Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 3/22 uku. 11
  • Baraza la Makanisa Ulimwenguni—Lakubali Kutofautiana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Baraza la Makanisa Ulimwenguni—Lakubali Kutofautiana
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Umoja Unatambulisha Ibada ya Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Sehemu ya 22: 1900 na kuendelea—Dini Bandia— Yafikiliwa na Wakati Wayo Uliopita!
    Amkeni!—1990
Amkeni!—1995
g95 3/22 uku. 11

Baraza la Makanisa Ulimwenguni—Lakubali Kutofautiana

WAKATI WA Agosti 3 hadi 14, 1993, jiji la Santiago, Hispania, lilikaribisha kundi lisilo la kawaida la wapigrimu. Jiji hilo liliandaa Kongamano la Ulimwengu juu ya Imani na Kanuni ya Kidini, likidhaminiwa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Lengo la wajumbe lilikuwa gumu—kuhuisha ile jitihada ya kuunganisha makanisa ya Jumuiya ya Wakristo.

Hali ilionyeshwa kwa wazi kuwa “muungamano usiotenda” na Desmond Tutu, askofu mkuu wa Kianglikana kutoka Afrika Kusini. “Twachovya vidole vyetu vya miguu majini, bali twakosa ujasiri wa kujitumbukiza ndani,” yeye alilalama.

Ujitumbukizaji wa muungano wa dini ulimwenguni hautakuwa rahisi. Migawanyiko miongoni mwa wajumbe ilitokea hata wakati wa sherehe ya ufunguzi katika kathedro ya Katoliki katika Santiago. Ule “Wimbo wa Mt. Yakobo,” ulioimbwa wakati wa ibada, ulichambuliwa kuwa ulitukuza zile karne za uonezi wa Wakatoliki Wahispania dhidi ya Wayahudi, Waislamu, na Waprotestanti, hata ingawa askofu mkuu wa Katoliki Rouco aliwatia moyo washiriki ili ‘kuwa na roho ya pigrimu na kutafuta upatano miongoni mwa Wakristo.’

Je, kuna msingi wowote ambao waweza kutumika ili kupatanisha Wakatoliki, Waorthodoksi, na Waprotestanti? Kundi moja la uchanganuzi lilidokeza kwamba makanisa tofauti tofauti yaone Imani ya Nicene “kuwa wonyesho wa msingi wa imani ya kimitume.” Walitumaini kwamba imani hii ingeweza kutumika “kama njia ya kuufikia umoja wa imani,” hata ingawa huenda kuwe na “utofautiano wa maoni.”

Ule “utofautiano wa maoni” ulijidhihirisha wenyewe tena na tena wakati wa kongamano hilo. Wajumbe wa Orthodoksi na Katoliki walitokeza mapingamizi yao kwa uamuzi wa Anglikana wa kukubali kutawazwa kwa wanawake. Kibishanio kingine kilikuwa ule uhasama kati ya makanisa ya Orthodoksi na Katoliki katika nchi za ule uliokuwa Ukomunisti. Askofu mkuu Iakovos wa Kanisa Orthodoksi la Kigiriki alidai kwamba lilikuwa kosa kusema juu ya “kueneza evanjeli upya kwa watu ambao kwa karne nyingi wamekuwa Wakristo” bali waliopatwa na masaibu ya kuishi kwa miongo chini ya Ukomunisti usioamini kuwako kwa Mungu. Kwa kweli, ripoti ya kongamano hilo ilishutumu “kugeuza imani” kuwa kizuizi cha umoja, hata ingawa lilikubali ule uhitaji wa ‘uelewevu ulio wazi zaidi wa hali ya umishonari ya kanisa.’

Samuel B. Joshua, askofu wa Bombay, kwa kununa alifafanua muungano wa makanisa kuwa “dhana ya kuwazia.” Baada ya yeye mwenyewe kujionea matatizo yaliyohusika katika kuunganisha madhehebu sita katika India, alisema “mafaa yamekuwa madogo” ilhali magumu “yamekuwa yasiyovumilika.” Yeye aamini kwamba muungamano wa Wakristo haupaswi kutafutwa katika “mafundisho na kanuni za kanisa.”

Lakini umoja unaopuuza mafundisho ungeweza kuwa umoja wa kweli? Je, dini ambazo bado ‘hazijui hali ya umishonari ya kanisa’ zingeweza kuwa kweli zafuata Kristo? Paulo alisema wafuasi wa kweli wa Kristo wapaswa kuendelea ‘kunia mamoja.’ (2 Wakorintho 13:11) Kukubali tu kutofautiana hukosa kutimiza kiwango hicho.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki