Ukurasa wa Pili
Magonjwa ya Kuambukiza—Je, Yataisha Wakati Wowote? 3-10
Yajapokuwa maendeleo ya kitiba na ya sayansi, magonjwa ya mlipuko na maradhi yaendelea kuongezeka. Je, magonjwa ya kuambukiza katika karne hii ya 20 yatimiza unabii wa Kibiblia kuhusu wakati wa mwisho? Je, tutapata ulimwengu usio na ugonjwa wakati wowote?
Njia Sita za Kulinda Afya Yako 11
Soma juu ya hatua sita uwezazo kuchukua ili kujilinda mwenyewe na familia yako dhidi ya vijidudu viwezavyo kusababisha ugonjwa.
Ghadhabu za Barabarani—Waweza Kukabilianaje? 21
Kukasirika na ujeuri unaotokea kati ya madereva ni tatizo linaloendelea kukua. Waweza kufanyaje ili ujilinde dhidi ya ghadhabu za barabarani?