Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 2/8 kur. 20-22
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Majibu ya Maswali
Amkeni!—1999
g99 2/8 kur. 20-22

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 22. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Kupitia roho ya Mungu, ni nini ambacho Wakristo wa karne ya kwanza wangeweza kufanya ambacho kingewasaidia kufundisha na kutumika kuwa ishara kwa wasioamini? (1 Wakorintho 12:30)

2. Njiwa alirudi kwa Noa akiwa na jani la mti upi? (Mwanzo 8:11)

3. Ni jina lipi la kijiografia linalosimamia kitu fulani kilicho sehemu ya kaskazini-magharibi ya Peninsula ya Sinai linalotajwa mara sita katika Biblia na ambalo lingeweza kuwakilisha ama jiji, eneo, ngome nyingi za mpakani, ama safu ya milima? (Mwanzo 25:18)

4. Yoabu alitumia nani kumsihi Mfalme Daudi kwa niaba ya Absalomu baada ya Absalomu kufukuzwa kwa miaka mitatu? (2 Samweli 14:4)

5. Ni nchi gani iliyokuwa ukingo wa mashariki mwa milki ya Mfalme Ahasuero? (Esta 1:1)

6. Katika unabii wa kurudishwa, ni miti gani iliyotabiriwa kuwa ingechukua mahali pa “michongoma” na “mibigili”? (Isaya 55:13)

7. Wayahudi walimshtaki Paulo kwa kitu gani mbele za Galio, prokonso wa Akaya, na kwa nini Galio alitupilia mbali kesi hiyo? (Matendo 18:12-17)

8. Biblia hufafanuaje hali ya wafu? (Matendo 7:60)

9. Ni nani waliokuwa wanaume wazee wawili ambao, ijapokuwa waliteuliwa kuwa sehemu ya wale 70 wa kusaidia Musa, hawakwenda kwenye hema ya kukutania? (Hesabu 11:14-17, 24-26)

10. Ni mji upi kwenye mpaka kati ya Efraimu na Manase uliopewa Efraimu, ilhali eneo linalouzunguka lenye jina hilo liligawiwa Manase? (Yoshua 16:8)

11. Ni zipi herufi nne za kwanza za alfabeti ya Kigiriki?

12. Kulingana na simulizi la Biblia, ni nini kilichotolewa dhabihu “siku ya kwanza ya keki zisizotiwa chachu”? (Marko 14:12)

13. Ni mwana yupi wa Yosia ambaye Farao Neko alimfanya kuwa mfalme wa Yuda na kumwita jina Yehoyakimu? (2 Wafalme 23:34)

14. Ni nini kilichomaanishwa Musa alipoitia baadhi ya damu ya mwanakondoo mume wa kuwekwa wakfu kwenye kidole gumba cha guu la kuume la Haruni na cha kila mmoja wa wana wake? (Mambo ya Walawi 8:22-24)

15. Ni nani aliyekuwa baba ya Yoshua? (Nehemia 8:17)

16. Ni nani aliyekuwa baba ya Yezebeli? (1 Wafalme 16:31)

17. Ni kabila gani lililopoteza washiriki wake 42,000 waliposhindwa kutamka neno la siri “Shibolethi”? (Waamuzi 12:1-6)

18. Ni kuhani mkuu yupi aliyemkemea Hana mwadilifu, akimhukumu kimakosa kuwa alikuwa amelewa? (1 Samweli 1:12-15)

19. Mwizi alitozwa nini chini ya Sheria ya Mungu kwa Israeli? (Kutoka 22:1-4)

20. Ni mti upi uliotumiwa sana katika ujenzi wa hekalu? (1 Wafalme 6:9-20)

21. Ni nini ambacho Mungu hawezi kufanya? (Waebrania 6:18)

22. Ni nani Mpinzani mkuu wa Mungu? (Zekaria 3:1)

23. Amosi aliona Yehova akishikilia nini mkononi mwake katika ono kuonyesha kwamba Israeli lilishindwa na jaribu la kuonyesha unyofu wa kiroho? (Amosi 7:7-9)

24. Kitabu cha Mithali chamlinganisha mwanamke asiye na akili na nini? (Mithali 11:22)

25. Yesu alituma wanafunzi wangapi kwenda kumchukua mwana-punda aliyemtumia kuingia Yerusalemu? (Marko 11:1)

Majibu ya Maswali

1. Kunena kwa lugha

2. Mzeituni

3. Shuri

4. Mwanamke mwenye hekima wa Tekoa

5. Bara Hindi

6. Msunobari na mhadesi

7. Kuongoza watu “kwenye sadikisho jingine katika kumwabudu Mungu.” Kwa sababu haikukiuka sheria ya Kiroma

8. Kama usingizi

9. Eldadi na Medadi

10. Tapua

11. Alfa, beta, gama, delta

12. Kafara ya Sikukuu ya Kupitwa

13. Eliakimu

14. Ili waweze kukazia uangalifu mgawo wao na kutembea kwa uthabiti kwa uwezo wao wote katika wajibu wao wa kikuhani wa kutoa dhabihu

15. Nuni

16. Ethbaali

17. Efraimu

18. Eli

19. Alilipishwa mara tano

20. Mwerezi

21. Kusema uwongo

22. Shetani

23. Timazi

24. “Pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe”

25. Wawili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki