Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/8 uku. 22
  • Mataifa Adui Yaliyoshambulia Israeli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mataifa Adui Yaliyoshambulia Israeli
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 12/8 uku. 22

Mataifa Adui Yaliyoshambulia Israeli

KUZUNGUKA Israeli yalikuwa mataifa adui ambayo yalikuwa na nia ya kuchukua urithi walo. Je, Israeli lingeshindwa? Mradi Israeli lilibaki likiwa lenye uaminifu, uamuzi ulikuwa upande walo. “BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.”—Yoshua 10:14.

Hili lilionyeshwa waziwazi wakati wa utawala wa Mfalme Yehoshafati (936-c. 911 K.W.K.). Majeshi yaliyoungana ya Amoni, Moabu, na Mlima Seiri yalikuja dhidi ya Yuda. Yehoshafati akamsihi Yehova hivi: ‘Tazama jinsi wanavyokuja kututupa kutoka milki yako, uliyoturithisha. Ee Mungu wetu je! hutawahukumu?’ Bila shaka Yeye angefanya hivyo! Yuda lilihakikishiwa hivi: “Vita si yenu bali ni ya Mungu.” Yehova aliwatatanisha adui, akiwafanya wachinjane.—2 Mambo ya Nyakati 20:1-23.

Mwishowe, baada ya karne nyingi za kupigania Israeli, Yehova aliruhusu mataifa adui yalishinde. Katika 740 K.W.K. Waasiria walimaliza ufalme wa makabila kumi “kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya BWANA.” (2 Wafalme 17:7-18) Kisha katika 607 K.W.K., kwa sababu ya kutotii kwao ufalme wa makabila mawili uliharibiwa na Wababiloni. (2 Wafalme 21:10-15; 22:16, 17) Kipindi hiki cha historia ya Israeli chakazia umaana wa kumtii Yehova.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki