Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 2/22 uku. 32
  • Zilivuta Uangalifu Wake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Zilivuta Uangalifu Wake
  • Amkeni!—1996
Amkeni!—1996
g96 2/22 uku. 32

Zilivuta Uangalifu Wake

Mnamo Mei 1995 mwanamke mmoja kutoka New York City aliandika barua kwa makao makuu ya Mashahidi wa Yehova katika Brooklyn, New York. Yeye alieleza hivi:

“Nilikuwa nikitembea kwenye barabara ya East 124th St., kati ya First Avenue na Second Avenue. Nikatukia kutazama chini, nao upepo ulikuwa ukipeperusha trakti kadhaa. Niliinama na kuokota trakti tatu zenu, Faraja kwa Walioshuka Moyo, Furahia Maisha ya Familia, na Ni Nani Hasa Anayeutawala Ulimwengu? Nilizisoma zote na kuzifurahia sana.

“Ningethamini sana ikiwa mngekuwa wenye fadhili sana na kuniletea habari zaidi juu ya mtaala wa funzo la Biblia nyumbani bila malipo. Pia, ikiwezekana, ningependa kupokea baadhi ya fasihi zenu. Kwangu mimi, ilikuwa ni baraka kwamba Bwana aliye mwema aliweka zile trakti tatu mbele yangu ili nizipate. Bwana hutenda kazi kwa njia za ajabu.”

Ikiwa ungependa kusoma trakti hizi zenye kuvuta uangalifu au kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki