Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 24. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ni nani ‘waliopiga kelele kwa furaha’ Mungu ‘alipoweka jiwe la pembeni’ la dunia? (Ayubu 38:4-7)
2. Ufalme wa Mungu hautapatwa na nini kamwe? (Danieli 2:44)
3. Daudi alijilinganisha na nini ili kumwonyesha Sauli kwamba hakukuwa na haja yoyote ya Sauli kumwinda? (1 Samweli 24:14)
4. Malaika wa saba alimwaga bakuli lake la hasira ya Mungu juu ya nini? (Ufunuo 16:17)
5. Kwa nini wazao wa Yakobo wanaitwa Waisraeli? (Mwanzo 32:28)
6. Ni maji gani yenye chumvi nyingi zaidi duniani? (Ona Mwanzo 14:3.)
7. Kwa nini Wakristo wanahimizwa kusali “kuhusu wafalme na wote wale walio katika cheo cha juu”? (1 Timotheo 2:1, 2)
8. Ni usemi gani wa Kisemiti ambao Yesu aliutumia alipokuwa akimponya mwanamume kiziwi aliyekuwa na kizuizi cha usemi? (Marko 7:34)
9. Yesu alifanyia wapi muujiza wake wa kwanza? (Yohana 2:11)
10. Jina la pili alilopewa Esau lilikuwa jipi? (Mwanzo 36:1)
11. Yesu alitumia mnyama gani katika kielezi ili kuonyesha tamaa yake ya kukusanya Yerusalemu lisiloitikia? (Luka 13:34)
12. Ni metali gani itumiwayo kunoa vifaa vya metali iyo hiyo? (Mithali 27:17)
13. Katika njozi, Yohana alimwona Mwana-Kondoo na wale 144,000 wakiwa wamesimama wapi? (Ufunuo 14:1)
14. Ni nani aliyepelekea baraza linaloongoza katika Yerusalemu lile swali muhimu la kutahiriwa kwa wasio Wayahudi? (Matendo 15:2)
15. Jiji kuu la ufalme wa kaskazini wa makabila kumi ya Israeli lilikuwa gani? (1 Wafalme 16:29)
16. Nambari ya “hayawani-mwitu” ni gani? (Ufunuo 13:18)
17. Kwa nini malkia wa Sheba alisafiri kwenda Yerusalemu? (1 Wafalme 10:4)
18. Ni mfalme yupi wa Yudea aliyekuwa na bidii sana kwa ajili ya ibada safi hivi kwamba alimwondoa nyanya yake katika wadhifa wake kwa sababu alifanyiza “sanamu ya kuchukiza”? (1 Wafalme 15:13)
19. Malaika wa pili alimwaga bakuli lake la hasira ya Mungu ndani ya nini? (Ufunuo 16:3)
20. Ni nani aliyekuwa mfalme mwovu wa Israeli aliyemtendea vibaya Tifsa? (2 Wafalme 15:16)
21. Ni silaha gani iliyotupwa kwa ukawaida? (Yoshua 8:18)
22. Mwezi wa Ethanimu baada ya uhamisho wa Babiloni uliitwaje?
Majibu ya Maswali
1. Wana wa kimalaika wa Mungu
2. “Hautaangamizwa”
3. “Kiroboto”
4. Hewa
5. Kwa sababu Mungu alibadili jina lake liwe Israeli
6. Bahari ya Chumvi
7. “Ili tupate kuendelea kuishi maisha yaliyo shwari na matulivu”
8. Efatha (linalomaanisha “funguka”)
9. Kana
10. Edomu
11. Kuku
12. Chuma
13. Kwenye Mlima Zayoni wa kimbingu
14. Paulo na Barnaba
15. Samaria
16. 666
17. Ili kusikia hekima ya Solomoni
18. Asa
19. Bahari
20. Menahemu
21. Mkuki
22. Tishri