Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/22 uku. 27
  • Jaribio la Makasisi la Kuwafikia Vijana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jaribio la Makasisi la Kuwafikia Vijana
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Daima Kaza Uangalifu kwa Kufundisha Kwako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Kwa Nini Sisi Twahitaji Maarifa Sahihi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Wafundishe Wapole Kutembea Katika Njia ya Mungu
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Jinsi ya Kuwasaidia Wengine Washike Amri za Kristo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2020
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 5/22 uku. 27

Jaribio la Makasisi la Kuwafikia Vijana

“Ukasisi wa Chuo Kikuu cha McGill . . . uliingiliwa na kikoa cha wahuni wenye nywele zenye mafuta-mafuta na waliovalia majaketi ya ngozi,” likaripoti The Gazette la Montreal, Kanada. Ingawa hivyo, “wahuni” hao, hawakuwa wale wa kawaida. Walikuwa washiriki wa jamii ya makasisi—makasisi wa chuo kikuu—na walikuwa sehemu ya kile gazeti hilo liliita “wimbi jipya la wanatheolojia lifanyalo kazi pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu kutafuta mnurisho wa kiroho.”

Makasisi hao walivalia kama “wahuni” mvao huo ukiwa kama kibandiko cha matangazo ili kutangaza utumishi wao kwenye chuo hicho. Mmoja wao, mhudumu Mpresbyteri aitwaye Roberta Clare, alieleza hivi: “Tuliamua kubuni kibandiko cha matangazo cha uhuni kwa sababu twataka kuondoka kutoka ile sura ya kihukumu ya watakatifu zaidi yenu ambayo mara nyingi watu hutuona kwayo.”

Ingawa hivyo, yeye alitaja kwamba wanafunzi wengi zaidi kuliko wakati uliopita wanapendezwa na kujifunza dini katika shule. Wengi wanang’ang’ana na maswali mazito na hutazamia majibu kutoka kwa walimu wa chuo kikuu na makasisi. Gazeti hilo lilimhoji mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa mdadisi kuhusu kwa nini dini ina athari yenye nguvu sana katika jumuiya, kwa nini kuna dini nyingi sana, na kwa nini yaonekana hizi zinasababisha taabu nyingi sana ulimwenguni. Alikuwa akimenyana na utambulisho halisi wa Yesu Kristo na vile vile swali juu ya chanzo cha ulimwengu wote mzima.

Je, makasisi hawa hutumia Biblia ili kusaidia wanafunzi wapate majibu ya Mungu kwa maswali hayo mazito? Yaonekana, ni kwa nadra sana. Wimbi hili Jipya la wanatheolojia lilikubali miongoni mwalo kutogeuza watu dini, ambako wanakuona kuwa “uibaji-kondoo.”

Ingawa huenda wakawa na nia nzuri, makasisi hao wameenda kando mbali sana kutoka kwenye mbinu za kufundisha ambazo Kristo na wafuasi wake walitumia. Wakristo wa mapema hawakujihangaisha na dhana ya “uibaji-kondoo,” ama kujizuia kufundisha Neno la Mungu na kusaidia watafuta-kweli wanyofu kulifahamu. (Luka 24:44, 45; Matendo 20:20) Kwa vyovyote, ujuzi sahihi wa Yehova Mungu na Mwana wake, Yesu Kristo, wahitajika ili kupata uhai wa milele. (Yohana 17:3) Mapenzi ya Mungu ni kwamba namna zote za watu zapaswa “kuja kwenye ujuzi sahihi wa kweli” ili zipate kuokolewa.—1 Timotheo 2:3, 4, NW.

Kazi ya Mashahidi wa Yehova inatia ndani kuongoza mafunzo ya Biblia nyumbani bila malipo pamoja na wale wanaotaka maswali yao ya Biblia yajibiwe. Mashahidi wa Yehova katika jumuiya yenu watafurahi kukusaidia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki