Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 10/8 kur. 11-14
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Majibu ya Maswali
Amkeni!—1999
g99 10/8 kur. 11-14

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 14. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Ni kabila gani la Israeli lililokuwa na idadi iliyopungua zaidi ya wale waliostahili kwa utumishi wa kijeshi—zaidi ya asilimia 60—watu walipohesabiwa mara ya pili huko nyikani? (Hesabu 1:23; 26:14)

2. Yesu alisema watu watakaofufuliwa hawatafanya nini? (Luka 20:35)

3. Aguri aliwaambia nani maneno yaliyoko katika Mithali sura ya 30? (Mithali 30:1)

4. Paulo alisema ni nini kinachohitaji kufanywa upya ili kufanya mapenzi ya Mungu? (Waroma 12:2)

5. Gamalieli alitoa mifano ya watu gani alipojaribu kushawishi Sanhedrini iache kuwasumbua Wakristo? (Matendo 5:34-40)

6. Yosefu alikusudia kufanya nini ili kuepuka kumfanya Maria awe “kitu cha kutazamwa na watu wote”? (Mathayo 1:19)

7. Kwa nini watu ‘waliokaa Lida na uwanda wa Sharoni . . . waligeuka kuelekea Bwana’? (Matendo 9:35)

8. Mafarisayo na Masadukayo walijaribuje kumshawishi Yesu? (Mathayo 16:1)

9. Yehova aliwafanya nini wale malaika waovu walioachilia mbali mahali pao wenyewe pa kukaa penye kufaa? (Yuda 6)

10. Mtu kuumbwa kwa mfano wa Mungu kulimaanisha nini? (Mwanzo 1:27)

11. Mungu alimaanisha nini aliposema kwamba dunia ni mahali pa kuweka miguu yake? (Isaya 66:1)

12. Kleopasi na mwanafunzi mwenzake walikuwa safarini kwenda wapi Yesu alipotwaa mwili uonekanao na kuandamana nao? (Luka 24:13)

13. Tunahakikishiwa nini endapo tutatembea “kwa ukamilifu”? (Zaburi 84:11)

14. Paulo na Akila walishirikiana katika jambo gani? (Matendo 18:3)

15. Mungu alitabiri Ishmaeli mwana wa Abrahamu angekuwa na wana wangapi? (Mwanzo 17:20; 25:16)

16. Kwa kufuata mwelekezo wa Farao ni “nafsi [ngapi] za nyumba ya Yakobo” zilizoingia Misri? (Mwanzo 46:27)

17. Yesu alifananisha wale wanaotendea mema mmoja wa wadogo zaidi sana wa ndugu zake na nani? (Mathayo 25:31-45)

18. Mungu hupewa cheo gani kutokana na herufi ya kwanza na ya mwisho ya alfabeti ya Kigiriki? (Ufunuo 1:8)

Majibu ya Maswali

1. Kabila la Simeoni

2. Hawataoa wala kuozwa

3. Ithieli na Ukali

4. Akili ya mtu

5. Theudasi na Yudasi Mgalilaya

6. Kumtaliki

7. Waliona kwamba Ainea alikuwa ameponywa na Petro kwa jina la Yesu

8. ‘Walimuuliza awaonyeshe ishara kutoka mbinguni’

9. Wamewekwa akiba “wakiwa na vifungo vya milele chini ya giza zito kwa hukumu ya siku kubwa”

10. Alikuwa na sifa zilizofanana na zile za Muumba wake na zilizomtofautisha na wanyama

11. Kitamathali, alimaanisha kwamba kiti chake cha ufalme kilicho mbinguni kiko juu kuliko dunia

12. Emausi

13. Ya kwamba Yehova ‘hatatunyima kitu [chochote] chema’

14. Kikazi walikuwa ni “watengeneza-mahema”

15. Kumi na wawili

16. Sabini

17. Kondoo

18. “Alfa na Omega”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki