Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Alipokuwa akishutumu waandishi na Mafarisayo, ni nani ambaye Yesu alisema “[aliuawa] kimakusudi kati ya patakatifu na madhabahu”? (Mathayo 23:35)
1. Alipokuwa akishutumu waandishi na Mafarisayo, ni nani ambaye Yesu alisema “[aliuawa] kimakusudi kati ya patakatifu na madhabahu”? (Mathayo 23:35)
2. Mwana mzaliwa wa kwanza wa Benyamini alikuwa nani? (Mwanzo 46:21)
3. Ni kuhani yupi wa Kiaroni aliyejulikana kuwa mnakili stadi na mwalimu wa Sheria? (Nehemia 8:1, 2)
4. Lazima mtu awe nini machoni pa ulimwengu ili awe mwenye hekima kwelikweli? (1 Wakorintho 3:18, 19)
5. Sehemu yenye kuning’inia ya sikio yaitwaje? (Mambo ya Walawi 14:14)
6. Paulo alisema kupenda fedha hutokeza nini? (1 Timotheo 6:10)
7. “Sakafu” ya gari la kimbingu katika ono la Ezekieli ilifanana na nini? (Ezekieli 1:22)
8. Ghuba ambayo mabaharia walihofu meli yao ingepanda mwamba walipokuwa wakimpeleka Paulo Roma akiwa mfungwa iliitwaje? (Matendo 27:17)
9. Fimbo ya Aroni ilitoka katika mti gani? (Hesabu 17:8)
10. Loti alilinda wageni wake kwa kadiri gani kutoka kikundi chenye ghasia? (Mwanzo 19:6-8)
11. Jina la Biblia la jiji la Misri Memphis ni jipi? (Isaya 19:13)
12. Paa mwekundu wa kike anaitwaje? (Mithali 5:19)
13. Ni wadudu gani waitwao “watu” kwa sababu ya utaratibu wao wa ushirikiano ulio tata kwa kadiri? (Mithali 30:25)
14. Ni nani aliyekuwa baba Mkanaani wa mke wa Yuda? (Mwanzo 38:2)
15. Uzao mvyauso wa punda-dume na farasi wa kike anaitwaje? (2 Samweli 13:29)
16. Ni nini kinachosemwa kuwa “chukizo kwa BWANA”? (Mithali 12:22)
17. Eliya aliambiwa kwamba watu 7,000 katika Israeli hawakuwa wamemwinamia mungu yupi asiye wa kweli? (1 Wafalme 19:18)
18. Ni neno jipi limetumiwa kutafsiri neno la Kiebrania na la Kigiriki Sheoli na Hadesi, likitokeza vurugu kuhusu kinachowapata wafu? (Matendo 2:31, King James Version)
19. Ni nani aliyemdhania vibaya Hana kuwa amelewa? (1 Samweli 1:13)
20. Katika kutaniko la Roma ni nani ambaye Paulo alimwita “aliye mkubaliwa katika Kristo”? (Waroma 16:10)
21. Ni mtume yupi ambaye maelezo yake mengi yalirekodiwa katika Gospeli kuliko yeyote kati ya wale wengine 11? (Mathayo 15:15)
22. Ni kwa kutangaza nini ndipo Paulo alipoponea kupigwa mjeledi? (Matendo 22:25-29)
23. Ni manukato gani ya aina mbili ambayo Nikodemo alitumia kuutayarisha mwili wa Yesu kwa ajili ya maziko? (Yohana 19:39)
24. Ni watu wangapi wenye ukoma ambao Yesu aliwaponya katika pindi moja ambapo mmoja tu ndiye aliyerudi kumshukuru? (Luka 17:12-19)
25. Sheria ilishutumu kutaja uovu juu ya mtu mwenye taabu gani, kwa kuwa hangeweza kujitetea? (Mambo ya Walawi 19:14)
Majibu ya Maswali
1. “Zekaria mwana wa Barakia”
2. Bela
3. Ezra
4. Mpumbavu
5. Ncha ya sikio
6. “Mambo mabaya,” kutia na ‘kuongozwa kupotea njia kutoka kwenye imani’
7. “Rangi ya bilauri”
8. Sirtisi
9. Mlozi
10. Aliwatolea binti zake
11. Nofu
12. Ayala
13. Chungu
14. Shua
15. Nyumbu
16. Midomo ya uwongo
17. Baali
18. Hell
19. Kuhani wa cheo cha juu Eli
20. Apelesi
21. Petro
22. Kwamba alikuwa Mroma
23. Manemane na udi
24. Kumi
25. Uziwi