Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 9/8 uku. 32
  • Profesa Aliyemfunza Alivutiwa Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Profesa Aliyemfunza Alivutiwa Sana
  • Amkeni!—1999
Amkeni!—1999
g99 9/8 uku. 32

Profesa Aliyemfunza Alivutiwa Sana

MNAMO Mei 1998, kitabu kipya cha kurasa 192 chenye jalada nyepesi kinachoitwa Je, Kuna Muumba Anayekujali? kilianza kutolewa katika nchi nyingi ulimwenguni pote. Hivi sasa, zaidi ya nakala milioni kumi zimechapishwa katika lugha 33. Watu wengi wamethamini kichapo hiki chenye kuimarisha imani.

Mwanafunzi mmoja muuguzi kutoka South Carolina, huko Marekani, alisema hivi kwa mshangao kuhusu kitabu hicho: “Sikuamini macho yangu nilipofungua sura ya 4 ya kitabu hicho kisha nikasoma nukuu kutoka kwa kitabu tunachotumia darasani!

“Jumatatu iliyofuata, nilimwuliza profesa aliyenifunza iwapo ningeweza kuzungumza naye kwa muda wa dakika moja tu. [Nilimpa] kitabu hicho nikamwambia kwamba nilijua angefurahia sana habari yake. Nilimwonyesha ukurasa wa 54 unaozungumzia ubongo. Alikisoma kimyakimya kisha akasema, ‘Ni kitabu cha kupendeza! Nitakichunguza.’ Baada ya kumpa nakala profesa aliyenifunza, niliwapa wanadarasa wenzangu wawili nakala walizoomba.”

Wewe pia waweza kuomba nakala ya kichapo hiki kilichofanyiwa utafiti kamili, na chenye uthibitisho wa kutosha kwa kujaza na kupeleka kuponi iliyopo hapa kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ihusuyo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nipelekeeni nakala ya kitabu Je, Kuna Muumba Anayekujali?

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Jalada: J. Hester and P. Scowen (AZ State Univ.), NASA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki