Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 11/8 kur. 31-32
  • “Shukrani Zangu kwa Mashahidi kwa Ajili ya Jumamosi Nzuri Ajabu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Shukrani Zangu kwa Mashahidi kwa Ajili ya Jumamosi Nzuri Ajabu”
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 11/8 kur. 31-32

“Shukrani Zangu kwa Mashahidi kwa Ajili ya Jumamosi Nzuri Ajabu”

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA NORWAY

Eivind Blikstad, mwandikaji wa makala za gazeti la kila siku la Norway Telemark Arbeiderblad, alitanguliza makala yake kwa kichwa kilichopo hapo juu. Kwanza, alionyesha jinsi anavyoudhika na barua za uuzaji, mauzo kupitia simu, na ziara zisizotakiwa—hasa Jumamosi asubuhi. Kisha akaandika:

“Kwa ghafula, wakawasili. Mlangoni pangu. Mashahidi wa Yehova. Jumamosi asubuhi. Wakiwa na gazeti lao la Amkeni!, Na. 17, la Septemba 8, 1996. [“Wahindi wa Amerika—Wakati Wao Ujao Una Nini?”] Waliniuliza kama ningependa kusoma gazeti hilo kwa sababu waliamini lilikuwa na jambo ambalo lingenipendeza. . . . Kabla sijapata nafasi ya kusema sipendezwi, mmoja wao akaongezea: ‘Kuna makala kuhusu Wahindi wa Amerika. Tunajua kwamba umekuwa ukiandika mengi kuhusu habari hii.’

“Pale nilinaswa. Kwa kuwa fahari ya mtu iamshwapo, azimio lako la mbeleni la kufukuza Mashahidi hutoweka. Nikiwa nimerudi ndani kwenye meza ya kifungua-kinywa, nashikwa na udadisi. Kwa kweli Mashahidi wa Yehova na wakati ujao wa Wahindi wa Amerika ni uhusiano usio wa kawaida. Nilivaa miwani zangu na kuanza kusoma. Nilikuwa na mwelekeo wa kwamba kulisoma ni kupoteza tu wakati.

“Kwa ufupi, makala ambayo Mashahidi wanatoa kuhusu hali ya Wahindi wa Amerika haikuwa nzuri tu—bali bora sana. Napendekeza kwamba walimu wa shule wa Norway waache ubaguzi wao. Agizeni makala kwa kila mmoja katika madarasa yenu! Matumizi ya vyanzo vya marejezo ni kielelezo bora, na uandikaji wenye kunufaisha walimu ni wazi kabisa. Pia inafuatia haki kabisa katika masuala ambayo maoni ya Wahindi yatofautiana na ya Mashahidi. Hakuna dalili za udanganyifu. Tatizo moja katika maeneo kadhaa yaliyotengewa Wahindi lahusu kuanzishwa kwa majumba ya kamari. Hizi hutokeza kazi za kuajiriwa zinazohitajiwa sana, lakini pia kuna hatari za kiadili. Swali hilo limeshughulikiwa kwa ustadi katika njia ya kwamba msomaji apata ufahamu wenye kina wa linalomaanishwa na kuwa Mhindi katika karne yetu.”

Blikstad amalizia: “Nikiwa nimeburudika kutokana na usomaji wangu, nilisoma sehemu iliyobaki ya Amkeni! Kama bakshishi, kulikuwa na makala yenye kugusa moyo sana kuhusu kufungwa kwa makanisa madogo na makubwa katika bonde la uchimbaji wa madini la Rhondda, kule Wales. . . .

“Je, nimepoteza kabisa uwezo wangu wa kufanya uamuzi vizuri? Je, mimi niliye mwatheisti, nimekubali itikadi za Mashahidi bila vipingamizi? . . . Si leo. Twahitaji vikumbusha vya daima juu ya umuhimu wa kung’oa magugu ya ubaguzi. Wakati ujao nitakaposikia Mashahidi wameshtakiwa kwa kusema uwongo, angalau ninajua ya kwamba hawakusema uwongo kuhusu Wahindi.”

Kwa sababu ya mahitaji ya pekee ya toleo la Amkeni! juu ya Wenyeji wa Amerika, nakala za ziada 37,000 zilichapishwa kwenye matbaa ya Watchtower Society ya New York. Kutaniko moja katika Arizona liliagiza 10,000 za kueneza kipekee eneo lao.

Ikiwa ungependa kuchunguza Mashahidi wa Yehova bila kubagua, tafadhali uwe huru kuandikia wachapishaji wa gazeti hili, ukitumia anwani ya karibu zaidi iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5, au piga simu kwenye Jumba la Ufalme la kwenu. Hakuna masharti, hakuna gharama. Utapata majibu manyoofu tu.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Uso wa Mhindi: D. F. Barry Photograph, Thomas M. Heski Collection; Mhindi achezaye dansi: Men: A Pictorial Archive from Nineteenth-Century Sources/Dover Publications, Inc.; mahema ya Wahindi: Leslie’s; michoro ya mstatili: Decorative Art; michoro ya mviringo: Authentic Indian Designs

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki