Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 4/22 uku. 32
  • Mwalimu wa Moscow Asaidiwa na Amkeni!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwalimu wa Moscow Asaidiwa na Amkeni!
  • Amkeni!—1998
Amkeni!—1998
g98 4/22 uku. 32

Mwalimu wa Moscow Asaidiwa na Amkeni!

Mwalimu mmoja aliandikia ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Urusi kusema kwamba anapanga kutumia makala kutoka katika gazeti la Amkeni! katika mafundisho yake ya shule. Yeye aeleza:

“Nahisi kwamba Amkeni! hunisaidia kupata nguvu mpya ya kuishi, hunihuisha, na huniweka huru kutokana na fikira zenye kushusha moyo. Nawashukuru kwa ajili ya makala nzuri ajabu kuhusu vita kati ya mwanadamu na vijiumbe-maradhi [toleo la Februari 22, 1996]. Nina hakika kwamba magazeti yenu huleta manufaa kwa kila nyumba iliyo nayo.” Aliongezea: “Ningependa sana kupokea Amkeni! . . . Bila shaka gazeti lenu laweza kunisaidia.”

Barua inayofanana na hiyo kutoka Stavropol, mji wenye idadi ya watu zaidi ya robo milioni, ulioko zaidi ya kilometa 1,000 kusini-mashariki mwa Moscow, yasema: “Ningependa kuagiza Amkeni! Muda mfupi uliopita nilipata nakala mbili za gazeti hili. Makala hizo zilionyesha uelewevu kwa matatizo ambayo watu hukabili. Nyingine zinaeleza mambo ambayo sikuwahi kusikia. Hii ndiyo mara ya kwanza nimepata maelezo halisi jinsi hiyo kuhusu mambo.”

Ikiwa ungefurahia kupokea nakala nyingine ya Amkeni! au ungependa mtu akutembelee nyumbani mwako ili kuzungumzia Biblia pamoja nawe, tafadhali andikia I.B.S.A. Box 47788, Nairobi, Kenya, au kwa anwani ihusuyo kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki