Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 8/8 kur. 15-21
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • 1. Ni kitu gani ambacho hapo awali Yesu alikuwa amewaambia wanafunzi wake wasibebe wakihubiri ambacho baadaye aliwaambia wakibebe? (Luka 9:3; 22:35, 36)
Amkeni!—1996
g96 8/8 kur. 15-21

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapishwa kwenye ukurasa 21. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Ni kitu gani ambacho hapo awali Yesu alikuwa amewaambia wanafunzi wake wasibebe wakihubiri ambacho baadaye aliwaambia wakibebe? (Luka 9:3; 22:35, 36)

2. Mbali na damu, taifa la Israeli pekee lilikatazwa lisile nini? (Mambo ya Walawi 3:17)

3. Gideoni alikuwa wapi wakati malaika wa Yehova alipomwagiza awe mwokozi wa Israeli? (Waamuzi 6:11-14)

4. Ni nabii yupi pekee, kati ya manabii wapatao 400, aliyemwambia Mfalme Ahabu ukweli kuhusu vita vyake dhidi ya Waashuru? (1 Wafalme 22:13)

5. Ni nini kilichokuwa kipimo cha vitu vikavu cha Waebrania cha kupimia mana ambacho kila Mwisraeli alipewa kila siku wakati wa safari yao ya miaka 40 jangwani? (Kutoka 16:16)

6. Jiji la Ninawi lenye uweza lilitabiriwa kwamba lingekuwa nini? (Sefania 2:13)

7. Musa alikufa juu ya kilima kipi baada ya kuona Bara Lililoahidiwa? (Kumbukumbu la Torati 32:49, 50)

8. Petro alilinganisha Wakristo wanaorudia njia zao za zamani za maisha na mnyama yupi ambaye hurudi kugaa-gaa matopeni baada ya kuoshwa? (2 Petro 2:22)

9. Mithali 23:27 hulinganisha kahaba na nini?

10. Ni waangalizi gani wawili wasafirio waliokuwa pamoja na Timotheo katika Korintho wakati salamu na kitia moyo zilipopelekewa kutaniko lililokuwa Thesalonike? (1 Wathesalonike 1:1)

11. Yakobo alisema ni nini ambayo Mungu hukubali kuwa “iliyo safi, isiyo na taka” maadamu mtu ‘anajilinda na dunia pasipo mawaa’? (Yakobo 1:27)

12. Ni mara ngapi kwa mwaka wanaume wote wa Waisraeli walipaswa ‘kutokea mbele za BWANA’ Yerusalemu? (Kumbukumbu la Torati 16:16)

13. Yesu alikula nini ili kuwathibitishia mitume wake kwamba wao hawakuwa wakiona roho Yesu alipowatokea baada ya kufufuliwa? (Luka 24:36-43)

14. Zaburi 146:3 husema usifanye nini, kwa kuwa wanadamu si chanzo cha wokovu?

15. Mtoto Musa alifichwa miongoni mwa mimea ya aina gani katika jitihada za kumwepusha asiuawe na Farao? (Kutoka 2:3)

16. Ni mungu yupi wa Wafilisti aliyedhilishwa mbele ya sanduku takatifu la Yehova? (1 Samweli 5:2-7)

17. Mungu huita kitu gani mahali “pa kuwekea miguu” yake? (Matendo 7:49)

18. Ni mti gani ulio nadra na wenye thamani ambao ulitumiwa katika ujenzi wa hekalu na vilevile katika ala za muziki? (1 Wafalme 10:12)

19. Ni farao yupi wa Misri aliyemwambia Mfalme Yosia, ambaye hakusikiliza na kuuawa, maneno “yaliyotoka kinywani kwa Mungu”? (2 Mambo ya Nyakati 35:22)

20. Mwanamke hufunguliwa kutokana na nini mume wake afapo? (Warumi 7:3)

Majibu ya Maswali

1. Mkoba

2. Mafuta

3. Katika Ofra

4. Mikaya

5. Pishi

6. Ukiwa na mahali pakavu kama jangwa

7. Kilima cha Nebo

8. Nguruwe

9. Shimo refu

10. Paulo na Silwano

11. Dini

12. Tatu

13. Samaki wa kuokwa

14. Kutumaini wakuu na wanadamu

15. Majani

16. Dagoni

17. Nchi

18. Msandali

19. Neko

20. Sheria yake

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki