Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 26. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ingawa Yehova aliruhusu maadui wake washinde watu wake wakati hawakuwa waaminifu, kwa nini baadaye alilipiza kisasi dhidi ya mataifa hayo? (Kumbukumbu la Torati 32:27; Isaya 64:2; Nahumu 1:2)
2. Raheli alimpa mwana wake wa pili jina jipi alipokuwa akifa wakati wa kuzaa? (Mwanzo 35:18)
3. Paulo alipolinganisha silaha za kiroho za Mkristo na zile za vita vya kimwili, alifananisha imani na nini? (Waefeso 6:16)
4. Daudi alipokuwa akimtoroka Mfalme Sauli, alipata kimbilio kwa mfalme yupi? (1 Samweli 27:2)
5. Ibilisi alimwahidi Yesu falme zote za dunia kwa kubadilishana na nini? (Luka 4:5-7)
6. Finehasi alichukua hatua gani ya haraka ambayo ilikomesha tauni iliyoua Waisraeli 24,000? (Hesabu 25:7-9)
7. Ni kwa kutumia maneno gani Ayubu alionyesha kwamba alikuwa ameponyoka kifo bila kitu, au karibu bila kitu? (Ayubu 19:20)
8. Ni mbao gani yenye rangi nyeusi-nyeusi ambayo mara nyingi hutumiwa na pembe za ndovu kwa vipambo? (Ezekieli 27:15)
9. Ni kwa sababu gani mfalme wa Ashuru Tiglath-pileseri alishambulia Siria, akateka Dameski, na kupeleka wahamishwa hao hadi Kiri? (2 Wafalme 16:7-9)
10. Baada ya kusikia kwamba mwana wake wa kwanza kupitia Bath-sheba alikuwa amekufa, Daudi alifanya nini lililowashangaza watumishi wake? (2 Samweli 12:21)
11. Yesu alikiita nini “taa ya mwili”? (Mathayo 6:22)
12. Yehova alisema atatumia nini kumwongoza Gogu hadi kwenye shambulio lake la mwisho juu ya watu wa Mungu? (Ezekieli 38:4)
13. Mikaeli yule malaika mkuu alibishana na Ibilisi kuhusu mwili wa nani? (Yuda 9)
14. Mungu aliandaa mmea gani ili umpe kivuli nabii Yona baada ya utume wake katika Ninawi? (Yona 4:6)
15. Kwa sababu alipendezwa sana Esta alipopata kuwa malkia, Ahasuero alifanyia nini majimbo yake? (Esta 2:18)
16. Ni nani aliyeshurutishwa kufanya utumishi wa kumsaidia Yesu kubeba mti wake wa mateso? (Luka 23:26)
17. Ni mzao gani wa Yuda ambaye, kwa kuwa hakuwa na wana, alimwoza binti yake kwa mtumishi wake Mmisri ili aendeleze uzao wake? (1 Mambo ya Nyakati 2:34, 35)
18. Kabla ya Raheli kufa wakati wa kuzaa, mkunga wake alimhakikishia nini? (Mwanzo 35:17)
19. Ni vitu gani vilivyotumiwa kumrembesha Esta pamoja na wanawake waliokuwa naye? (Esta 2:12)
20. Ni nani aliyezusha suala la mtu mwingine kuteuliwa mahali pa Yuda asiye mwaminifu? (Matendo 1:15-22)
21. Ni nani aliyekuwa baba ya Yezebeli? (1 Wafalme 16:31)
22. Ni wanaume gani wawili ambao Yehova aliwaweka kusimamia ujenzi wa tabenakulo? (Kutoka 31:2, 6)
23. Ni shauri gani alilotoa Yesu kuhusu kuapa ovyoovyo? (Mathayo 5:37)
24. Ni mmea gani wa viungo ambao ni Yesu pekee anaoutaja katika Biblia? (Mathayo 23:23)
Majibu ya Maswali
1. Kwa sababu ya jina lake takatifu—ili kuyanyenyekeza mataifa hayo yenye kiburi na majivuno
2. Benoni
3. Ngao kubwa
4. Mfalme Akishi wa Gathi
5. “Tendo la ibada”
6. Aliwachoma mwanamume huyo na mwanamke huyo kwa fumo
7. “Na ngozi ya meno yangu tu”
8. Mpingo
9. Alihongwa na Mfalme Ahazi wa Yuda
10. Aliacha kufunga na kuanza kula
11. Jicho
12. Kulabu katika mataya yake
13. Mwili wa Musa
14. Mtango
15. Msamaha
16. Simoni wa Kirene
17. Sheshani
18. Kwamba mwana wake angezaliwa akiwa hai
19. Mafuta ya manemane na manukato
20. Petro
21. Ethbaali, mfalme wa Wasidoni
22. Bezaleli na Oholiabu
23. “Acheni tu neno lenu Ndiyo limaanishe Ndiyo, La yenu, La”
24. Mnanaa