Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/8 uku. 22
  • Utendaji wa Kiunabii wa Eliya na Elisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Utendaji wa Kiunabii wa Eliya na Elisha
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 12/8 uku. 22

Utendaji wa Kiunabii wa Eliya na Elisha

ELIYA alikuwa nabii ambaye alitaka mtihani wa uungu ufanywe kwenye Mlima Karmeli. Ufalme wa kaskazini ulikuwa ukifisidiwa na ibada ya Baali. Lakini Eliya alisai kwa ujasiri manabii wa Baali 450 wathibitishe kwamba Baali ndiye aliyekuwa Mungu wa kweli. Saa nyingi za sala ya hisia zenye kupita kiasi kwa upande wao hazikuwa na matokeo yoyote. Kisha Eliya akaandika dhabihu yake, kuilowesha kwa maji kwa kurudia-rudia, na kusali kwa Yehova. Moto ulipoanguka mara moja kutoka mbinguni, kumeza ile dhabihu, na kuramba maji, hao watu walipaaza sauti hivi: “Yehova ndiye Mungu wa kweli!” Kwa hilo, Eliya akaamuru kwamba manabii wa Baali wachinjwe.—1 Wafalme 18:18-40, NW.

Hata hivyo, Eliya alishikwa na hofu alipojua kwamba Malkia Yezebeli alikuwa akipanga kumwua. Yeye alikimbia kilometa zipatazo 150 hadi Beer-sheba na kisha kusafiri kilometa nyingine 300 hadi Mlima Sinai. Yehova hakumkataa Eliya kwa sababu ya kukosa kwake ujasiri kwa muda bali alimhakikishia kwamba kulikuwa na kazi zaidi ya kiunabii kwake kufanya.—1 Wafalme 19:1-18.

Elisha ndiye aliyechukua mahali pa Eliya. Elisha alipozungukwa na magari ya kivita ya Wasiria, alikuwa na imani kutambua kwamba majeshi ya Siria ndiyo kwa kweli yaliyozungukwa—na idadi kubwa sana ya magari ya kivita ya kimalaika!—2 Wafalme 6:15-17.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki