Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/8 kur. 13-14
  • Si Siri Tena Kamwe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Si Siri Tena Kamwe
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Barua Yenye Huzuni
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2018
  • Siri Unayoweza Kuwaambia Wengine
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Pambano la Muda Mrefu Dhidi ya Utumwa
    Amkeni!—2002
  • Vita Ambayo Itavimaliza Vita
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 5/8 kur. 13-14

Si Siri Tena Kamwe

“Tafadhali iweke siri hii na usiisomee mgeni yeyote”

BILA usanifu wa utamukaji na utuaji wa kisasa, katika 1863, wakati wa Vita ya Kiraia ya Marekani, William H. Morey aliandika onyo hili la utangulizi akiwa katika Acquia Creek, Virginia, kwa mke wake mchanga, Elisa Ann, katika Pennsylvania. Alikuwa na umri wa miaka 24, akiwa ameoa hivi majuzi, na askari aliyejiandikisha kutoka Hanover Township, Pennsylvania. Alipigania upande wa Mwungano wa Majimbo ya Kaskazini. Na maadui wake? Wale Waamerika wengine waliounga mkono Mwungano wa majimbo ya kusini ambayo yaliondoka kutoka kwa Mwungano, kwa kutoa hoja kwamba Mwungano (wa kaskazini) uliingilia kutoka Washington, D.C, mambo yao ya kiuchumi. Ni nini Morey alitaka kiwekwe siri? Muda si muda tutapata ni nini, lakini kwanza tufikirie habari fulani itakayotuelewesha katika jambo hili.

Vita ya Kiraia ya Marekani ililipuka katika 1861 baada ya majimbo saba ya kusini kuondoka kutoka kwa Mwungano, mara yalifuatwa na manne zaidi. Haya 11 yaliunda Mwungano. Uendelezo wa utumwa ulikuwa mojapo masuala makubwa kati ya Kaskazini na Kusini. Ilisemwa na wenye mashamba makubwa ya kusini kwamba Kaskazini ingeweza kumaliza utumwa, kwa sababu uchumi wao ulitegemezwa na maelfu ya Wanaulaya wahamiaji. Hata hivyo, uchumi wa kusini, uliotegemea pamba, ulihitaji karibu watumwa milioni nne ili unawiri. Angalau, hilo ndilo waliloamini.

Na je, Rais Abraham Lincoln aliamini nini? Aliandika katika Agosti 1862 hivi: “Dhamira yangu kubwa katika vita hii ni kuuokoa Mwungano, na si ama kuuokoa ama kuuharibu utumwa. Ikiwa ningeweza kuokoa Mwungano bila kuacha huru watumwa wowote, ningefanya hivyo: na ikiwa ningeweza kuuokoa kwa kuwaachilia huru watumwa wote, ningefanya hivyo.” Muda mfupi baada ya hili, Januari 1, 1863, Lincoln alitangaza uhuru kwa ajili ya watumwa wote waliokuwa chini ya wanamgambo. Jambo hili lilipiga pigo kubwa mno la kiuchumi kwa wenye watumwa walioishi kusini, ambao, kama walivyoonelea, walipoteza “dola bilioni kadhaa za mali ya watumwa” bila kurudishiwa gharama yoyote.

Hiyo vita ya kiraia yenye msiba iligharimu uhai wa angalau Waamerika wachanga 618,000 wakati wa miaka 1861-1865, kwa kuongezea wengi zaidi waliojeruhiwa—majeruhi wengi wa Amerika kuliko vita nyingine yoyote. William Morey alijipata ameingia katika mgongano huu alipoandika katika kitabu chake cha matukio ya kila siku na barua yake ya siri katika Januari 25, 1863. Akiwa askari wa kawaida, mikataa yake ya siri kuhusu vita ilikuwa nini?

Barua Yenye Huzuni

Afungua barua yake kwa kumshukuru mke wake kwa ajili ya “hiyo tumbaku na vitu vingine” ambavyo alikuwa amempelekea halafu aandika hivi: “Naamini na kuona kwamba hii vita ni chambo kamili na vita ya kufanyiza fedha kila mtu hujaribu kufanya fedha nyingi na hilo ndilo jambo pekee linalofanya vita viendelee na sasa tunaona jinsi vita vinavyoendelea kukua ikiwa tu nilikuwa nyumbani tena ningempiga ngumi mtu wa kwanza kuniomba nijiandikishe tena jeshini hapa twatendewa kama mbwa hata mbwa hutendewa afadhali kutuliko na nakwambia ikiwa tu nilikuwa na fedha kwa miezi hii minne ningejaribu kutoroka twatendewa vibaya zaidi kila siku.”a

Alieleza mahali walipowekwa hivi: “Ni mahali pazuri na mwono mzuri unaweza kuona mashua zikija kwenye [mto] potomac . . . baadhi ya siku hapa tunafanya kazi sana kupakia magari ya [reli] na tunapata nusu ya chakula tuhitajicho na idadi kubwa ya wavulana wanaongea kuhusu kutoroka ikiwa wangekuwa na fedha zao . . . twapiga miguu na kufanya kazi ngumu wakati wote.”

Hata hivyo, unyimivu huu si kitu ukilinganishwa na ule unaowafika walio vitani. Katika pigano moja, jenerali wa kusini D. H. Hill alipoteza wanaume wake 2,000 kati ya 6,500. Yeye aliandika hivi: “Hiyo haikuwa vita, yalikuwa mauaji ya kimakusudi.” (Gray Fox, kilichoandikwa na Burke Davis) Masharti ya kulazimishwa kuwa askari Kaskazini na Kusini yalikuwa kwamba wale wenye fedha wangeweza kuachiliwa ama kuondolewa kutoka kwa utumishi wa jeshi kwa kulipa fedha. Walio maskini zaidi katika Kusini walilalamika kwamba ilikuwa “vita ya tajiri na pigano la maskini.” Koplo Morey alilipwa zaidi kwa kutumikia kwenye vita, naye akajenga kiokeo cha mikate.

Wale walioishia kambi za gereza, kama vile Andersonville, Georgia, mara nyingi walikuwa chini ya hali zenye kusononesha. “Kijito fulani kilitiririka polepole kupitia kambi hiyo. Maradhi na viwango vya kifo vilikuwa vya juu zaidi, kukiwa na mfumo wa usafi usiotosha, msongamano, kupatwa kwa urahisi na maambukizo, mlo usio kamili huo ukichangia hali zisizofaa.” (Andersonville, broshua fulani) Hata mabaya zaidi yalikuwa mauaji ya kimakusudi, matendo ya kuibiwa yaliyotendewa wafungwa na wahalifu wajanja, walioitwa Wavamizi, ambao pia walikuwa wafungwa. Walikuza “ufasiki wa kuiba na jeuri.” Kutokana na visababishi mbalimbali, angalau askari 12,920 walikufa kwenye Andersonville.

Katika 1995, je, mwanadamu amefanya maendeleo yoyote zaidi? Je, mafunzo ya historia watu walijifunza lolote kutokana nayo? Uchinjaji wenye kutisha katika Rwanda, Liberia, Balkani na mahali kwingine kwingi kwa vita ni vielelezo vya majuzi vya unyama wa mwanadamu kwa mwanadamu. Waumini Wakatoliki na Waothodoksi, wajapodai kuwa Wakristo, wameshindwa kuishi kulingana na kielelezo chenye upendo cha Kristo Yesu. Ni Mashahidi wa Yehova tu wamedumisha kutokuwamo kwao na kukataa kujifunza ama kufanya vita kamwe tena. Na hilo si siri.—Isaya 2:4; Mika 4:3.

[Maelezo ya Chini]

a Uendelezo usio mzuri na ukosefu wa vituo ni kulingana na barua yenyewe.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki