Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g02 1/8 uku. 26
  • Nzumari za Nyasi za Visiwa vya Solomon

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nzumari za Nyasi za Visiwa vya Solomon
  • Amkeni!—2002
  • Habari Zinazolingana
  • Ninapenda Muziki, Maisha, na Biblia
    Amkeni!—2007
  • Kinanda cha Mianzi—Ajabu ya Kimuziki ya Filipino
    Amkeni!—1994
  • Nyasi Si Mmea wa Kijani Tu Unaokua Katika Udongo
    Amkeni!—2002
  • Maisha Nyakati za Biblia—Wanamuziki na Vyombo Vyao vya Muziki
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2002
g02 1/8 uku. 26

Nzumari za Nyasi za Visiwa vya Solomon

Na mwandishi wa Amkeni! katika Visiwa vya Solomon

JE, UMEWAHI kujaribu kupiga nzumari? Unapovuta na kutoa pumzi inavyotakikana unaweza kushikwa na kizunguzungu. Lakini ebu wazia kupiga nzumari zenye urefu wa meta mbili na kipenyo cha sentimeta tano, huku ukisogeza mwili wako wote ili kutokeza muziki. Nzumari 40 za aina hiyo huunganishwa ili kutengeneza ala moja ya nzumari za nyasi za Visiwa vya Solomon. Ndiyo, kila nzumari katika ala hiyo imetengenezwa kwa nyasi! Nyasi tofauti-tofauti za misitu ya tropiki ya Visiwa vya Solomon, hutumiwa kutengeneza nzumari zenye sauti nyembamba kabisa hadi zile zenye sauti nzito kabisa.

Tutembelee ghala fulani huko Honiara, ambamo kikundi cha Narasirato Pipers hutengeneza ala zao na kufanya mazoezi kabla ya kufunga safari ya kwenda Taiwan ili kufanya maonyesho ya muziki huko. Ala fulani zina nzumari tatu zilizounganishwa, nazo hutokeza noti tatu zilizolinganishwa. Wanamuziki wanashika nzumari hizo tatu pamoja na kuzigonga kwenye jiwe tambarare ili kuhakikisha zinatokeza noti zinazolingana. Zisipolingana, wanakata sehemu ya mwishomwisho ya nzumari isiyo na noti sawa. Nzumari hizo tatu zilizounganishwa hazipulizwi. Kipande cha mpira hufungwa kwenye sehemu ya chini ya kila nzumari. Muziki hutokezwa wakati nzumari zote zilizounganishwa zinapogongwa ardhini. Ni sauti ya ajabu iliyoje!a

Ni vigumu kueleza muziki unaotokezwa na nzumari hizo. Nyakati nyingine zinatokeza sauti nyororo sana; na nyakati nyingine mshindo mkubwa sana. Wanamuziki wanapopiga ala hizo wanabadilishana mahali pa kusimama kulingana na mpangilio maalumu. Nyakati nyingine muziki huo unatia hofu, lakini kwa kawaida hufurahisha. Huenda utaweza kututembelea siku moja na kusikia nzumari za ajabu za nyasi za Visiwa vya Solomon!

[Maelezo ya Chini]

a Nzumari nyingine hutokeza muziki zinapogongwa na kipande kinene cha mpira.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki