Walipokea Zawadi ya Kwanza
Wanafunzi wawili wachanga katika Madras, India, walishiriki zawadi ya kwanza kutokana na kiolezo chao cha kituo cha angani chenye chombo cha angani na uwanja wa kurushia chombo. Mvulana na msichana wachanga, wenye kuonekana katika picha hii, walipata wapi wazo la mradi wao?
Hao vijana walieleza katika barua kwa watangazaji wa Amkeni! hivi: “Twachukua fursa hii kuwashukuru kipekee, kwani tulipokea hizo zawadi kwa sababu tu ya ule mfululizo kuhusu uvumbuzi wa angani ambao ulitokea katika Amkeni! la Septemba 8, 1992, (Kiingereza).”
Amkeni! huchapishwa ili kuelimisha familia nzima. Desturi na watu katika nchi nyingi, maajabu ya uumbaji, sayansi halisi, na mambo yenye upendezi wa mwanadamu, zote hutiwa katika uandishi walo. Kwa kuwa na Amkeni! kwa ukawaida nyumbani kwako, unaweza kusaidia watoto wako kuongeza ujuzi wa ujumla, ambao utawanufaisha shuleni na katika maisha ya baadaye.
Ikiwa ungependa kupokea nakala ya ziada ya Amkeni! au ungependa mtu akutembelee nyumbani kwako ili kuzungumza nawe thamani ya elimu ya Biblia, tafadhali andikia I.B.S.A, Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani iliyo karibu nawe iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.