22, 1975, p. A8.

102. New York State Journal of Medicine, May 1976, pp. 765, 766.

103. The Journal of the American Medical Association, February 5, 1968, p. 399.

104. California Medicine, February 1967, pp. 124, 127.

105. New York State Journal of Medicine, October 15, 1972, pp. 2526, 2527.

[Maelezo ya Chini]

a Habari-chanzo kwa ajili ya marejezo, kurasa 61-64.

b Marejezo mengine (kutoka karne ya pili na ya tatu) yenye kuunga mkono utumizi huu wa Matendo 15:28, 29 yanapatikana katika: Against Celsus VIII, 29, 30 cha Origen, na Commentary on Matthew XI, 12; The Instructor II, 7 cha Clement na The Stromata IV, 15; The Clementine Homilies VII, 4, 8; Recognitions of Clement IV, 36; Dialogue XXXIV cha Justin Martyr; Treatises XII, 119 cha Cyprian; The Teaching of the Twelve Apostles VI; Constitutions of the Holy Apostles VI, 12; On the Death of the Peregrinus 16 cha Lucian.

c Uchunguzi unaonyesha kwamba kwa kutumia utibabu wenye chuma, uzalishi wa chembe nyekundu unaweza kuongezwa kufikia mara mbili mpaka nne za ile kadiri ya kikawaida.77

d PVP (polyvinylpyrrolidone) ingali pia ikitumiwa katika mabara fulani-fulani.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki