Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 6/8 kur. 26-27
  • Je, Nyumba Yenu ni Yenye Kukinza Tetemeko la Dunia?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Nyumba Yenu ni Yenye Kukinza Tetemeko la Dunia?
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mambo Muhimu Yakinzayo Tetemeko la Dunia
  • Kujenga Jengo Likinzalo Tetemeko la Dunia
  • Tetemeko la Ardhi
    Amkeni!—2002
  • Kukabiliana na Hasara
    Amkeni!—2002
  • Matetemeko Makubwa Zaidi Yanatazamiwa
    Amkeni!—2010
  • Tetemeko la Dunia!
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 6/8 kur. 26-27

Je, Nyumba Yenu ni Yenye Kukinza Tetemeko la Dunia?

Na mleta-habari wa Amkeni! katika Japani

“NISAIDIENI! Nisaidieni!” Katika giza la asubuhi na mapema la Januari 17, 1994, mwanamume fulani alipaaza sauti kutoka chumba cha orofa ya kwanza ambacho katika hicho orofa mbili za juu zilikuwa zimebomoka na kulaliana. Tetemeko la dunia la kipimo cha 6.6 kwenye mizani ya Richter lilikuwa limepiga Los Angeles, California, Marekani, likitwaa uhai wa watu 16 katika jengo hilo. Uharibifu wenye kuhuzunisha wa uhai katika hilo eneo ulikuwa zaidi ya watu 50.

Septemba 30, 1993, tetemeko la dunia la kiwango cha chini kidogo lilipiga jimbo la Maharashtra magharibi mwa India. Liliua watu wengi kufikia 30,000. “Ikiwa lingetukia mahali penginepo ambapo . . . majengo yamejengwa vizuri, halingekuwa lenye msiba mkubwa vile,” akasema Sri Krishna Singh, mtaalamu mmoja wa matetemeko. Nyingi za nyumba katika eneo lililoathiriwa zilijengwa kwa matofali ya matope.

Kwa upande ule mwingine, tetemeko la karibu kiasi hichohicho cha India lilipiga Tokyo, Japani, katika 1985. Hilo lilikuwa lenye nguvu kupita yoyote yaliyopata kupiga hilo eneo kwa miaka 56. Lakini, hakukuwa na vifo, hakukuwa na mioto, hakukuwa na uharibifu wa mali wa kiwango kikubwa. Ni nini kilifanyiza hiyo tofauti?

Jibu moja lapatikana kwenye mbinu za ujenzi zilizotumiwa kwa hayo majengo. Nchi nyingi katika maeneo yaelekeayo kupatwa na matetemeko ya dunia kwa ukawaida huhitaji wahandisi wa ujenzi kushikamana kabisa na kanuni za ujenzi ili kufanyiza majengo yawezayo kukinza tetemeko la dunia. Kama kielelezo, acheni tuone namna majengo yenye kukinza tetemeko la dunia hujengwa katika Japani.

Mambo Muhimu Yakinzayo Tetemeko la Dunia

Majengo ya kikale ya Japani yalikuwa na mambo muhimu yakinzayo tetemeko la dunia yaliyotiwa katika ujenzi bila kujua. Kwa kuwa nyumba zilizo nyingi zilijengwa kwa mbao, unamna wa jointi ulitumiwa. Hili liliruhusu nyumba kuyumba na kunyumbuka wakati wa tetemeko na bado isianguke. Pagoda na kasri zitumiazo kanuni hizi zimeokoka tangu nyakati za kale. Uchunguzi wa majengo haya wafunua kwamba siri iko katika kuwa nyumbufu badala ya kuwa thabiti. Wazo hili latumiwa katika majengo ya kisasa.

Katika majengo yenye kupanda mno, utumizi wenye matokeo wa feleji huamua kama jengo litakinza matetemeko ya dunia ama la. Si tu vizingo vya feleji na mihimili yaweza kutumiwa bali fito za kutia nguvu za feleji zatiwa na kukazwa ndani ya miimo ya saruji, sakafu, na kuta ili kufanyiza jengo lililo imara lakini lenye kunyumbuka. Feleji huandaa unyumbufu ambao husaidia kushikamanisha jengo pamoja tetemeko la dunia ligongapo.

Utafiti mpya umewezesha pia kujua jinsi tetemeko la dunia liyumbishavyo jengo. Jambo hili limeongoza kwenye ufikirio muhimu sana katika kubuni jengo fulani likinzalo tetemeko la dunia: kiasi chalo cha mtikisiko. Jengo dogo ama jengo thabiti lina kiwango cha juu cha mtikisiko, hivyo uharibifu mwingi, kuliko jengo refu ama jengo lenye kunyumbuka zaidi. Kwa kuongezea, ni muhimu kwamba jengo libuniwe ili kutikisika katika kiwango tofauti na kile cha udongo linalosimama juu yawo. Jambo hili litapunguza athari ya udukiziwimbi, ambao hukuza nguvu za huo msukosuko.

Ufikirio mwingine ni msingi. Kampuni moja imefanyia majaribio jengo fulani lililojengwa juu ya vinyeo vya mpira vitumiavyo unato wenye unyevu kwa mafanikio. Hivi hutenda kama vifyonza mshindo na kwa hakika hupunguza athari ya mtetemeko kwa wastani wa asilimia 60 kwenye upande wa juu wa jengo. Katika visa vingine, vifaa vya ujenzi ni lazima vishindiliwe chini kwenye tabaka imara zaidi la mchanga wa chini. Hata orofa ya chini yaweza kuandaa usawaziko unaotosha ili kuzuia jengo lisiegame.

Kujenga Jengo Likinzalo Tetemeko la Dunia

Tawi la Japani la Watch Tower Society lilijenga mwongezo mpya kwenye matbaa yalo katika 1989. Hilo jengo ni meta 67 urefu, meta 45 upana, na orofa sita kwenda juu, likiwa na orofa ya chini kamili. Ili kulifanya kuwa jengo likinzalo tetemeko la dunia, miundo 465 ya saruji ilichimbiwa kwenye ardhi.

Kwenye hilo eneo mbinu isiyofanya makelele na isiyotikisika ilitumiwa ili kushindilia miimo ardhini. Miundo yenye kipenyo cha sentimeta 80 na meta 12 urefu, ilikuwa mabomba. Baada ya keekee likiwa na pekecho lalo kwenye ncha kuingizwa ndani ya ile miundo, liliinuliwa likiwa katika kikao cha uwima juu ya mahali ambapo lingechimbwa. Keekee lilipopekechwa, liliondoa udongo kupitia katikati ya hiyo miundo, na hiyo miundo ilishinikizwa ndi ndani ya hilo shimo lenye kubana. Ili kupata kina kirefu zaidi, sehemu nyingine ya muundo ingeweza kulehemishwa kwenye kipande kilichoshindiliwa tayari.

Mara zilipofika kwenye kina kihitajiwacho, pekecho zilizoko kwenye ncha ya keekee zilipanuliwa, na shimo lililo pana lilichimbwa kwenye mkalio wa muundo. Baada ya keekee kuondolewa, saruji ilishindiliwa kwenye tundu lililo katika muundo, na muundo uliachwa mahali pawo saruji ilipogandamana.

Baada ya miundo yote kuwekwa kwenye msingi, iliunganishwa pamoja na boriti ambazo juu yazo sakafu na kuta za orofa ya chini zingeegemea. Likiwa na msingi wa aina hiyo, jengo lapasa kuweza kustahimili kiwango fulani cha tetemeko kali.

Je, nyumba yenu ni salama wakati wa tetemeko la dunia? Hakuna mbinu yoyote ama tahadhari nyingine au ubuni iwezayo kuhakikishia kwamba jengo fulani litabaki bila kudhurika wakati wa tetemeko. Tetemeko la dunia huenda likawa kubwa mno hivi kwamba hata majengo yaliyoundwa kwa njia bora zaidi yasiweze kustahimili uharibifu walo, kama lile tetemeko kali la dunia katika Kobe, Japani, katika Januari lilivyodhihirisha. Licha ya hilo, kwa kuchagua kuishi katika jengo ambalo lilijengwa kwa umakini, unaweza kuhisi salama zaidi tetemeko la dunia likumbapo eneo lenu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki