Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 11/8 uku. 32
  • “Machozi Yalitiririka Usoni Mwangu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Machozi Yalitiririka Usoni Mwangu”
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 11/8 uku. 32

“Machozi Yalitiririka Usoni Mwangu”

“Nimefungua tu Amkeni! langu la Machi 8, 1995, na kusoma ile makala kwenye jalada la nyuma lenye kutoa broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa. Makala hiyo ilikuwa na kichwa ‘Imekuwa Vigumu Sana Kukua Bila Yeye.’ Machozi yalitiririka usoni mwangu nilipokuwa nikisoma maelezo kutoka kwa kijana katika Austria ambaye alimpoteza baba yake miaka kumi iliyopita. Nina umri wa miaka 50, na nilimpoteza baba yangu nilipokuwa na umri wa miaka 7. Yeye alikufa kwa kansa alipokuwa na umri wa miaka 39. Nilianza tu kuomboleza kifo chake nilipolazwa hospitalini kwa ajili ya mshuko-moyo mkubwa miaka sita iliyopita. Nimekuwa nikipata tiba kwa miaka mitano iliyopita na nimelazimika kujifunza kukabili mambo magumu sana.

“Hadi niliposoma barua hii kutoka Austria, nilikuwa nikiamini kwamba mimi au imani yangu ilikuwa na kasoro kubwa. Nilifikiri nilikuwa mtu pekee ambaye alikuwa na utupu huu mkubwa ndani na umivu kubwa mno la upweke kwa ajili ya baba yangu. Inatia moyo sana kujua kwamba siko peke yangu na kwamba kuna wengine ambao huhisi kama ninavyohisi.

“Niliisoma broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa kutoka jalada hadi jalada. Kulingana na maoni yangu hicho kilikuwa kichapo bora kuliko vyote vilivyopata kuandikwa kwa mahitaji yangu.”—Bi. A. G., Connecticut, Marekani.

Je, umempoteza mpendwa katika kifo? Je, ungependa kupata faraja ya kweli ambayo Biblia hutoa? Basi jihisi huru kuomba nakala ya broshua hii ya kurasa 32 kwa kuandikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki