Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 3/22 uku. 31
  • Maji na Afya Yako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maji na Afya Yako
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Maji Ni Muhimu kwa Uhai
    Amkeni!—2003
  • Je, Maji Yanazidi Kupungua Ulimwenguni?
    Amkeni!—2001
  • Maji Yanayobubujika Ili Kutokeza Uzima wa Milele
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Sehemu Zenye Shida Zaidi
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 3/22 uku. 31

Maji na Afya Yako

“HUWEZI kutegemea kiu kikuamulie ni kiasi gani cha maji ambayo mwili wako wahitaji,” lataja gazeti Health. Lakini, kunywa maji mengi ni muhimu kwa hali njema yetu ya kimwili na kihisia-moyo, na hata kwa sura yetu. Miili yetu huendelea kupoteza maji kwa kutokwa jasho, machozi, na mikojo na vilevile kwa kupumua. Umajimaji huu uliopotezwa lazima urudishwe. Ni kiasi gani kinachohitajika? Wenye mamlaka wengi hupendekeza kunywa angalau glasi nane za maji—visaga viwili—kila siku.

Kwa nini? Maji ni muhimu kwa kusafirisha virutubishi ndani ya miili yetu na kuondoa uchafu. Ni ya muhimu katika kusawazisha ujoto wa miili yetu na kulainisha viungo vyetu. “Hata ukosefu kidogo sana waweza kukuacha ukijihisi mchovu . . . au mgonjwa,” lataja gazeti Health. “Ukosefu wa maji mwilini ni kisababishi cha uchovu ambacho hupuuzwa kwa kawaida.” Gazeti hilo lapendekeza: “Usidanganyike na namna ya umajimaji ya kahawa na chai, vinywaji vitamu vyenye kafeni, na alkoholi; kwa hakika hivyo huchangia ukosefu wa maji mwilini.” Kafeni na alkoholi hutenda kama dawa ya kukojoza na hufanya mwili upoteze maji.

Kwa kuongezea, “ngozi yako yahitaji maji ili idumu ikiwa nyororo na bila kukauka.” Ili kusaidia katika hili, viongeza-unyevu vyaweza pia kupakwa katika ngozi. Lakini haviongezi unyevu. Badala yake, hivyo huacha utando wenye kinga ambao husaidia kuhifadhi umajimaji ambao tayari upo kwenye ngozi. Kuhifadhi unyevu huu huwa wa maana zaidi kadiri umri usongavyo, kwani ngozi yetu hupoteza uwezo fulani wake wa kuhifadhi maji kadiri tuendeleavyo kuzeeka.

Kwa kusikitisha, katika maeneo mengi ya ulimwengu, jitihada kubwa zinahitajiwa ili kupata maji safi ya kutosha. Lakini jitihada hiyo yastahili kufanywa. Kwa wazi, kunywa maji mengi, na upate manufaa za njia hii sahili ya kufanya uonekane na kuhisi bora zaidi!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki