Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 10/8 uku. 32
  • Msaada kwa Vijana Wenye Mkazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msaada kwa Vijana Wenye Mkazo
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 10/8 uku. 32

Msaada kwa Vijana Wenye Mkazo

Wakati kijana msichana katika shule ya New Jersey, Marekani, alipoudhika na kukimbia kutoka darasani, mwanadarasa mwenzake alimfuata kwenye vyoo vya wanawake. “Nilipomfikia,” huyo mwanadarasa mwenzake akasema, “alikuwa akilia naye aliniambia kuhusu baadhi ya matatizo ya familia yake. Wazazi wake walikuwa wanataka kutalikiana, naye alisema ilikuwa vigumu kwake kuwa makini darasani. Alinieleza kwamba alikuwa anataka kutoroka nyumbani.”

Mwanadarasa mwenzake alimweleza huyo msichana mwenye mkazo kwamba angependa kumletea kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi. Siku iliyofuata alikileta, akiweka alama kwenye vichwa vya sura kama vile “Sababu Gani ‘Niheshimu Baba Yangu na Mama Yangu’?,” “Kwa Nini Baba na Mama Waliachana?,” “Naweza Kukabilianaje Na Msongo wa Marika?,” na “Je! Niondoke Nyumbani?”

“Nilipompa hicho kitabu,” huyo mwanadarasa mwenzake akasema, “wasichana wengine wawili walikiona nao walikuwa wadadisi. Waliuliza kama wao pia wangeweza kupata nakala. Basi niliwapa kila mmoja nakala ya hicho kitabu. Watoto wengine katika darasa langu walimwona mmoja wa hao wasichana akifungua-fungua hicho kitabu, na wote walitaka kukiona. Hicho kitabu kilipitiwa na darasa lote kwa kibali cha mwalimu.”

Ikiwa ungependa kupata nakala ya Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi au kuwa na funzo la Biblia la nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki