India na China Zatishwa na Tumbaku
NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA INDIA
HUKU vikwazo dhidi ya utangazaji wa tumbaku vikiongezeka na elimu juu ya hatari za kiafya za kuvuta sigareti ieneapo katika nchi za Magharibi, makampuni makubwa ya tumbaku yanauza bidhaa zake upande wa Mashariki. Uchunguzi unaothaminiwa na Benki ya Dunia unatabiri kwamba idadi ya watu wanaokufa kila mwaka kutokana na tumbaku huko China huenda ikafikia milioni moja mwaka wa 2010. Jarida British Medical Journal lilitaarifu kwamba Wachina wapatao milioni 100 wenye umri unaopungua miaka 29 watakufa kwa sababu ya kuvuta sigareti.
Shirika la Afya Ulimwenguni linatabiri kwamba India, sawa na China—ikiwa na idadi ya watu ipatayo bilioni moja—inaelekea kukumbwa na “ongezeko kubwa na la haraka sana la magonjwa yanayohusiana na tumbaku.” Ripoti zinadai kwamba kila mwaka takriban watoto milioni 20 huanza kuvuta sigareti huko India. Mwanamume mmoja mkazi wa India Kusini alikuwa mvutaji sugu wa sigareti kwa miaka mingi. Aliwaandikia wachapishaji wa Amkeni! ili kuonyesha uthamini wake kwa ajili ya makala moja ya gazeti hilo iliyomsaidia kuacha kuvuta sigareti kabisa. Ilikuwa makala “Waweza Kuacha—Sisi Tuliacha!” katika toleo la Desemba 8, 1998.
Waweza kutoa sababu gani za kuacha kuvuta sigareti? Baadhi ya sababu zenye kuamsha fikira ziko katika ukurasa wa 25 wa broshua Mungu Anataka Tufanye Nini? yenye kurasa 32. Waweza kuomba nakala kwa kujaza na kupeleka kuponi iliyopo hapa kwa anwani iliyoonyeshwa au anwani inayohusu iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.
□ Nipelekeeni nakala ya broshua Mungu Anataka Tufanye Nini?
□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.