Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 12/22 uku. 32
  • “Je, Watu Wote Watapata Kupendana?”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Je, Watu Wote Watapata Kupendana?”
  • Amkeni!—1998
Amkeni!—1998
g98 12/22 uku. 32

“Je, Watu Wote Watapata Kupendana?”

Wakati wa Oktoba na Novemba 1997, nakala zaidi ya milioni 300 za ile trakti yenye kurasa nne “Je, Watu Wote Watapata Kupendana?” zilienezwa ulimwenguni pote katika lugha zaidi ya 100. Maelezo mengi mazuri yalitolewa kuihusu, kutia ndani pitio hili lifuatalo juu yake katika Express-Times ya Easton, Pennsylvania, Marekani:

“Inataja vielelezo vya majirani wanaokosa kuonyeshana shauku—hata kuwindana, kama kule Bosnia-Herzegovina na Rwanda, ambako watu waliokuwa majirani kwa muda mrefu lakini ambao walikuwa wa makabila tofauti na dini tofauti waliuana.

“Ikigusia hali za nyumbani, inazungumzia wazee-wazee wakiishi peke yao bila kutembelewa na mtu yeyote, na picha moja ya umaana yaonyesha uso wa mwanamke mmoja akichungulia kwa hofu kupitia mwanya wa mlango uliofungwa kwa mnyororo.”

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Slovenia ilipokea ombi lifuatalo kutoka kwa chama cha The Philosophical Literature Club Impresie: “Kwa kusikitisha, Kanisa Katoliki ya Kiroma katika Slovenia, ndilo lina udhibiti wa kufafanua kweli ya kidini. Ili kufahamu kweli hizi za kidini kwa njia bora, twawaomba mtufanyie hisani kwa kutupelekea nakala 50 za trakti yenye kichwa “Je, Watu Wote Watapata Kupendana?” Inatupendeza kwa kuwa ni ya kipekee, si kwa yaliyomo tu, bali pia kwa sura yake ya kutokeza.”

Ikiwa ungependa kupata uthibitisho kwamba watu wanaweza kuishi kwa amani na upatano, tafadhali jaza na upeleke kuponi iliyoambatanishwa.

◻ Nipelekeeni nakala ya broshua Je! Kweli Mungu Anatujali?

◻ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki