Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 10/22 uku. 32
  • Yeye huthamini sana Mnara wa Mlinzi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yeye huthamini sana Mnara wa Mlinzi
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 10/22 uku. 32

Yeye huthamini sana Mnara wa Mlinzi

“Hata ingawa mimi ni Mkatoliki wa Kiroma,” akaandika mwanafunzi mmoja wa darasa la sita kutoka Toledo, Ohio, Marekani, “ningependa kufanya andikisho la gazeti lenu zuri. Sababu iliyonifanya nipendezwe na Mnara wa Mlinzi ilikuwa Trevor. Yeye huketi kando yangu darasani. Tumekuwa marafiki kwa karibu mwaka mmoja sasa, na amenifunza mambo mengi kuhusu Yesu, Yehova, na Mashahidi wa Yehova.

“Tuna umri sawa na urefu sawa na Trevor, na yeye ameshikamana sana na dini yake. Ana andikisho la Mnara wa Mlinzi na aliniazima gazeti lake moja. Nilipenda makala zenye kupatana na akili ambazo ninyi huandika. Natumaini mtaniruhusu niwe na andikisho la gazeti lenu hata ingawa mimi si mmoja wa Mashahidi wa Yehova.”

Kote ulimwenguni gazeti gazeti lenu na gazeti-jenzi Amkeni!, husomwa kwa furaha na watu wa mataifa mengi na dini nyingi. Mwaka jana pekee nakala zaidi ya milioni 900 za magazeti yote hayo mawili zilichapishwa kwa lugha zaidi ya 120!

Wewe pia waweza kufaidika kwa kusoma Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwa ukawaida. Ikiwa ungependa nakala au funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A. Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani inayohusu iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki