Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 6/22 uku. 32
  • Je, Una Kiu ya Ujuzi wa Biblia?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Una Kiu ya Ujuzi wa Biblia?
  • Amkeni!—1996
Amkeni!—1996
g96 6/22 uku. 32

Je, Una Kiu ya Ujuzi wa Biblia?

KWA miongo mingi hakukuwa na uhuru wa mazungumzo juu ya Biblia katika nchi za Kikomunisti. Lakini baada ya Vita Baridi, mamia ya maelfu ya watu yameanza kutafuta ujuzi wa Biblia. Ingawa, jambo hilo latukia hasa katika jamhuri za ule uliokuwa Muungano wa Sovieti, ndivyo hali ilivyo pia katika nchi za Ulaya Mashariki.

Kwa kielelezo, mazungumzo ya Biblia yalimletea shangwe kuu mwalimu mmoja wa biolojia na kemia mwenye umri wa miaka 45 katika Pecs, Hungaria. “Lilikuwa jambo la kusisimua na lenye shangwe kuzungumza na mmoja wa Mashahidi wa Yehova nilipozuru Budapest,” akaandika mwalimu huyo. “Napenda kusoma Maandiko, nami ningethamini kuwa na funzo la Biblia. Nitakubali msaada wenu kwa shukrani.”

Mashahidi wa Yehova wanafurahi kuandaa msaada kama huo kwa watu kila mahali. Ikiwa ungependa mtu akutembelee nyumbani kwako ili kuzungumzia Biblia pamoja nawe, tafadhali andikia I.B.S.A., P.O. Box, 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki