Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 8
  • Watu Wakubwa Mno Duniani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Watu Wakubwa Mno Duniani
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Uasi Katika Makao ya Roho
    Roho za Wafu—Je! Zaweza Kukusaidia au Kukuumiza? Je Ziko Kweli?
  • Malaika—Jinsi Wanavyohusika Katika Maisha Yetu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Malaika—“Roho kwa Ajili ya Utumishi wa Watu Wote”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Msaada wa Malaika wa Mungu
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 8
Mwanamume mkubwa sana anataka kumpiga mwanamume mwingine

HADITHI YA 8

Watu Wakubwa Mno Duniani

IKIWA mtu angekuwa akikaribia kwako naye ni mrefu sana kama dari ya nyumba yenu, ungeona namna gani? Mtu huyo angekuwa mkubwa mno! Wakati mmoja kulikuwa watu wakubwa mno duniani. Biblia inaonyesha kwamba baba zao ni malaika waliotoka mbinguni. Lakini ilikuwa namna gani?

Kumbuka, Shetani malaika mbaya alikuwa akifanya matata. Hata alikuwa akigeuza malaika wa Mungu wawe wabaya. Mwishowe, malaika wengine walianza kumsikiliza Shetani. Waliacha kufanya kazi waliyopewa na Mungu huko mbinguni. Wakaja duniani na kujivika miili ya kibinadamu. Unajua sababu?

Biblia yasema wana hao wa Mungu waliona wanawake wazuri duniani wakataka kukaa pamoja nao. Kwa hiyo, wakaja duniani kuoa wanawake hao. Biblia inasema hilo lilikuwa kosa, kwa sababu Mungu aliumba malaika wakae mbinguni.

Mwanamume mkubwa sana anaiba chakula cha familia

Malaika hao na wake zao walipozaa watoto, watoto hao walikuwa tofauti. Kwanza labda hawakuonekana tofauti sana lakini walizidi kuwa wakubwa na nguvu sana, mpaka wakawa wakubwa mno.

Watu hao walikuwa wabaya. Na kwa vile walivyokuwa wakubwa mno na nguvu sana, waliumiza watu. Walijaribu kumlazimisha kila mtu awe mbaya kama wao.

Henoko alikuwa amekufa, lakini sasa kulikuwako mtu mmoja duniani aliyekuwa mzuri. Mtu huyo ni Nuhu. Sikuzote alifanya mapenzi ya Mungu.

Wakati mmoja Mungu alimwambia Nuhu kwamba wakati wake umefika wa kuharibu watu wote wabaya. Lakini Mungu alitaka kumwokoa Nuhu, jamaa yake na wanyama fulani wengi. Na tuone namna alivyofanya hivyo.

Mwanzo 6:1-8; Yuda 6.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki