Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 1/22 uku. 32
  • Kitabu Ambacho Kinapendwa Zaidi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kitabu Ambacho Kinapendwa Zaidi
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 1/22 uku. 32

Kitabu Ambacho Kinapendwa Zaidi

Books We Love Best, ni mkusanyo wa maelezo ya vijana kuhusu vitabu ambavyo wavipenda zaidi uliochapishwa karibu miaka mitano iliyopita katika California, Marekani. Kijana mmoja alichagua Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi kuwa kitabu alichokipenda zaidi. Mwandikaji huyo mchanga alieleza sababu:

‘Kitabu hiki kizuri sana kinazungumzia maswali na majibu ambayo vijana hujiuliza leo kama vile, “Mbona wazazi wangu hawanielewi?” “Je, nitumie dawa za kulevya au alkoholi?” “Nijueje kama ni upendo halisi?” “Wakati wangu ujao una nini?” “Vipi juu ya ngono kabla ya ndoa?” Hivyo ni baadhi ya vichwa vya sura katika kitabu hiki. Ninakipenda kitabu hiki kwa sababu si kwamba kina maswali ya kibinafsi tu bali huyajibu kwa njia rahisi inayoridhisha. Watoto wangekipenda.’

Alkoholi na dawa za kulevya vilitumiwa kama mifano ya vishawishi vinavyokabili vijana leo. ‘Magazeti na vipindi vya televisheni huonyesha vinywaji na alkoholi ambavyo hukushawishi uvitumie,’ alieleza kijana huyo. ‘Vijana na matineja wengine hukushawishi uvitumie. Hivyo si ajabu kwamba vijana huonekana wamechanganyikiwa juu ya kile wapaswacho kufanya. Kitabu hiki hujibu maswali ya aina hiyo. Basi sasa wajua kwa nini nakipenda kitabu hiki. Mama yangu nami hujifunza kitabu hicho pamoja kila Alhamisi. Sasa tumesoma nusu ya kitabu.’

Bila shaka wewe pia utafaidika sana kutokana na kichapo hiki chenye kurasa 320 ambacho kina picha zenye kuvutia. Ikiwa ungependa kupokea nakala ya kitabu hicho au ungependa kuwa na funzo la Biblia bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., P. O. Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ihusuyo katika ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki