Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/8 uku. 32
  • Kusitawisha Jamii Ifaayo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kusitawisha Jamii Ifaayo
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 5/8 uku. 32

Kusitawisha Jamii Ifaayo

MAKAMU wa mhariri wa gazeti la New African aliandika majuzi hivi: “Nenda katika nchi yoyote ya Kiafrika leo nawe utapata kikundi kidogo cha walio bora kikiishi kwa ustarehe huku halaiki ya watu wa hali ya chini ikiteseka katika umaskini wenye kulemea. . . . Twaweza kuepukaje mtego huu wa umaskini? Suluhisho la kisahili ni: ondoa kikundi cha walio bora na ugawanye utajiri. Kwa uhalisi hilo halifanyi kazi. Kwanza, hakuna utajiri wa kutosha kwa wote. Jambo la pili, ondoa kikundi cha walio bora na mara kingine kitachukua mahali pacho. Jambo la tatu, majaribio katika dhana za usoshalisti [yamefaulu] tu katika kueneza umaskini kwa usawa.

“Kuna suluhisho moja tu kwa maendeleo ambalo limefanya kazi katika nchi zote katika mihula yote: usitawishi wa mtu mmoja-mmoja. Ni watu wanaofanyiza jamii. Watu wenye elimu nzuri, wenye afya, walio chanya na wenye ubuni kwa wazi hutokeza jamii nzuri, na tendaji.”

Makamu wa mhariri angelikuwa akitafuta kielelezo, angepata kimoja katika Mashahidi wa Yehova. Katika Afrika, kwa kweli ulimwenguni pote, Mashahidi wanafanya kazi ili kusaidia watu wawe washiriki wenye elimu, na wafaao wa jamii ya kitufe. Miongoni mwa mambo mengine, wao wanafundisha watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wajue kusoma na kuandika. Kupitia vichapo vyao, wao hutoa maagizo katika usafi wa ujumla, utunzaji wa afya, na mahusiano ya kifamilia. Kwenye mikutano yao na vilevile mtu mmoja-mmoja, Mashahidi hutiana moyo mmoja na mwenzake kutii shauri la Biblia la kuwa mfuatiaji haki, mwenye bidii ya kazi, na mwenye kutokeza mazao.

Tokeo ni jamii imara, tendaji inayofanyizwa kwa karibu watu milioni tano ulimwenguni pote. Lakini Mashahidi hawachukui sifa kwa jambo hili. Wanaelekeza ufanisi wao wa kiroho kwa Mungu anayeishi, asemaye: “Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.”—Isaya 48:17.

Ikiwa ungependa habari zaidi kuhusu Biblia na shauri layo lenye kutumika, tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika Jumba la Ufalme la mahali penu, au uandikie anwani iliyo karibu zaidi ipatikanayo kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki