Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 2/8 uku. 3
  • Je, Kweli Mungu Yuko?—Wanasayansi Fulani Wajibu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kweli Mungu Yuko?—Wanasayansi Fulani Wajibu
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Muumba Aweza Kufanya Maisha Yako Yawe na Maana Zaidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Chanzo cha Ulimwengu na Uhai Ni Nini?
    Amkeni!—2002
  • Ulimwengu Wetu Wenye Kustaajabisha—Je, Ulitokea kwa Nasibu?
    Amkeni!—2000
  • Je, Ulimwengu Ulitokea Wenyewe Tu, Au Uliumbwa?
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 2/8 uku. 3

Je, Kweli Mungu Yuko?—Wanasayansi Fulani Wajibu

PROFESA wa fizikia Ulrich J. Becker, wa Taasisi ya Tekinolojia ya Massachusetts alisema hivi alipokuwa akieleza kuhusu kuwapo kwa Mungu: “Ninaweza kuwapo namna gani bila muumba? Sifahamu jibu lolote lenye kusadikisha lililopata kutolewa.”

Je, hili lilipinga maoni yake ya kisayansi? Jibu la profesa huyo lenye kuamsha fikira lilikuwa, “Ikiwa ulitambua namna gurudumu moja katika ‘saa’ linavyozunguka—huenda ukakisia jinsi ambavyo mengine husonga, lakini huna haki ya kuita kisio hilo kuwa la kisayansi na ni afadhali ukose kujibu swali kuhusu ni nani aliyezungusha kinesi hicho.”

Kinyume na maoni ya wengine, wanasayansi wengi wanaostahiwa hawakatai wazo la kuwapo kwa Mungu—Mwanzilishi-Mwamba Mkuu aliyeumba ulimwengu wote mzima na mwanadamu.

Fikiria mifano miwili zaidi kuhusu hoja hii. Profesa wa hisabati John E. Fornaess, wa Chuo Kikuu cha Princeton, alipoulizwa maoni yake kuhusu kuwapo kwa Mungu, alijibu: “Ninaamini kwamba kuna Mungu na kwamba Mungu hutokeza umbile kwenye ulimwengu wote mzima kwa viwango vyote, kuanzia vitu vya msingi hadi viumbe hai hadi vikundi vingi vya nyota.”

Profesa wa fizikia Henry Margenau, wa Chuo Kikuu cha Yale, alisema kwamba amesadikishwa kuwa sheria za asili ziliumbwa na Mungu, akiongezea hivi: “Mungu aliumba ulimwengu wote mzima pasipo kitu katika tendo ambalo pia lilitokeza kuwapo kwa wakati.” Kisha akasema kwamba katika kitabu The Mystery of Life’s Origin, wanasayansi watatu wanaeleza kwamba Muumba ndiye mwenye kutoa ufafanuzi wenye kukubalika kuhusu chanzo cha uhai. Akiunga mkono maoni haya, mwastronomia Fred Hoyle amesema kwamba kuamini kuwa chembe ya kwanza ilijitokeza kwa nasibu ni sawa na kuamini kwamba chamchela inayopita kwa kasi kwenye uga wenye sehemu zilizotenganishwa za ndege aina ya Boeing 747 na zilizovurugika ingeweza kutokeza ndege aina ya Boeing 747.

Kwa majibu haya twaweza kuongezea maneno ya mwandikaji wa Biblia Paulo: “Sifa za [Mungu] zisizoonekana zaonwa waziwazi tangu uumbaji wa ulimwengu na kuendelea, kwa sababu zafahamiwa kwa vitu vilivyofanywa, hata nguvu zake za milele na Uungu.”—Waroma 1:20.

Naam, kweli Mungu yuko! Lakini sababu gani ameruhusu hali za ulimwengu za sasa zenye kusikitisha? Ni nini kusudi lake kwa dunia? Je, tunaweza kumjua Mungu wa kweli barabara?

[Blabu katika ukurasa wa 3]

“Ikiwa ulitambua namna gurudumu moja katika ‘saa’ linavyozunguka—huenda ukakisia jinsi ambavyo mengine husonga, lakini . . . ni afadhali ukose kujibu swali kuhusu ni nani aliyezungusha kinesi hicho”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki