Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/10 uku. 11
  • Amkeni! Liliokoa Uhai wa Mtoto Aliye Tumboni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Amkeni! Liliokoa Uhai wa Mtoto Aliye Tumboni
  • Amkeni!—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Biblia Inabadili Maisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Mnahitaji Kuwa na Uvumilivu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Desturi ya Kale ya Waamerika Wahindi
    Amkeni!—1996
  • Kuudhiwa Kingono—Naweza Kujilindaje?
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2010
g 2/10 uku. 11

Amkeni! Liliokoa Uhai wa Mtoto Aliye Tumboni

● Mwanamke mmoja nchini Mexico anayeitwa Anita, alikuwa na watoto watatu na alikuwa mjamzito tena.a Alimwambia mume wake kuwa hakutaka mtoto mwingine na alikuwa tayari kufanya lolote lile ili kutoa mimba hiyo. Hata alitishia kujiua! Wakati huo, Anita alikuwa anajifunza Biblia na Mashahidi wa Yehova lakini hakuwa akifanya maendeleo sana. “Nilikuwa na kiburi,” anasema Anita.

Shahidi aliyejifunza na Anita alimweleza kanuni za Biblia zilizohusika. Kwa mfano, alimwonyesha kwamba uhai wa mtoto aliye tumboni ni mtakatifu machoni pa Mungu. Katika Israeli la kale, ikiwa mtu angemwumiza mwanamke mwenye mimba, naye mwanamke huyo au mtoto wake aliye tumboni afe, Sheria ya Mungu ilisema kwamba mtu huyo angehukumiwa kuwa mwuaji. (Kutoka 21:22, 23)b Lakini Anita hakuchukua maneno hayo kwa uzito. Tayari alikuwa ameamua kutoa mimba hiyo.

“Mtu fulani aliniambia kwamba nikijidunga dawa fulani nitaharibu mimba hiyo,” akasema Anita. “Hivyo, nilinunua dawa hiyo na kumwomba rafiki yangu anidunge. Alifanya hivyo, lakini hakuna kitu kilichotokea. Baadaye nilijua kwamba hakutaka kushiriki kutoa mimba hiyo, badala ya kunidunga dawa hiyo aliibadili kwa siri na kunidunga maji safi.”

Lakini bado Anita alitaka kutoa mimba hiyo. Mwezi wa nne wa ujauzito alipata daktari aliyekubali kutoa mimba hiyo. Siku sita kabla ya siku aliyopaswa kwenda kwa daktari kutoa mimba hiyo, Shahidi aliyekuwa akijifunza naye alimpa makala moja ya gazeti la Amkeni! la Mei 22, 1980 (la Kiingereza) iliyokuwa na kichwa “Diary of an Unborn Child,” (Kitabu cha Kumbukumbu cha Mtoto Aliye Tumboni). Kumbukumbu hiyo ilimalizia kwa maneno haya: “Leo mama yangu aliniua.” Maneno hayo yalimshtua Anita sana na kumfanya alie kwa saa kadhaa. Anita anasema, “Habari hiyo ilinifungua macho.”

Anita alijifungua mtoto msichana mwenye afya nzuri. Anita anasema, “Leo, nina pendeleo la kumjua Yehova, ambaye ninampenda kwa moyo wangu wote.” Pia, anamfundisha binti yake Neno la Mungu ili yeye pia ampende Yehova. Binti yake naye anakubali waziwazi kwamba yuko hai kwa sababu ya Yehova—kwanza, kwa sababu yeye ndiye Chanzo cha uhai, na pili kwa sababu mafundisho yaliyo katika Neno lake, yaliyozungumziwa katika gazeti la Amkeni!, yaliokoa uhai wake.

[Maelezo ya Chini]

a Jina limebadilishwa.

b Maneno ya lugha ya awali yanarejelea kifo cha mama au mtoto.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki