Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 4/8 kur. 12-14
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • (Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika Maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 14. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
  • Majibu ya Maswali
Amkeni!—1999
g99 4/8 kur. 12-14

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika Maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 14. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Ni fungu gani la maneno linalotumiwa mara nyingi kurejezea jiji la Yerusalemu na wakazi wake? (Zekaria 9:9)

2. Paulo alipokuwa akirudi Antiokia, huko Siria baada ya kumaliza safari yake ya kwanza ya umishonari, alitoka Asia Ndogo kupitia mji upi wenye bandari? (Matendo 14:25, 26)

3. Watu wa ule ufalme wenye makabila kumi walipokuwa wakimchagua yule ambaye angekuwa mfalme wa sita wa Israeli, waligawanyika katika uchaguzi wa watu gani wawili? (1 Wafalme 16:21, 22)

4. Mfalme Balaki alimpeleka nabii Balaamu mahali gani pa tatu palipoinuka alipokuwa akijaribu kumfanya awalaani Waisraeli? (Hesabu 23:28)

5. Ni yupi kati ya wale wana 12 wa Yakobo ambaye jina lake humaanisha “Heri”? (Mwanzo 30:11, Zaire Swahili Bible)

6. Paulo alikata rufani kwa Kaisari yupi, ambaye baadaye alitoa amri auawe? (Ona Matendo 25:11, 21, kielezi-chini New World Translation of the Holy Scriptures With References.)

7. Ni nini kilichohitaji kuongezwa kwa kila kitu kilichotolewa kwa Yehova katika madhabahu? (Mambo ya Walawi 2:13)

8. Kulingana na unabii wa Yesu, ni kazi gani muhimu inayofanyika kabla ya mwisho wa mfumo huu wa mambo? (Mathayo 24:3, 14)

9. Nehemia alikamilisha mradi wake wa siku 52 wa kujenga upya kuta za Yerusalemu katika mwezi upi wa Kiyahudi? (Nehemia 6:15)

10. Kwa nini wanawake walirejea kwenye kaburi la Yesu siku ya pili baada ya mwili wake kulazwa humo na kaburi kufungwa? (Luka 23:55–24:3)

11. Solomoni alikamilisha ujenzi wa hekalu katika mwezi upi wa Kiyahudi? (1 Wafalme 6:38)

12. Daudi alifanya nini alipopata habari ya kwamba mwana wake wa kwanza aliyemzaa na Bath-sheba alikuwa amekufa? (2 Samweli 12:20-23)

13. Katika siku za Yesu, watu fulani-fulani walidhihirisha nguvu zinazopita zile za kibinadamu kwa uwezo gani? (Marko 5:3, 4, 15)

14. Kulingana na mtume Paulo, tunapata faida gani tunapokubali kuzoezwa na nidhamu? (Waebrania 12:11)

15. Tofauti na ndege wengine, ni ndege yupi ambaye macho yake mawili hutazama mbele, yakimwezesha kuona kitu kwa macho yote mawili kwa wakati uleule? (Zaburi 102:6)

16. Tofauti na mali za kilimwengu, ni nini kitakachokuwa chenye faida katika siku ya Mungu ya ghadhabu. (Mithali 11:4)

17. Tukiwa watumishi wa Mungu, Yesu alisema tunapaswa kuwa na mtazamo upi tunapofanya kazi tuliyogawiwa? (Luka 17: 9, 10)

18. Mfalme Asa alichukua hatua gani ya ujasiri kuhusu ile “sanamu ya kuchukiza kwa Ashera” aliyoifanya nyanya yake Maaka? (1 Wafalme 15:13 NW)

19. Kwa nini Yesu akawasihi sana wale waliolemezwa mizigo kuchukua nira yake juu yao? (Mathayo 11:30)

20. Musa aliliona Bara Lililoahidiwa akiwa wapi kabla hajafa? (Kumbukumbu la torati 32:49, 50)

21. Twapaswa kulionaje neno la Mungu la kiunabii, na kwa sababu gani? (2 Petro 1:19)

22. Ni mashahidi wangapi wanaohitajiwa ili kuthibitisha jambo? (2 Wakorintho 13:1)

Majibu ya Maswali

1. Binti Sayuni

2. Atalia

3. Tibni na Omri

4. Peori

5. Gadi

6. Nero

7. Chumvi

8. “Habari njema hii ya ufalme itahubiriwa katika dunia yote inayokaliwa”

9. Eluli

10. Kuuhifadhi mwili wake zaidi kwa mafuta na manukato.

11. Buli

12. Aliacha kufunga na kulia akaanza kula

13. Walikuwa wamepagawa na roho waovu

14. Itatoa “tunda lenye kufanya amani, yaani, uadilifu”

15. Bundi

16. Haki

17. Ya kwamba ni pendeleo nasi tunafanya tu yale tunayopaswa kufanya

18. Aliikata sanamu akaiteketeza, naye akamwondolea cheo chake asiwe “malkia,” au mama-malkia, katika ufalme

19. Hilo lingewaburudisha, kwa maana nira yake ni ya fadhili na mzigo wake ni mwepesi

20. Kilima cha Nebo

21. Kuwa jambo tunalopaswa kulikazia uangalifu, kwa kuwa limefanywa hakika zaidi na ni lenye kuaminika

22. Angalau wawili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki