Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 12/8 kur. 14-19
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Majibu ya Maswali
Amkeni!—1998
g98 12/8 kur. 14-19

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 19. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Ni nani aliyeshurutishwa kusaidia Yesu kubeba mti wa mateso? (Mathayo 27:32)

2. Ni usemi gani aliotumia Mungu zaidi ya mara 90 kumwita nabii Ezekieli ili kukazia kwamba alikuwa mwanadamu tu? (Ezekieli 2:1)

3. Ni kifaa gani cha ukulima ambacho Yehova aliona kimbele kingeweza kutumiwa kama silaha, kama ionyeshwavyo katika Sheria? (Kutoka 21:18, NW)

4. Kusudi mpaji afaidike Paulo alisema kazi za hisani zapaswa kutegemea nini? (1 Wakorintho 13:3)

5. Yesu alitabiri Petro angefanya nini mara tatu siku hiyo kabla jogoo hajawika? (Luka 22:34)

6. Ni kabila gani la Israeli lililopokea urithi wao upande wa mashariki na wa magharibi wa Yordani? (Yoshua 13:29; 17:5)

7. Ili mtu awe mkubwa kwa kweli, Yesu alisema apaswa kujiendesha namna gani? (Luka 9:48)

8. Kwa nini Samsoni alichagua mke miongoni mwa Wafilisti? (Waamuzi 13:25–14:4)

9. Ingawa tayari watoto kumi wa Hamani walikuwa wameuawa, Esta aliomba nini? (Esta 9:13)

10. Watawala wakuu wa wilaya za mamlaka waliitwaje katika milki za Babiloni na Umedi? (Danieli 6:1)

11. Ili mwili uokolewe, Yesu alisema ni nini kitakachofanywa kwa siku za “dhiki kubwa”? (Mathayo 24:21, 22)

12. Alipokuwa akikaribia kufa, Yusufu aliwahakikishia wana wa Israeli jambo gani? (Mwanzo 50:24; Waebrania 11:22)

13. Ni nani aliyekuwa mwanzilishi na mfalme wa milki ya kwanza baada ya Furiko? (Mwanzo 10:8-12)

14. Mfalme Omri alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa nani kwa talanta mbili kabla hajakifanya kuwa jiji lake kuu? (1 Wafalme 16:24)

15. Ni katika jiji lipi ambapo Paulo na Barnaba walichukuliwa kimakosa kuwa miungu Hermesi na Zeusi? (Matendo 14:8-12)

16. Daudi na watu wake walipokuwa wakitoroka Yerusalemu baada ya uasi wa Absalomu, ni nani aliyekuwa akitembea kandokando ya kilima akiwatupia mawe na kuwarushia mavumbi? (2 Samweli 16:13)

17. Danieli alipokea njozi ya mng’ang’ano kati ya wafalme wa kaskazini na kusini kwenye kingo za mto upi? (Danieli 10:4)

18. Mnara wa Babeli ulijengwa wapi? (Mwanzo 11:2)

Majibu ya Maswali

1. Simoni wa Kirene

2. “Mwanadamu”

3. Jembe

4. Upendo

5. Angekana kwamba hamjui Yesu

6. Manase

7. “Aliye mdogo zaidi”

8. Alikuwa akitenda kwa kupatana na mwelekezo wa roho ya Mungu; ndoa ya namna hiyo ingemwandalia fursa ya kupigana dhidi ya Wafilisti

9. Kwamba, kama baba yao, watundikwe juu ya mti mbele za watu wawe fedheha

10. Maliwali

11. Siku hizo zitakatwa ziwe fupi

12. Kutoka kwao Misri na kuingia katika Bara Lililoahidiwa

13. Nimrodi

14. Shemeri

15. Listra

16. Shimei Mbenyamini

17. Hidekeli

18. Shinari

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki