Amkeni! Lilisaidia Kuokoa Uhai
Mmoja wa Mashahidi wa Yehova nchini Ekuado alipokuwa akingoja fundi amalize kutengeneza gari lake, mke wa huyo mekanika alimwambia huyo Shahidi kwamba alikuwa na wasiwasi kuhusu mwana wake mchanga, Byron. Alikuwa akifurukuta mara tano au sita kwa juma, na madaktari walishindwa kugundua ugonjwa wake. Byron hata alikuwa amepelekwa kwa wataalamu katika Quito, ambalo ni jiji kuu.
“Nilipokuwa nikizungumza na mama huyo,” Shahidi huyo akaeleza, “niliona mfanyakazi akipaka rangi gari, nikakumbuka makala fulani ya Amkeni! iliyohusu sumu ya risasi. Makala hiyo ilitaja kwamba moja ya dalili za kusumishwa na risasi ni kufurukuta. Nikamwambia mwanamke huyo nitamletea makala hiyo.”
Wazazi wa Byron waliposoma hiyo makala, walimpeleka mwana wao apimwe kama amesumishwa na risasi. Kiwango cha juu cha risasi kilipatikana katika damu ya Byron. Tiba na kuepuka risasi kukatokeza maendeleo makubwa katika afya ya Byron. “Hajafurukuta hata mara moja katika miezi minne ambayo imepita,” Shahidi huyo akasema. “Tayari baba yake ameongea na madaktari wengi kuhusu kisa hicho, naye sikuzote amelisifu Amkeni! kwa kuokoa uhai wa mwana wake. Sasa hata baadhi ya madaktari hao wanasoma Amkeni!
Tuna hakika kwamba wewe pia utanufaika kwa kusoma Amkeni! Ikiwa ungependa kupata nakala au ungependa mtu aje nyumbani kwako kuzungumza juu ya Biblia pamoja nawe, tafadhali andikia I.B.S.A., P. O. Box, 47788, Nairobi, au kwa kutumia anwani ihusuyo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.