Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 7/22 uku. 32
  • “Uniletee Arobaini. Nitazigawanya”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Uniletee Arobaini. Nitazigawanya”
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 7/22 uku. 32

“Uniletee Arobaini. Nitazigawanya”

Ikiwa sehemu ya kazi yao ya kuelimisha watu Biblia katika kusini mwa Ujerumani, Wolfgang na mkewe, Waltraut, mara kadhaa walimtolea mtu fulani nakala za Amkeni! Sikuzote alikuwa akikataa, akisema: “Tayari nina mengi sana ya kusoma.”

Hata hivyo, wenzi hao waliooana wakafikiri kwamba huenda ikawa mtu huyo aweza kusoma makala isemayo “Kuondoa Mawazo Yasiyo ya Kweli Kuhusu Mashahidi wa Yehova,” katika toleo la Amkeni! la Novemba 22, 1996. Hiyo makala ilihusu hotuba iliyotolewa katika Rotary Club huko California, Marekani.

Wolfgang alipofungua gazeti hilo kwenye ile makala na kumwonyesha mtu huyo, alianza kuisoma. Kisha akaomba abaki nalo. “Nitaisoma usiku nitakapokuwa nimetulia,” akasema.

Wolfgang na mkewe wakakutana na mtu huyo siku tatu baadaye. Aliitikiaje? “Hiyo makala ilikuwa yenye kupendeza sana,” akasema.

Kwa nini alivutiwa sana? Yaonekana kwamba alikuwa amekuwa na mawazo fulani yasiyo ya kweli kuhusu Mashahidi wa Yehova. Sasa alikuwa na uhakika kwamba marafiki wake wa Rotary Club wangefurahia kusoma makala hiyo. “Je, unaweza kupata nakala nyingi zaidi za hiyo makala?” akauliza.

“Unataka ngapi?” Waltraut akauliza.

“Uniletee arobaini. Nitazigawanya.”

Ikiwa ungependa kuwa na nakala ya Amkeni! au ungependa kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani iliyo karibu zaidi na wewe iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki