Daktari-Mpasuaji wa Moyo Apongeza Amkeni!
Amkeni! la Desemba 8, 1996, lilikazia mfululizo wa makala zenye kichwa “Maradhi ya Moyo—Ni Nini Kinachoweza Kufanywa?” Profesa Thomas Stegmann, mmoja wa madaktari-wapasuaji wa moyo aliye maarufu katika Ujerumani, na msimamizi wa idara ya kidari na mishipa ya damu, alisoma makala hizo na kuwaandikia wachapishaji kama ifuatavyo:
“Nilisoma kwa upendezi ripoti yenu juu ya maradhi ya moyo na, hasa, mishiko ya moyo. Nikiwa mtaalamu katika uwanja huu, nalazimika kuwaambia kwamba ufafanuzi wenu juu ya mishiko ya moyo na habari juu ya somo hilo zilikuwa nzuri sana—zikionyesha, kwa upande mmoja, uelewevu kwa mgonjwa mmoja-mmoja aliye na maradhi ya moyo na, kwa upande mwingine, simulizi sahihi la mambo ya hakika ya kitiba. Ufafanuzi huo huandaa maoni ya ujumla yanayofaa na habari iliyofanyiwa utafiti. Kuambatisha kwenu umaana wa pekee kwa utambuzi wa mapema wa dalili za mshiko wa moyo kulikuwa kwa maana pia.
“Ijapokuwa jitihada za pamoja za sayansi ya kitiba na jamii kwa ujumla, mrundamano wa vitu vyenye mafuta-mafuta katika ateri—na hasa mshiko wa moyo—ni kisababishi cha kifo kilicho cha kawaida zaidi katika nchi za Magharibi. Nikiwa daktari-mpasuaji wa moyo ambaye hushughulika na mabadiliko makubwa ya mrundamano wa vitu vyenye mafuta-mafuta katika ateri (kufanywa kuwa ngumu, kudumaza, ufyonzaji wa gesi wa mishipa ya damu) kila siku na ambaye hutibu maradhi haya kwa kutumia njia za namna mbalimbali za upasuaji wa moyo, ninajua jinsi ufafanuzi ulio wa kweli na mambo ya hakika ulivyo wa maana kwa watu—na pia kwa mtu anayeweza kuwa mgonjwa.
“Niruhusuni nitoe pongezi zangu changamfu kwa njia ambayo mmefafanua somo hili—pamoja na matumaini ya kuwa makala yenu itaweza kupatikana kwa watu wengi iwezekanavyo.”
Ikiwa ungependa kusoma Amkeni! kwa ukawaida au mtu fulani akutembelee ili kuongoza funzo la Biblia nyumbani pamoja nawe bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ihusuyo katika ukurasa wa 5.