Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 8/8 kur. 21-27
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Majibu ya Maswali
Amkeni!—1999
g99 8/8 kur. 21-27

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Yesu alifanya nini ili kuwafundisha mitume wake somo la unyenyekevu na kuwa tayari kutumikia bila upendeleo? (Yohana 13:12)

2. Maneno ya upendo ya mwandamani wa mchungaji Mshulami yalifananishwa na kivuli cha kupendeza cha mti gani? (Wimbo Ulio Bora 2:3)

3. Yakobo asema kwamba “namna ya ibada [ya mtu] ni ya ubatili” asipofanya nini kwa ulimi wake? (Yakobo 1:26)

4. Kazi ya mwisho kuripotiwa ya uumbaji wa kidunia wa Mungu ni gani? (Mwanzo 2:22; 3:20)

5. Ni nani aliyechochea jiji la Shekemu liasi dhidi ya Abimeleki, na hivyo kusababisha kuharibiwa kwa jiji? (Waamuzi 9:28)

6. Jina la Kiamori la Mlima Hermoni lilikuwa gani? (Kumbukumbu la Torati 3:9)

7. Waisraeli walipaaza kilio wakitaka nini huko jangwani, baada ya kuchoshwa na mana? (Hesabu 11:4)

8. Paulo alibadilisha mashua katika mji gani wenye bandari alipokuwa amechukuliwa kama mfungwa kutoka Kaisaria hadi Roma? (Matendo 27:5)

9. Ni mambo gani yenye kuchukiza sana ambayo Ezekieli aliyaona kwenye ono yakifanywa kwenye hekalu la Yerusalemu? (Ezekieli 8:9-16)

10. Ni sehemu zipi za ule mfano wa ndoto ya Mfalme Nebukadreza zilizokuwa zimefanyizwa kwa fedha? (Danieli 2:32)

11. Yesu alifanya nini viongozi wa Kiyahudi walipotaka kumpiga kwa mawe kwenye hekalu? (Yohana 8:59)

12. Musa alifanya nini uso wake ulipong’aa sana hivi kwamba Waisraeli hawangeweza kuutazama? (Kutoka 34:35)

13. Baba ya Musa alikuwa nani? (Hesabu 26:59)

14. Kwa kuwa Zelofehadi hakuwa na wana, Yehova aliagiza nini? (Hesabu 27:1-8)

15. Majirani Wanazareti waliwatambulisha ndugu za Yesu kuwa nani? (Marko 6:3)

16. Kwa habari ya barua kwa Filemoni, Paulo alifanya jambo gani ambalo halikuwa kawaida yake? (Filemoni 19)

17. Kwa nini Yeremia alinunua shamba wakati Wababuloni walipokuwa wakizingira Yerusalemu? (Yeremia 32:8-15, 44)

18. Roho mwovu alimwomba Yesu asimfanyie nini? (Luka 8:28-31)

19. Adamu aliwapa wanyama wote nini? (Mwanzo 2:20)

20. Ni mwanamke yupi asiyekuwa Mwisraeli aliyetenda kwa ujasiri na kumuua Sisera? (Waamuzi 4:21)

21. Wakorintho waliitwa “barua” iliyoandikwa kwa njia gani? (2 Wakorintho 3:3)

22. Petro alimfanyia Malko nini, akitumia upanga wake? (Yohana 18:10)

23. Mithali husema “mwana aliyeachiliwa” atamfanyia mama yake nini? (Mithali 29:15)

24. Mithali humlinganisha mwanamke mwenye sura nzuri asiye na hekima na nini? (Mithali 11:22)

25. Yesu alitoa onyo gani kukazia upumbavu wa kurudia mambo tuliyoacha nyuma? (Luka 17:31, 32)

Majibu ya Maswali

1. Aliosha miguu yao

2. Mtofaa [NW]

3. Asipouongoza kwa hatamu

4. Hawa

5. Gaali, mwana wa Ebedi

6. Seniri

7. Nyama

8. Mira

9. Kulikuwa na wazee 70 waliokuwa wakiabudu sanamu zilizochongwa ukutani, wanawake wakimlilia mungu wa Wababuloni Tamuzi, waasi-imani 25 wenye kuabudu jua

10. Kifua na mikono

11. Alijificha na kwenda kutoka hekaluni

12. Aliutia utaji

13. Amramu

14. Kwamba binti zake wapaswa kupewa urithi wa baba yao

15. “Yakobo na Yosefu na Yudasi na Simoni”

16. Aliiandika kwa mkono wake mwenyewe

17. Kuwa ishara ya kurudishwa ambako kungekuja wakati ambapo, baada ya miaka 70 ya uhamisho, mashamba yangenunuliwa tena katika Yuda

18. ‘Asimtese-tese’ na kumwagiza pamoja na roho waovu wenzake waende zao kuingia katika abiso

19. Majina

20. Yaeli

21. Juu ya mioyo, “kwa roho ya Mungu aliye hai”

22. Alikatilia mbali sikio lake

23. Atamwaibisha

24. “Pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe”

25. “Mkumbukeni mke wa Loti”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki