Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 25. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ni rasi gani iliyoko pwani ya mashariki ya Krete ambayo Paulo aliabiri kuipitia akiwa njiani kwenda kesini Roma? (Matendo 27:7)
2. Musa alikuwa akifanya nini alipopatikana na binti ya Farao lililomfanya binti ya Farao amwonee huruma? (Kutoka 2:6)
3. Yesu alisema ni wangapi wangepata barabara iongozayo kwenye uhai? (Mathayo 7:14)
4. Kani ya utendaji ya Mungu ilikuwa ikifanya nini baada ya uumbaji wa dunia? (Mwanzo 1:2, NW)
5. Baada ya kupaka miguu ya Yesu mafuta yenye marashi ya bei ya juu, Maria alitumiaje nywele zake? (Yohana 12:3)
6. Maandiko ya Kiebrania huwaitaje waume kuhusiana na wake zao? (Esta 1:20, NW)
7. Ni nini kilicho kipimo kikubwa zaidi cha Kiebrania cha uzani na cha thamani ya kifedha? (2 Wafalme 23:33)
8. Ingawa ilifanywa na Musa ili kuzuia watu kufa, nini alichoharibu Mfalme Hezekia kwa sababu kilikuwa kikiabudiwa katika wakati wake? (2 Wafalme 18:4)
9. Mwanamke wa Filipi aliyekuwa na ugumu wa kutatua jambo fulani na dada yake Mkristo Sintike aliitwa nani? (Wafilipi 4:2, 3)
10. Musa alitengeneza nini, kwa amri ya Mungu, ili kubeba mabamba ya mawe ya Sheria? (Kumbukumbu la Torati 10:1-5)
11. Ni miungu gani iliyoabudiwa na Waavi, ambao mfalme wa Ashuru aliwaweka katika Samaria baada ya kuwateka Waisraeli? (2 Wafalme 17:31)
12. Mtu “asemaye salamu” kwa mwasi-imani huwa nini kulingana na Maandiko? (2 Yohana 11)
13. Ingawa Wakorintho waaminifu walisemwa na Paulo kuwa “barua ya Kristo” iliyoandikwa mioyoni, ni nini ambacho anasema hakikutumiwa? (2 Wakorintho 3:3)
14. Ni katika ujirani wa jiji gani ambapo Samsoni alichochewa kwanza na roho ya Mungu na baadaye kuzikwa? (Waamuzi 13:25; 16:31)
15. Yesu alifananisha fundisho la Mafarisayo na Masadukayo na nini ambacho kilikuwa na athari ya kufisidi? (Mathayo 16:11, 12)
16. Kwa nini Yohana alitokwa na machozi wakati alipoona hati-kunjo yenye vifungo saba? (Ufunuo 5:1-4)
17. Ni jipi jina la pili la Esau, ndugu-pacha wa Yakobo? (Mwanzo 36:1)
18. Kwa nini Daudi alikuna-kuna mbao za mlango, mbele ya Mfalme Akishi wa Gathi na kuacha mate yaanguke juu ya ndevu zake? (1 Samweli 21:13)
19. Mwenyeji wa Gathi huitwaje? (2 Samweli 15:22)
20. Kwa nini Daudi alimsifu Yehova kwenye Zaburi 139:14?
21. Sehemu ya nyuma ya mashua huitwaje? (Marko 4:38)
22. Wazazi wa Musa waliweza kumficha kwa miezi mingapi baada ya kuzaliwa kwake? (Waebrania 11:23)
23. Yesu alimwita Shetani baba ya nini? (Yohana 8:44)
24. Hamani alifanya nini ili kuamua siku yenye heri ya kuharibu Wayahudi katika Milki ya Uajemi? (Esta 3:7)
25. Pamoja na mzeituni na mzabibu, ni upi ulio mmojawapo mimea mashuhuri sana ya Biblia? (Yohana 1:48)
26. Ni mahali gani ambapo Yonathani mwana wa Sauli alikubali kwamba Daudi angekuwa mfalme afuataye wa Israeli? (1 Samweli 23:16-18)
27. Ni nani aliyekuwa mtawala wa Uajemi ambaye alifunua hati iliyoandikwa na Sairasi na kuruhusu hekalu lijengwe upya? (Ezra 6:1-12)
28. Ni mnyama yupi mwenye uhusiano wa karibu na sungura lakini mkubwa? (Mambo ya Walawi 11:6, NW)
Majibu ya Maswali
1. Salmone
2. Akilia
3. Wachache
4. “Ikienda na kurudi juu ya uso wa maji”
5. Kuifuta miguu yake ili kuikausha
6. Wenye kumiliki
7. Talanta
8. Nyoka ya shaba
9. Euodia
10. Sanduku la agano
11. Nibhazi na Tartaki
12. “Mshiriki katika kazi zake mbovu”
13. Wino
14. Eshtaoli
15. Chachu
16. “Kwa sababu hakuna yeyote aliyepatikana kuwa astahili kufungua hiyo hati-kunjo au kutazama ndani yayo”
17. Edomu
18. Ili kumsadikisha mfalme kwamba alikuwa na kichaa na hivyo aponyoke
19. Mgiti
20. Kwa sababu ‘aliumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha’
21. Tezi
22. Mitatu
23. Uwongo
24. Aliamuru puri (kura) ipigwe
25. Mtini
26. Horeshi
27. Dario
28. Kitungule