Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/22 uku. 32
  • ‘Tafadhali Niletee Nakala 100’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Tafadhali Niletee Nakala 100’
  • Amkeni!—1996
Amkeni!—1996
g96 9/22 uku. 32

‘Tafadhali Niletee Nakala 100’

Hildegard, ambaye ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova aishiye Ujerumani, alimpa daktari wake wa magonjwa ya wanawake nakala moja ya toleo la Amkeni! la Februari 22, 1995. Gazeti hilo lilikuwa na mfululizo wa makala wenye kichwa “Uelewevu Mzuri Zaidi wa Komahedhi.”

Baadaye, binti ya Hildegard alipomzuru daktari uyo huyo, alipata kwamba alikuwa amesoma makala hizo. Daktari akaomba: “Tafadhali muulize mama yako kama anaweza kuniletea nakala mia moja.”

Magazeti hayo yalipopelekwa, daktari huyo akasema: “Usifikiri kwamba ninakuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Lakini makala hizi juu ya komahedhi ziliandikwa kwa njia nzuri sana hivi kwamba wagonjwa wangu wote wapaswa kuzisoma.”

Muda mfupi baadaye, Hildegard alisikia kwamba hilo gazeti lilikuwa limepokewa kwa utayari na wagonjwa wa huyo daktari. Mwanamke mmoja hata akasema kwamba hakufurahia tu kusoma makala za komahedhi bali vilevile makala nyinginezo katika gazeti hilo. Hivyo, Hildegard akapiga simu kwenye ofisi ya daktari kuona kama nakala nyinginezo zaidi zilitakikana. “Tunaweza kupata nyinginezo mia moja?” akauliza msaidizi wa daktari.

Ikiwa ungependa kupata nakala ya Amkeni! au ungependa kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A, P. O. Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ihusuyo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki