Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 28. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ni nani aliye mpinzani mkuu wa Yehova? (Ufunuo 20:2)
2. Ingawa “Yehova” ndiyo matamshi yanayojulikana zaidi katika Kiswahili ya jina la Mungu, wasomi Waebrania hupendelea nini?
3. Mwana mzaliwa wa kwanza wa Abrahamu, Ishmaeli alifanya kazi gani ili ajitegemeze nyikani? (Mwanzo 21:20)
4. Ukosefu wa nani wa kumwonyesha staha baba yake ulitokeza laana kwa mwana wake? (Mwanzo 9:22-25)
5. Akiwa bila nia ya kumwachilia aende, Solomoni aliahidi kutoa mapambo ya aina gani kwa mwanamwali Mshulami? (Wimbo Ulio Bora 1:11)
6. Musa aliliona Bara Lililoahidiwa kutoka mahali gani, ijapokuwa hakuruhusiwa kuliingia? (Kumbukumbu la Torati 3:27)
7. Sehemu zote mbili za ndani na za nje za safina ya Noa zilifunikwa kwa kutumia nini? (Mwanzo 6:14)
8. Paulo alisema lazima tufanye nini ili “tukimbie kwa uvumilivu shindano la mbio lililowekwa mbele yetu”? (Waebrania 12:1)
9. Ni nani aliyefanya ufufuo wa kwanza uliorekodiwa? (1 Wafalme 17:21-23)
10. Kulingana na maneno ya Yesu, kwa nini divai mpya haiwekwi ndani ya viriba vikuukuu vya divai? (Marko 2:22)
11. Ni rekodi gani inayopatikana katika Mwanzo sura ya 6 hadi 9? (Mwanzo 6:9)
12. Kwa kuongezea dhahabu, fedha, na pembe za tembo, ni aina gani mbili za wanyama ambazo Solomoni aliingiza kutoka nchi za nje kila baada ya miaka mitatu ya safari za baharini za merikebu zake za Tarshishi? (1 Wafalme 10:22)
13. Ni nini kilichotokea wakati Mfalme Rehoboamu na Adoramu, ambaye alikuwa msimamizi wa shokoa, walipoingia eneo la mataifa ya kaskazini yenye kujitenga? (2 Mambo ya Nyakati 10:18)
14. Mungu anasema ni nini kilicho ‘kibago cha miguu yake’? (Matendo 7:49)
15. Ni nani aliyekuwa yatima wakati mama yake alipokufa akimzaa, baada ya kusikia ya kwamba mumewe alikuwa ameuawa? (1 Samweli 4:19-21)
16. Ni wale wanaokosa nini ambao Mungu ‘huwaongezea nguvu’? (Isaya 40:29)
17. Ilipotolewa kwa Mungu, ni nini ambayo haikupaswa kuwa na chachu au “asali”? (Mambo ya Walawi 2:11)
18. Mika alitabiri nini ambayo taifa lolote halingejifunza tena kamwe? (Mika 4:3)
19. Yesu alisema Neno la Mungu ni nini? (Yohana 17:17)
20. Baba ya Yona alikuwa nani? (Yona 1:1)
21. Mfalme Ahasuero alitolea nini majimbo aliyokuwa anamiliki katika kusherehekea kutawaza Esta awe malkia wake? (Esta 2:18)
22. Ni nini kilichofanywa ili kuonyesha kwamba mtumwa Mwebrania alichagua kwa kupenda kutoachwa huru bali abaki katika utumwa wa bwana wake? (Kutoka 21:5, 6)
23. Msamaria mwenye ujirani alimpeleka wapi yule mtu aliyejeruhiwa ili aweze kutunzwa? (Luka 10:34)
[Sanduku katika ukurasa wa 28]
Majibu ya Maswali
1. Shetani Ibilisi
2. Yahweh
3. Mpiga mishale
4. Hamu
5. “Mashada ya dhahabu” na “vifungo vya fedha”
6. Kilele cha Pisga
7. Lami
8. “Tuondoe kila uzito na dhambi ambayo hututatanisha kwa urahisi”
9. Eliya
10. Ngozi zitapasuka, na divai na vilevile ngozi itapotezwa
11. Historia ya Noa
12. Nyani na tausi
13. Adoramu alipigwa mawe hadi akafa, huku Rehoboamu akakimbia na kunusurisha uhai wake
14. Dunia
15. Ikabodi
16. Nishati yenye msukumo
17. Sadaka ya unga
18. Vita
19. Kweli
20. Amitai
21. Msamaha
22. Sikio lake lingetobolewa kwa uma
23. Hoteli ndogo